Nani wa kwanza anaepaswa kuihudumia familia yake ni baba au mama?

stable woman

JF-Expert Member
Nov 12, 2013
3,887
4,467
Habarini

Leo tuzungumzie hilo kwenye kuhudumia familia ni nani Wa kwanza anaetakiwa kuwa mstali Wa mbele kwenye kutoa huduma kwenye familia

Kuna familia nyingine mwanamke ndo anaehudumia familia baba anatumia pesa kwenye mambo yake,Familia nyingine mwanaume ndo anaewajibika huku mwanamke akitumia pesa yake kwa raha zake!

Yupi anatakiwa awe mstari Wa mbele kuhudumia familia?
Nawasilisha! Asanteni
 
hapa nadhamni ni makubaliano yenu katika kutoa hizo hudumu yupi ashike lipi na yupi afanye nini?
 
Jinsi dunia ilivyo toka mwanzo mwanamke na mwanaume (wanandoa) walikuwa wanapanga maisha na wanasaidiana kuanzia kutafuta kipato, matumizi ya familia, majukumu ya kijamii na kulea. Tamaduni chache za kitajiri za Ulaya ndio wanawake walikuwa hawajihusishi sana na kipato. Lakini wanawake wameshirikiana na wanaume kuanzia Adamu na Hawa.
So women have always been bread winners alongside men.
Ndoa kamilifu ni ile ambayo kila kitu mnapanga na kufanya pamoja, hakuna cha mume wala hakuna cha mke. Kama hufanyi/ hujui hayo basi hujui maana ya ndoa.
After saying that sidhani kama hilo swali lina nafasi katika mfumo wa ndoa kamilifu.

BTW: Watu wengi wanadhani wanawake zamani walikuwa wanaletewa(calling them goal keepers) ila asilimia kubwa hawakuwa hivyo.
 
Baba ndio anayetakiwa kuiela familia hata km mama anapesa mama yeye ni msaidizi tu weo toa pesa yeye aandae fullstop
 
Mwanaume ndio kichwa cha Nyumba, na anawajibika kuitunza familia yake. Ila kama mke ataamua kusaidia sehemu mojawapo, well and fine. Napinga kwa nguvu zote mwanaume kuweka utegemezi kwa mkewe kwenye swala la kuihudumia familia yake.

Mwanaume atakula kwa jasho... hii habari ya kuweka utegemezi kwa wanawake,,, ndio mwanzo wa zereu...
 
ukweli ndo huu REAL MAN lazima atafute pesa ya kutunza familia,ajue usalama wa familia yake..
mke ni msaidizi /ubavu wa mumewe all decision making must done by father of family
mwanaume ambaye anategemea mke wake kwa kweli hataokuwa huru hata kidogo inamfanya anakosa kauli ila mwanamke jukumu lake ni kumsaidia mumewe pale anapohitaji msaada

mwanaume ambaye ni tegemezi kwa mkewe wengi wao hizo ndoa zina matatizo zipo mikao ya chura ...
 
kwa kweli Baba ndo mwenye jukumu kuu mwanamke ni msaidizi katika kuyatekeleza yale mambo yanayopangwa na

baba,kutokana na hali za maisha kuwa ngumu na ili kupisha mambo ya kimaendeleo yaweze kuja tunashauri mama

amsaidie baba kwenye mambo mengine lakini hii haiondoi jukumu la baba kuwa ndo mlezi mkuu.
 
Ukishaita familia hakuna wa kwanza wala wa mwisho woote ni jukumu lenu kuiweka familia sawa
 
ICHANA you are a real WOMAN, Thank you!!! Sending friendship kisses and hugs your way.

Mwanaume akiwa tegemezi kwa mkewe, uhusiano wao unakuwa kama ulivyo wa Marekani au Uingereza na Tanzania. [Marekani/Uingereza akiwa ndio Mke na Mume akiwa ndio Tized (Tanzania)] Terms and conditions apply.

Tangia apo mwanaume hanaga akili au sense ya utegemezi kwa mwanamke yajapo maswala ya msingi na yanayogusa nafasi ya mwanaume. Kwa hiyo ukiona mwanaume anautegemezi kwa mwanamke, ujue tu ana shida mahali kwenye utambuzi wake, na tayari ameshapoteza sauti yake. (Anayetoa mahitaji ndio anayeheshimiwa nd yeye ndio mwenye maamuzi) Hata maandiko huwa yanasema "HEKIMA YA ASIYE NACHO HUWA HAISIKILIZWI''

ukweli ndo huu REAL MAN lazima atafute pesa ya kutunza familia,ajue usalama wa familia yake..
mke ni msaidizi /ubavu wa mumewe all decision making must done by father of family
mwanaume ambaye anategemea mke wake kwa kweli hataokuwa huru hata kidogo inamfanya anakosa kauli ila mwanamke jukumu lake ni kumsaidia mumewe pale anapohitaji msaada

mwanaume ambaye ni tegemezi kwa mkewe wengi wao hizo ndoa zina matatizo zipo mikao ya chura ...
 
