Naogopa kumueleza Mke wangu ukweli kwamba nilichepuka

Habari Wana Jf wenzangu

Kuna jambo limenikuta Jana, wakati wa mida saa 4 napita kutokea kwenye mishe zangu pembezoni mwa bar moja hivi maarufu hapa Dar nikaitwa na rafiki mmoja hivi wa kike ambaye sikuonana nae muda kidogo nikaenda tukaa pale.

Binafsi sio mnywaji wa pombe tofauti na huyo dada yeye anapenda tukapiga story kazaa baada ya pale sikumbuki kilichoendelea nimejikuta nipo ghetto la huyo dada wakati nimemka leo asubuhi Tena nikiwa nipo uchi hata huyo dada hivyo hivyo.

Kwa mazingira hayo nivyoyaona sikutaka hata nimuulize je tumefanya mapenzi maana sikumbuki chochote kikichotokea kwanini nimekuwa na wasiwasi huyu demu mafaili yake nayajua ana list ndefu Sana na ameshawahi kudate na wasanii wawili maarufu wa hapa Bongo ambao wanajulikana kabisa kwakugonga Sana mademu.

Ukiachana na Hilo me nina mtu wangu ambaye ninaishi nae kama mke na Mume ninampenda Sana, ananiheshimu na mimi namuheshimu,ni mtu muhimu Sana kwenye maisha yangu yeye ni kama kiungo kwenye chakula.

Sijawahi kuchepuka wala sijawahi kufikiria hicho kitu kwa namna navyompenda mtu wangu nimeamka nimekuta missed call 4 zake kwenye simu yangu.

Ndugu zangu ninashindwa sijui nitamuambiaje mtu wangu na je nikimwambia ukweli ulivyo atanielewa kwa sababu binafsi sijadhamiria kufanya hivyo na sijui kilitokea kitu gani kikatokea hicho kitu.Naombeni ushauri wenu ndugu zangu nimwambie nini mke wangu anielewe.

to yeye
Zero IQ
Yna2
financial services
Darmian
Mzigua90
Carleen
Joanah
Amehlo
DeepPond
Watu8
joseph1989
Numbisa
Shunie
Usher-smith MD
Bujibuji Simba Nyanaume
Saint Anne

NB: Naomba tusiweke masiala kwenye issue sensitive kama unataka kufanya hivyo Bora tu usicomment kabisa kwenye uzi wangu nipo serious
HAhahahahhaha
 
Leo ndo nafahamu kuwa mwanaume anaweza kusex na asifeel kiashiria chochote cha kumuwezesha kujua kwamba alingonoka.
Anyway fuata ushauri wa wadau anza PEP kabla ya masaa 72 kupita huyo sexual partner ni high risk
Hlf ukute kaacha mimba humo weeeh
 
Mmh hakikisha mmeenda kupima ili mjue status ya afya zenu na kama mmojawapo atakutwa positive basi inabidi uanze kutumia PEP kabla hayajapita masaa 72 .

Pili wala haina haja ya kumwambia maana kama alikua anakuamini ndiyo hatokua akikuamini tena, ushafanya kosa basi jisamehe mwenyewe na usirudie kama kweli unampenda mwenzio.

Mwisho , ni kweli hukujitambua hadi unaenda nyumbani kwa huyo dada ? Unahisi uliwekewa madawa ya kulevya? Na kwanini? Kwamba una mkuyenge mtamu sana hadi dada wa watu akuleweshe na kukupeleka kwake?
 
Hapo chakumwambia ndio changamoto kumbuka sijalala home nimekuta missed 4 zake kwenye simu yangu na bado kanipigia mchana sijapokea unadhani nitamwambia nini anielewe?

Ila wanawake wana huruma sana, we naye una mwanamke ndani…. kwa uoga huu lazima huwa unachezea vitasa.
 
Tumia diplomasia, ikishindikana Tumia udikteta.

Njia zote Ni sahii na zinasolve tatizo lako kabisa
Kuna siku shemeji yangu hakulala kwake... Katafutwa kwa simu wapiii kesho yake anapiga simu asubh. kuulizwa eti nililala polisi...kulitokea kutoelewana mahali (kwenye pombe i think)

Siku ingine akasema nililelewa sana nikalala kwa dogo.(wakiume)

Sio mara 1 hii mambo.

Inabidi tu ukubali ht km sio kweli ila najua kbs alikua muongo yule
 
Hlf ukute kaacha mimba humo weeeh
Nasusa dada yangu Leo hata sijaenda kwenye mishe mishe yangu kabisa na teyari nipo now home nimemtaarifu kabisa mpenzi wangu kuna changamoto ingetokea akifika home nitamueleza zaidi maana yeye Mara nyingi anafika kuanzia saa 2 usiku
 
Mmh hakikisha mmeenda kupima ili mjue status ya afya zenu na kama mmojawapo atakutwa positive basi inabidi uanze kutumia PEP kabla hayajapita masaa 72 .

Pili wala haina haja ya kumwambia maana kama alikua anakuamini ndiyo hatokua akikuamini tena, ushafanya kosa basi jisamehe mwenyewe na usirudie kama kweli unampenda mwenzio.

Mwisho , ni kweli hukujitambua hadi unaenda nyumbani kwa huyo dada ? Unahisi uliwekewa madawa ya kulevya? Na kwanini? Kwamba una mkuyenge mtamu sana hadi dada wa watu akuleweshe na kukupeleka kwake?
Hilo swali ulizoniuliza kwenye paragraph la mwisho ni ngumu Sana kukujibu kuhusu mkuyenge wangu ni mtamu au vipi nadhani mwenye majibu sahihi ni huyo dada na kuhusu huyo dada kuniwekea madawa kulevya may be Unaweza ukawa sahihi au la hata mimi nilikuwa nalifikiri hili
 
Pole sana mkuu. Mimi kuna sista kila nikionana nae ananilazimisha kunywa sijui ndio mipango hii. Bahati mbaya naonana nae mara kwa mara kwa ishu za kikazi hivyo sitaki mambo yawe mengi vibe itakuwa weird.

Katafute PEP fasta kwanza kabla ya kuzungumza na huyo msichana ulielala nae. Huyo mtu wako hamna neno uwongo uko mwingi tu wa kutumia.
 
Hilo swali ulizoniuliza kwenye paragraph la mwisho ni ngumu Sana kukujibu kuhusu mkuyenge wangu ni mtamu au vipi nadhani mwenye majibu sahihi ni huyo dada na kuhusu huyo dada kuniwekea madawa kulevya may be Unaweza ukawa sahihi au la hata mimi nilikuwa nalifikiri hili
Am trying to think out loud, kama ulikua hujitambui hivo hata mkuyenge ulipata erection kweli? Kama ulipata aargh usituzuge ulienjoy show na kugugumia juu then unakuja unalalamika hukujitambua, kaongo sana wewe. 😂
 
kuna tukio kama hilo la kulala nje liliwahi mtokea jamaa yangu alichofanya yeye ni kuongea na askari wale wa defender wakampiga pingu wakaenda naye nyumbani kwake , walipofika wakamwambia mkewe walimkata jamaa toka jana yake anakunywa muda wa kazi akalazwa selo na wakitaka yaishe watoe elfu 50 yaishe na ndiyo mkewe mshikaji akalimaliza kwa kuwapa manjagu chao na jamaa yangu kupewa pole za kutosha na mkewe na ikawa ndiyo pona pona ya mshikaji na kuokoa ndoa yake.
Hyo mbinu itatumika in future inaokoa sna
 
Back
Top Bottom