Nani wameiba 480 billion Hazina?

Nani wameiba 480 billion Hazina?

Tunajiuliza nini wakati wezi ni maccm, hata kifo cha Mgimwa usikute ilikuwa ni kuficha ushahidi, ccm ni hatari mtanzania, endeleeni kujipendekeza, ili mtolewe kafara na wengine waendelee kufanya maisha.

Cc: Chris Lukosi
 
Na bado, wataiba hadi hicho kidogo ulichonacho wanakitaka....!!@Tz is perishing. Laana ya rushwa ilishaingia nchini sio rahisi kuiondoa, angalia hata vijana wa cku izi hata ww pia ukiwekwa pale utawaza kuiba tu afu waTZ tumekuwa wazembe wa kutaka sana mafanikio ya haraka pasipo kufanya kazi...! Ila msijali dhahabu haiwezi ng'ara pasipo kuiingiza motoni...! Jubilee imekaribia hawa majambazi wataumbuka haujapata kuona. Rais mwenyewe mwizi mkubwa unafikiri atakemea wizi...? pengine ndo sababu ya kumpoteza Mgimwa maana yule mzee alitaka kuwasemea kwa wananchi na hiyo ndio sababu ya rais wenu kuweka vilaza kwenye hiyo wizara ili wizi ufanyike kwa ufanic zaidi....! Ukiangalia mambo yake huyu jamaa(rais wenu) analipua lipua tu ili yy amalizie asepe zake amechukua chake.....!!Anyways tuendelee kutoa macho uku wenzetu wanakuwa mabilionea bila jasho.
 
Kama ni kweli inauma sana. Ukiangalia matatizo yanayotuzunguka kuna watu hawana uwezo wa kupata hata mlo mmoja. Wengine niliwaona wanatia chumvi kwenye maji yenye joto na kufanya kuwa ni mboga. Ukijua ukweli wa maisha ya wengi machozi wanashidwa kuzuilika.
Ndugu yangu mwenye shibe huwa hamkumbuki mwenye njaa hata siku moja sana sana hao wakutia chumvi kwenye maji wataambiwa kama hawakuwa na mboga kwanini hawakula keki. Hivi vitu vinaumiza mno hasa ukijua kuwa mtu wa kijijini ambaye ndiye mpiga kura hajui na hata ukimwelewesha hawezi kuelewa. Wananchi wanahitaji elimu ili waweze kujikomboa kama hatutapeleka elimu ya uraia vijijini kamwe ukombozi tutauota tu. Hapo juu umetoa mifano ya viongozi waliopita na hatima yao lkn kumbuka kuwa nchi walizoacha bado zipo kwenye dimbwi kubwa la umasikini. Tufanye sehemu yetu tusimwachie Mungu kwani Mungu ametupa akili na vitu vyote kwa ajili ya ukombozi so tutoke kwenye maombi tuanze kuwaelimisha wengine wasiojua.
 
Kwani wezi huwajui ni wale wale wa EPA,Walioiba Meremeta,Dowans nk majina bado baba Riz moko ananyafanyia kazi tusubiri tuu.

Mwizi anafanyia kazi majina ya wezi! Nahisi mkulu amejiandaa kuhama nchi baada ya 2015
 
Je jamii na yenyewe inahusika katika kufanikisha hili?

Unajua ukisikia taarifa kama hii - kwa yeyote yule anayeitakia mema nchi hii, kuona sote tunasonga mbele kama taifa moja lazima upate uchungu sana. Lakini hapo hapo linakuja swali, kwa nini matatizo kama haya yanajirudia? Je sisi ni watu wa aina gani tusiojifunza kutokana na makosa?

Hapa jamii na yeyenyewe ina swali la kujibu. Kwanini kwenye mambo "sensitive" kama haya, tunahindwa kusimama pamoja na kusema 'NO" kuzuia mambo haya yasiendelee?

Wengine watasema, aah sasa unafikiri utaweza! Ndio tunaweza kwanini tushindwe?

Rushwa inayofanyika SERIKALINI ni TAASISI. Ina structure yake, wafanikishaji na wale wanaotumika tu na kufaidika na chochote. Hii ndio rusha iliyokidhiri Tanzania. Kama Rushwa ni Taasisi basi tunaweza kuchunguza na kujua nani wanahusika katika "chain" hii ya MAFISADI.

Inashangaza sana, watu wako na GREED namna hii. KUKOSA MAISHA YA "PURPOSE' PENGINE NDIO SABABU KUU YA WATU WETU KUONA MATERIAL POSSESSION NDIO FARAJA YAO.....LAKINI HAITOSHI HATAHIVYO.

Fire Burn Corrupt Government.
 
Jaribu kujiandikisha hata vituo vya ngumbaru kama vipo na utapata elimu nzuri tu kuliko elimu uliyo nayo sasa.
Sawa kabisa, lakini kabla sijaenda kujiandikisha shule kwa ushauri wako, hebu onyesha shule yako imekusaidia nini hata ukajenga hoja kituko kama hiyo.

