Nani yuko sahihi?

Lady.A

JF-Expert Member
Dec 13, 2013
392
191
Habari zenu wakuu, Leo napenda kushare na nyinyi juu ya hili swala la lawama kwa pande zote mbili.

Siku hizi imezuka misemo utasikia eti "wanaume/wanawake walikuwa zamani bwana siku hizi hakuna kitu" kwani hawa wanawake/wanaume WA siku hizi wamezaliwa wapi na wamelelewa na akina nani?

Mawazo yangu ni kwamba, watu ni walewale tatizo ni kupanda mno kwenda na wakati mpaka tunajishangaa na kushangaana. Wewe mwanaume/mwanamke kwa nini usiwe Kama ulivyo? Kwa nn uwe na tamaa za ajabu na kukifanya kuwa sehemu ya maisha yako?

Na he kwa mtindo huu WA kulaumiana wanaume wanasema wanawake wamezidi na wanawake wanasema wanaume wamezidi, ni nani anadhani yuko sahihi?
 
Wanawake wamezidi kutoa mambo ya chumbani kuyaweka kibarazani na wamekuwa na ujasiri Wa maiaha unaowapoteza eti kuwa wanaweza kuishi bila kumtegemea mume

Ikiangalia hayo yote zamani hayakuwepo
 
Wanawake wa zamani walikuwa tegemezi lakini wana heshima...Hawa wa siku hizi ni tegemezi lakini wana jeuri/viburi
 
Na wanaume wazamani walikuwa sio tegemezi kwa wanawake tena walionyesha ujogoo haswa wa siku hizi wanalelewa kabisa kama mabinti.

Hao wanaowategemea wanawake ni wavulana siyo wanaume. Imeandikwa mwanamke atazaa kwa uchungu na mwanaume atakula kwa jasho.
 
Hakuna kilichobadilika zaidi ya wigo mpana wa kubadilishana mawazo na kupeperusha taarifa.

Kwa mfano, mtu anagombana na mkewe saa 5 usiku na kurusha taarifa JF, fb, Twitter, Insta n.k ndani ya dakika 15. Enzi zetu ungomvi ungeishia kwenye kuta nne!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom