Nani wa ku apply kupitia TCU na NACTE?!

TheDealer

JF-Expert Member
Nov 19, 2012
2,424
1,130
NACTE wanajihusisha na Technical Institution mfano IFM, TIA, CBE nk na TCU wanajihusisha na Universities mfano UDSM, UDOM nk.

Technical Institutions nao pia wanatoa bachelor degrees, diploma, certificates the same with universities. Sasa kuna pahala panawachanganya wengi, Je ni nani anayepaswa ku apply kupitia TCU na nani anayepaswa kupitia NACTE?!

Ikumbukwe kabla ya matokeo ya form six CAS ya NACTE ilikuwa 'on' kudahili wanafunzi wa technical institutions pekee, na sasa ipo 'on' kudahili pia lakini ni certificate, diploma na higher diploma pekee!

Sasa Je, CAS ya NACTE na CAS ya TCU inatofauti gani?!

Changieni!

------------------------------------------------------------------------------

Nijuavyo:

Kama unataka kupiga degree vyuo vikuu unapaswa kudahili kupitia CAS ya TCU na kama unataka kupiga degree kupitia vyuo vya ufundi unapaswa kudahili kupitia CAS ya NACTE. Na ndio maana UDOM wanajidahilia wenyewe wa certificate na diploma. Period.
 
Back
Top Bottom