Nanyaro azidi kufanya makubwa Kata ya Levelosi - Arusha

Nanyaro azidi kufanya makubwa Kata ya Levelosi - Arusha

Crashwise

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
22,227
Reaction score
8,760
Diwani wa kata ya Levelosi mhe. Nanyaro Ephata ameendelea kufanya makubwa ndani ya kata yake baada ya jana kukabidhi unga na sukali na kukagua ujenzi wa jiko la kisasa kwenye shule ya msingi Levelosi ikumbukwe mwenyezi uliopita hospitali ya Levelosi alifanikiwa kuipandisha hadhi na kuwa hospitali ya wilaya.
Baada ya kufanikiwa kuipandisha hadhi hospitali ya Levelosi na kuwa hospitali ya wilaya diwani Nanyaro ameendelea kufanya makubwa ndani ya kata ya levelosi baada ya jana kukabidhi unga na sukari kama kawaida kwaajili ya watoto wa shule hiyo kupata uji na walimu kupata chai.
Pia Diwani huyo alikagua ujenzi wa jiko la kupikia na kushuhudia walimu wakiahamia kwenye nyumba alizo zisimamia ..Akiongea na waandishi wa habari Mwalimu mkuu(Kaaya) wa shule hiyo alisema waalimu na wanafunzi wanamshukru sana diwani huyo kwa juhudi zake za kuhakikisha shule hiyo ina kuwa ya kisasa kabaisa kwani kwasasa kuna miradi zaidi ya mitano inaendelea shuleni hapo na miwili ikiwa imekamilika kwa 100% na mitano 70% kama mnavyoona kuna mradi wa thamni ya mil 12 wa kuvuna maji ya mvua ambao unaendelea kwa sasa huku chama chake kikiwa kimeahidi kupaka rangi mabati ya majengo yote ya shuleni hapo hii hijawahi kutokea alisema Mwalimu Kaaya
naye mwalimu Fred aliye pokea unga na sukali alisema wana mshukru Diwani huyu wa chadema kwa juhudi zake kwani sasa wanafunzi wanaafya na hata mahudhulio yameongezea sana ambalo ndiyo lilikuwa dhumuni la kuwapatia watoto uji.
DSC08180.JPG
Wanafunzi wa shule ya msingi Levelosi wakimsaidia Diwani wa kata hiyo Mhe. Nanyaro Ephata kushusha mifuko ya unga na sukari kutoka kwenye gari la diwani huyo.
DSC08187.JPG
Mhe. Nanyaro Ephata akikabidhi unga na sukari kwenye shule iliyopo kwenye kata yake ya Levelosi
DSC08197.JPG
Nanyaro kushoto na wa katikati ni mwalimu mkuu wa shule ya Levelosi.

DSC08202.JPG
DSC08203.JPG
Moja ya sehemu zinazotumika kwasasa kupikia uji...
DSC08200.JPG
Moja ya majengo ya kuishi waalimu yaliyojengwa na diwani huyu.
 
Hapa mimi ndio nasemaga chadema nitafauti sana nachama chochote chakisiasa hapa nchini yanatekelezwa yale yaliyo semwa. Big up Diwani tupo pamoja kuijenga Arusha
 
Hapa mimi ndio nasemaga chadema nitafauti sana nachama chochote chakisiasa hapa nchini yanatekelezwa yale yaliyo semwa. Big up Diwani tupo pamoja kuijenga Arusha

hakika ukichagua chadema umechagua maendeleo..
 
