Nani mwenye akili kuliko Mwl Nyerere?

Nani mwenye akili kuliko Mwl Nyerere?

Jini mahaba

Senior Member
Joined
Feb 24, 2014
Posts
151
Reaction score
39
MI MPAKA LEO SIAMINI KAMA KUNA MWENYE AKILI NA BUSARA KAMA NYERERE
sasa busara zake zinasema hivi ......................
"Huwezi kuniua kwa nia njema, halafu useme kwamba haujaniua. Utakuwa umeniua tu. Na ukifufua serikali ya Tanganyika ni sawa na kuua Muungano, kama hamlijui hilo.
Hivyo, huwezi ukavunja Muungano halafu ukasema kwamba haukujua kama utauvunja MUUNGANO, Utakuwa umeshauvunja, na hautaweza kuurudisha tena. Msidhani mimi (Nyerere) na Karume hatukuziona serikali tatu" - Mwl. Nyerere 1993, Dodoma.

Nashangaa mbowe na magwanda ya chadema yanampinga Mwalimu nyerere kama sio laana kumpinga mzee nyerere ni nini
 
Enzi za nyerere ni tofauti na enzi hizi za sasa. Enzi za nyerere kulkuwa hakuna muingiliano mkubwa kati ya waznz na watanganyika hata biashara ilikuwa ndogo. lengo kuu lake lilikuwa ni ulinzi na usalama. katika zama hizi ambazo idadi ya watu inakuwa kwa kasi na watu wa pande mbili kuingiliana kwa kasi zaidi huku rasilimali za kila sehemu kugundulika na sehemu moja kuzuia rasilimali zake,NI WAKATI MUAFAKA WA KUWA NA SERIKALI TATU. znz kuna mafuta na gesi smz inasema yawe ya znz,lakini ya tanganyika hesabu zake zinaingia hazina ambako ni serikali ya muungano? hapo huoni tofauti?

Miaka ya 90 , dar ardhi ilikuwa ikigawiwa bure hata znz, sasa inapanda bei na upande mmoja hauruhusu wengine kumiliki ardhi huku utalii ukitegemea nguvu kazi kubwa ya bara,je mpishi wa hoteli apange nyumba maisha yake yote kisa serena arusha ilimuajiri baadae ikamuhamishia serena znz? basi alipwe kama international.polisi aliyetolewa tanga kuja znz miaka yote asiruhusiwe kununua hata banda la kuwaachia wanae?.

kwa upande wa znz wanalia kuwa mawaziri wao hawana mamlaka wawapo nje ya tz ,kwa kuwa hujulikana tz pekee na sio znz.kwa nini mambo yasiyo ya muungano yasihudumiwe na nch washirika ili na wenzetu wa znz viongozi wao waweze kuheshimika nje na kupata misaada kadri itakavyowezekana?
 
Sawa mzee alikuwa genious lakini muungano aliufanya kisanii mno ndo maana adi leo matatizo hayaishi
Muungano wa kisanii usingedumu kwa miaka 50 waliofanya muungano ya kisanii yote haikudumu. "Tanzania kwanza"

 
Hakika kama anaona jinsi gani nchi inavyoendelea...... basi anatamani kurudi
 
wewe kumbe bado upo kwenye zama zile za zidumu fikira SAHIHI za mwenyekiti. pole.

MI MPAKA LEO SIAMINI KAMA KUNA MWENYE AKILI NA BUSARA KAMA NYERERE
sasa busara zake zinasema hivi ......................
"Huwezi kuniua kwa nia njema, halafu useme kwamba haujaniua. Utakuwa umeniua tu. Na ukifufua serikali ya Tanganyika ni sawa na kuua Muungano, kama hamlijui hilo.
Hivyo, huwezi ukavunja Muungano halafu ukasema kwamba haukujua kama utauvunja MUUNGANO, Utakuwa umeshauvunja, na hautaweza kuurudisha tena. Msidhani mimi (Nyerere) na Karume hatukuziona serikali tatu" - Mwl. Nyerere 1993, Dodoma.

Nashangaa mbowe na magwanda ya chadema yanampinga Mwalimu nyerere kama sio laana kumpinga mzee nyerere ni nini
 
Sidhani kama alikuwa na akili kiasi ambacho mnamsifia.. muungano ni mgogoro tu toka uwepo wake.

Nyerere alikosea mengi tu na mojawapo ni hili la kuiuwa Tanganyika.

Kama alivyoshindwa ujamaa.

Kama alivyoshindwa uchumi.

Na hili la uchumi linajionesha wazi kuwa limeshindwa.

Anaebisha kama fikra za Nyerere hazidumu basi aongelee Serikali tatu. Mimi wa kwanza, naongelea Serikali tatu.
 
Binafsi simuungi mkono mwl.nyerere hata robo.Hakuna wa kushauriwa,aliamini mawazo yake,aliforce n.k.hapa ni baadhi tu
 
Watu wengine ni mazuzu kweli ina maana mtu kama mbowe anaakili gani kumzidi nyerere?hii tanganyika hadi muende kaburini hamtaiona kamwe,warioba mwenyewe anajuta, sahizi anahaha huku na huku kwa upotoshaji alioufanya.
 
Mangi Mareale na Tuntemeke Sanga ndio walikuwa wana akili kuliko mealimu

1+1=3 !!!! Uliona wapi hiyo.By J.K Nyerere
 
nakumbuka nyerere katika moja ya hotuba zake alisema
'katika miaka 23 ya serikali aliyoiongoza kuna mambo ya maana na yakijinga wameyafanya. Ila utashangaa watu watayaacha ya maana na kung'ang'ania ya kijinga'
Na ndio kinachoendelea sasa hv serikalini.
 
Back
Top Bottom