Hela iliyoibiwa, umedai, ni nyingi mno kwa sababu inazidi bajeti nzima ya baadhi ya wizara kama vile ya uchukuzi.

Bajeti ya wizara ya uchukuzi, umetuambia, ni bilioni 491; hela iliyoibiwa bilioni 480.

Kwa hiyo, kwa sababu kipimo cha wingi wa hela ni bajeti za wizara, basi shule yako uliyotumia kunishauri mie niende shule inatuambia hela iliyoibiwa ni ndogo kwa sababu haizidi hata bajeti ya wizara ya uchukuzi! Watanzania kwa nini hizo shule zetu tunazojivunia zinashindwa kutufundisha kuchambua hata the simplest of phenomena?

Tunasema kiasi hicho cha fedha zilizoibwa ni kikubwa kwa sababu ni zaidi ya bajeti ya mwaka kwa baadhi ya wizara, zikiwamo wizara kubwa kama ya Uchukuzi ambayo katika mwaka wa fedha wa 2013/14, kwa mfano ilitengewa Sh491 bilioni.
 
hiyo ndio serikali sikivu ya ccm, mi kwa mtazamo wangu ni sikivu kwa kutekeleza ufisadi tu
 
mwandishi wa habari amenifurahisha eti serikali imekaa kimya, unategemea iseme nini wakati imeshiriki. hazina haiko chini ya usamamizi wa mwansakafukyi wala masawe au masanja bali ni chini ya serikali. Hivyo ni jukumu lake kulinda hazina iliyopo na ikipotea mikononi mwa mlinzi mwenye mali anatakiwa kuwa mbogo na kumshughulikia mlinzi. Hapa napo kuna kituko cha mwaka, mwenye mali ambaye ni mwananchi yupo kimyaaaa eti amemwamini mlinzi ajisemee, ajichunguze na kujiwajibisha. Thubutu

ngoja watuibie, maisha yazidi kuwa magumu labda akili zitafanya kazi. Shake before use
khaaa, nchi ya wananchi wasobweka, wameacha inaendeshwa hovyo hovyo tu


pengine 2015 ktk uchaguzi, ----- atashtuka
 
Wana JF na wasomaji wa JF,

Bila ya shaka yoyote Fedha hii itakuwa imnechukuliwa na Vigogo wa CCM ambacho ni chama Tawala kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa 2015 pamoja na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwishoni mwa mwaka huu wa 2014.

Mabilioni ya EPA yalipotea na kuibiwa katika mazingira ya kutatanisha kwenye kipindi cha miaka ya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2005. Watu wasiumize kichwa wala kutafuta mwizi hii mbesa. Ni CCM na serikali yake. Tumesikia kuhusu Kigogo mmojawapo anayepigiwa upatu wa Kugombea na hatimaye kuukwaa Urahisi wa Nchi hii kwamba mpaka sasa ameshatumia Tshs. 6.7 Bilioni kwa kuhonga kwenye makanisa,misikiti,viongozi wa kidini na Kisiasa pamoja na watu binafsi ili kujihakikishia Ushindi wa kishindo mwaka 2015.

Fikiri juu ya 6.7 bilioni kutumiwa na mtu mmoja tu kama rushwa kwa ajili ya Urais na Kampeni bado kabisa mpaka 2015. Kama kwa sasa tu meweza kutumia hizo bilioni kuhonga tu,Je, kwenye Kampeni atutumia Bilioni ngapi na anazipata wapi kama siyo Hazina ya Serikali kupitia hiyo Wizara ya Marehemu Mgimwa???

Kwa sasa CCM na serikali yake wanafanya kila wawezalo kupata Fedha ya Uchaguzi mkuu 2015 kwa njia yoyote ile iwe haramu au halali bora Fueza ipatikane. Ndiyo maana kwa sasa tunashuhudia Biashara haramu za MADAWA YA KULEVYA,PEMBE ZA NDOVU NA WIZI WA PESA ZA SERIKALI!!!

CCM kweli ni janga la kitaifa. Watanzania wanatakiwa kushikamana ili kuiondoa madarakani hii serikali dhalimu!!
 
Au ndio maana wanataka wampooze mwingereza mgimwa baada ya baba yake kutangulizwa alipotaka kufuatilia huu uporaji...?Duh huyu mkwe.re sijui katutokea wapi,na sasa anasema tuchinjane wamechoka uvumilivu!!
 
Aisee acha kabisa wazo hilo, utaambiwa kwakuwa nchi hii ina amani hayo mambo mengine ni uchochezi tu wawapinzani. Na bado wataiba sana na utaona wakati wa uchaguzi watu wakipigwa vibaya sana kwa ushirikiano wa vyombo vya ulinzi ili watu wasijefungwa huko mbeleni.
Kumbe upo muda Sana humu
 
Back
Top Bottom