Last edited by a moderator:
Kabisa dadaangu. Umenena vyema kabisa. Ni hatari sana kwa baba kupoteza mamlaka yake kwenye familia. Maisha ni kusaidiana ila sio mwanaume kuweka utegemezi wa kimajumu kwa Mkewe.

Unajua utegemezi huanzaga pole pole sana, kuna vijana hawajaoa ila wantaka sijui wafuliwe huko waliko panga, wafanyiwe usafi, wafuliwe na wapasiwe pia....wao ni kuweka miguu juu tu... saa mtu kama huyu anayefuliwa hadi nguo za ndani na GF wake akipata mwanya wa kumtegemea huyu msichana au pengine akija kuwa mke.. si ndio anakuwa lelemama kabisa?

Nashukuru Mzazi wangu alikuwa mkali kwangu toka nikiwa mdogo sana, alinijengea kubeba majukumu mapema sana. Mwanaume anaheshimika kwa kubeba kwake majukumu na kufanya maamuzi anayoyasimamia kwa uthabiti wake. Ukihamisha majukumu tayari umepoteza maamuzi. period

kwa kweli Baba ndo mwenye jukumu kuu mwanamke ni msaidizi katika kuyatekeleza yale mambo yanayopangwa na

baba,kutokana na hali za maisha kuwa ngumu na ili kupisha mambo ya kimaendeleo yaweze kuja tunashauri mama

amsaidie baba kwenye mambo mengine lakini hii haiondoi jukumu la baba kuwa ndo mlezi mkuu.
 
ICHANA you are a real WOMAN, Thank you!!! Sending friendship kisses and hugs your way.

Mwanaume akiwa tegemezi kwa mkewe, uhusiano wao unakuwa kama ulivyo wa Marekani au Uingereza na Tanzania. [Marekani/Uingereza akiwa ndio Mke na Mume akiwa ndio Tized (Tanzania)] Terms and conditions apply.

Tangia apo mwanaume hanaga akili au sense ya utegemezi kwa mwanamke yajapo maswala ya msingi na yanayogusa nafasi ya mwanaume. Kwa hiyo ukiona mwanaume anautegemezi kwa mwanamke, ujue tu ana shida mahali kwenye utambuzi wake, na tayari ameshapoteza sauti yake. (Anayetoa mahitaji ndio anayeheshimiwa nd yeye ndio mwenye maamuzi) Hata maandiko huwa yanasema "HEKIMA YA ASIYE NACHO HUWA HAISIKILIZWI''

u say the truth kwenye blue uhusiano unakuwa mgumu
kwa maisha ya sasa ya vijana wengi kupenda UAMARIO
ni shida sana familia kujijenga,vijana wengi wamekuwa waoga wa maishaa hawapendi kujitUma,hawawezi kufanya hta usafi as u say
hta kama unaishi na mkeo onyesha ya kuwa wewe ni mwanaume wa ukweli unaweza kufanya kazi zote za nyumbani na kutafuta pesa bila yake msaada wake..muonyeshe u can live ur life without her

mwanaume kauli bhana ukishaongea kinachfuata ni utekeelezaji tu,ukirudi home watoto wajue baba karudi sio wakuone kama mchumba umekuja naongelea mwanaume kujitambua,mwenye maamuzi na kauli sio DIKTETA

ndoa nilizoona wanawake ndo kiongozi zina matatizo "laki kumi"
 
Kabisa dadaangu. Umenena vyema kabisa. Ni hatari sana kwa baba kupoteza mamlaka yake kwenye familia. Maisha ni kusaidiana ila sio mwanaume kuweka utegemezi wa kimajumu kwa Mkewe.

Unajua utegemezi huanzaga pole pole sana, kuna vijana hawajaoa ila wantaka sijui wafuliwe huko waliko panga, wafanyiwe usafi, wafuliwe na wapasiwe pia....wao ni kuweka miguu juu tu... saa mtu kama huyu anayefuliwa hadi nguo za ndani na GF wake akipata mwanya wa kumtegemea huyu msichana au pengine akija kuwa mke.. si ndio anakuwa lelemama kabisa?

Nashukuru Mzazi wangu alikuwa mkali kwangu toka nikiwa mdogo sana, alinijengea kubeba majukumu mapema sana. Mwanaume anaheshimika kwa kubeba kwake majukumu na kufanya maamuzi anayoyasimamia kwa uthabiti wake. Ukihamisha majukumu tayari umepoteza maamuzi. period

Mazoea hujenga tabia ni kweli kabisa mtu huanzia mbali,ajabu vijana wa leo ukimuuliza kwanini ameoa atakujibu amechoka kufua,anataka apikiwe na azae,akizaa kutunza anakwepa majukumu.kweli baba yako alikufunza vyema sifa kwake.
 
Back
Top Bottom