Kule Chalinze hayo majengo wangeita chuo kikuu. Hivi hatuwezi kufanya utaratibu Mtu kama Nanyaro anaazimwa labda kwenda Bagamoyo miezi 6 hivi anawaonyesha mbinu za maendeleo kisha anarudi? tusiwe wachoyo wa maendeleo, wale jamaa wanakichagua kile chama wengine ni kwa ajili ya zile kanga na t shirts tuu! Tusiwatelekeze ni wenzetu na msaada ni huo peleka kwa muda mtu kama Nanyato basi kitaeleweka na watajitambua
 
Kumbe watanzania tukiamua tunaweza! Ni mara yangu ya kwanza kuona nyumba za waalimu zilizo bora. Ongera Kamanda!

ni bora na bado bei nafuu lakini kama ingekuwa intarahamwe wangeongeza mara 16 kama wanavyofanya bei za ticket za ndeke na RAV 4 kwa mil 80..chezea intarahamwe akaa CCM wewe
 
Kule Chalinze hayo majengo wangeita chuo kikuu. Hivi hatuwezi kufanya utaratibu Mtu kama Nanyaro anaazimwa labda kwenda Bagamoyo miezi 6 hivi anawaonyesha mbinu za maendeleo kisha anarudi? tusiwe wachoyo wa maendeleo, wale jamaa wanakichagua kile chama wengine ni kwa ajili ya zile kanga na t shirts tuu! Tusiwatelekeze ni wenzetu na msaada ni huo peleka kwa muda mtu kama Nanyato basi kitaeleweka na watajitambua
Mkuu umenichekesha sana...
 
Diwani mdogo mwenye akili,upendo,uchapakazi mfano wa kuigwa ni huyu Nanyaro,hakika Arusha mna viongozi! Sisi huku singida madiwani yote hayafanyi kazi sijui kwa kua tumechagua ccm.
 
Hongera diwan wetu kwa kz nzur hayo ni matunda ya Mh lema kwa kuwaanda madiwan vzr, akili ya diwan mmoja ni sawasawa na akili za wabunge wa ccm 10 ndo zimfikie diwan wa chadema
 
Mkuu umenichekesha sana...
Mkuu umeniuzi sana! mie nasema kwa uchungu wewe unacheka? Unajua nani keshakuwa mbunge pale kwa miaka 15 na hali iko vile? Bahati mbaya niko na simu sasa baadae niitaweka picha ya shule za huko ndio badala ya kucheka utalia. Kuna shule shule huko Chalinze ofisi ya Mwalimu Mkuu haifikii ubora wa choo cha shule hiyo ya Nanyaro.
Btw acha nipate ya baridi hapa nawe endelea na nyama choma za A town hawa Chalinze fursa waliipata majuzi hawakutaka kuitumia
 
ni bora na bado bei nafuu lakini kama ingekuwa intarahamwe wangeongeza mara 16 kama wanavyofanya bei za ticket za ndeke na RAV 4 kwa mil 80..chezea intarahamwe akaa CCM wewe
Mkuu umetaja hiyo ya Rav4 milioni 80 mpaka nimepaliwa kabia kangu. Eti waziri naye bila aibu anasimama na kutetea. Hii ni nchi ya aina yake hapa duniani na sitashangaa siku moja Mtz akikutana na raia wa nje akijitambulisha wAtu wanaangua kicheko.
Baya zaidi wabunge wa CCM wakashangilia
 
Mkuu umeniuzi sana! mie nasema kwa uchungu wewe unacheka? Unajua nani keshakuwa mbunge pale kwa miaka 15 na hali iko vile? Bahati mbaya niko na simu sasa baadae niitaweka picha ya shule za huko ndio badala ya kucheka utalia. Kuna shule shule huko Chalinze ofisi ya Mwalimu Mkuu haifikii ubora wa choo cha shule hiyo ya Nanyaro.
Btw acha nipate ya baridi hapa nawe endelea na nyama choma za A town hawa Chalinze fursa waliipata majuzi hawakutaka kuitumia

nisamehe mkuu..
 
Mkuu umetaja hiyo ya Rav4 milioni 80 mpaka nimepaliwa kabia kangu. Eti waziri naye bila aibu anasimama na kutetea. Hii ni nchi ya aina yake hapa duniani na sitashangaa siku moja Mtz akikutana na raia wa nje akijitambulisha wAtu wanaangua kicheko.
Baya zaidi wabunge wa CCM wakashangilia

alipobanwa eti ni aina nyingine ila walizilabel RAV 4
 
Back
Top Bottom