Naomba ‘connection’ niwe utingo wa gari kubwa

Kwetu Tunduru

Member
Feb 7, 2023
16
57
Wakuu habari zenu,

Hongereni na majukum na poleni kwa yale magumu yanayotuandama.

Nimekuja kwenu wakulungwa. Kama Kuna dereva wa hizi gari kubwa, au kwa namna yoyote unahusika na hizi gari kubwa Kama msimamizi, dalali au vinginevyo, basi naomba unisaidie connection ya utingo hata Kama kutakuwa na kiingilio kidogo niko tayari kuchangia.

Lengo ni kuwa dereva wa gari hizo, ada ya veta Sina ndio maana naomba kuwa tingo wakulungwa.

Nawasilisha.
 
Hiyo pesa ya kiingilio jitahidi uijazie uende NIT ukasomee udereva wa malori.

Sasa hivi bila cheti cha NIT hupati Leseni has a za mabasi na hayo malori.

Hakuna short cut kwenye maisha, lielewe hili vizuri.
 
Onyesha alipotaka short cut kwenye maisha,

Mtu anatafuta kazi ya utingo,yupo tayari hata kutoa visent alivyonavyo ili apate hiyo kazi kisha apate hiyo hela ya kwenda huko NIT kisha wewe unamwambia hakuna short cut! punguza ujuaji jomba.
 
Hiyo pesa ya kiingilio jitahidi uijazie uende NIT ukasomee udereva wa malori.

Sasa hivi bila cheti cha NIT hupati Leseni has a za mabasi na hayo malori.

Hakuna short cut kwenye maisha, lielewe hili vizuri.
Mkuu Matola NIT pale anatakiwa dereva ambae tayari yuko competent sio anaejifunza.isitoshe,tofauti na veta hiyo ya kihonda hapo Morogoro ndio wanafundisha kiasi hizi gari kubwa ila hata hivyo nao baadae wanakutafutia mtu wa transit au unatafuta mwenyewe.
Sasa kwanini Mimi nisitafute kabisa ili nikishayaelewa kupata leseni na cheti iwe rahisi zaidi?
Madogo haya nayaendesha bila wasi.
Nawasilisha.
 
Hiyo pesa ya kiingilio jitahidi uijazie uende NIT ukasomee udereva wa malori.

Sasa hivi bila cheti cha NIT hupati Leseni has a za mabasi na hayo malori.

Hakuna short cut kwenye maisha, lielewe hili vizuri.
NIT hawafundishi kuendesha gari bali wanakutest kama unajua kuendesha gari then wanakupiga msasa hasa kwny suala la sheria za usalama barbaran, driving philosophy etc. Hvo yaaaan

Asije fikiria eti ukienda NIT unaanza kuelekezwa enhee kona ya semi trailer unakatia huku enhe hii inaitwa sprinter ina high na low enheeee ukifika hapa unamwaga upepo hakuuuuuuna ktu kama hcho NIT!!
 
Back
Top Bottom