Nani mhamiaji haramu Kagera? pitia waraka huu

Nani mhamiaji haramu Kagera? pitia waraka huu

KUNA watu mkoani Kagera wanaitwa ‘wahamiaji haramu’. Hawa wanaoitwa wahamiaji haramu ni wale wanaoishi miongoni mwa jamii zao zilizogawanywa na wakoloni walipoweka mipaka miongo mingi iliyopita.
Ni muhimu kutambua kuwa sehemu zote za mipakani zina matatizo ya aina hii. Kwa sehemu kubwa matatizo haya yanatokana na kutofahamu sheria za uhamiaji.
Kwa bahati mbaya sana, operesheni za kuhamisha hawa wanaoitwa wahamiaji haramu, zimekuwa zikitokea kwa vipindi tofauti, na ghafla zinatoweka baada ya wahusika wa operesheni hizi kuwa wamenufaika na mali wanazopora kutoka kwa watu hawa, hasa mifugo na wakati mwingine hongo ya fedha.
Kitu ambacho watawala wetu wamekataa kutambua ni ukweli kwamba wakati wakoloni wakiweka mipaka, hawakuangalia kama kabila moja limegawanywa na mpaka.
Walichokifanya ni kuweka hiyo mipaka na kuacha makabila tofauti ya mipakani yakiangukia pande mbili za nchi tofauti.
Isitoshe, wakati mwingine makabila haya yalikuwa chini ya himaya moja kama ilivyo Bunyoro Kitara iliyojumuisha watu wa Kagera na sehemu za nchi jirani.

Tangu kupatikana kwa uhuru wa nchi za Afrika Mashariki, suala hili limekuwa likiachwa bila msimamo unaojulikana.
Watu wakaendelea na shughuli zao hadi kunapotokea tatizo la kisiasa kati au baina ya nchi zenye mpaka mmoja, basi suala hilo huibuka na kuwataka wale wanaoshabihiana kwa sura na jamii iliyo upande wa pili, kuondoka na kurudi ‘kwao’.
Kwao ni wapi? Vurugu hizi zimekuwa zikiibuka na kutoweka. Ni ukweli kuwa kutojua sheria si utetezi, lakini je, si busara serikali yeyote makini kuwasaidia wananchi wasio na uelewa wa mambo haya ili kuondoa mzozo wa mara kwa mara?
Hawa tunaowaita wahamiaji haramu, wengi wao wanasalitiwa na maumbile yao ya kinasaba.
Mkoa wa Kagera una watu wa jamii ya wafugaji waitwao Wahima ambao wamekuwa katika mkoa huu kwa miaka mingi.
Haiyumkini watu hawa wanashabihiana zaidi na wenyeji wa nchi jirani, lakini wanaweza kuwa siyo raia wa nchi hizo.
Ni kweli kuna walio raia wa nchi jirani, lakini pia kuna walio raia wa Tanzania.
Kuna wahamiaji wachache wanaweza kuwa wameingia nchini kinyume cha sheria; hawa wanaweza kuondolewa. Lakini si aina hii ya operesheni yenye uonevu ndani yake.
Mimi ninayeandika haya, baba mzaa babu ni kutoka Nkole kule Uganda. Isitoshe, marehemu baba yangu anamiliki shamba Wilaya ya Lakai hukohuko Uganda; hata bibi yangu mzaa huyo baba amezikwa huko.
Leo utaniambia niondoke nirudi ‘kwetu’ Nkole? Kwetu wapi? Baadhi ya hawa wanaoitwa wahamiaji haramu katika Mkoa wa Kagera, hususan Wilaya ya Missenyi, kinachowaponza ni utajiri wao wa mifugo. Hapa aliye muungwana atakubaliana na ukweli huu.
Wenzetu hawa wana talanta ya ufugaji na wengi wao wamepata ng’ombe wa kuanzisha ufugaji huo kutoka kwa jamii nyingine mkoani humu.
Hii ni talanta yao kama walivyo wenzetu Wachagga katika umahiri wa uchuuzi na biashara. Sisi wakazi wa Kagera tusimame kidete kukataa uporaji huu wa mali za watu kwani uchumi wa mkoa wetu utarudi nyuma.
Tuangalie mfano wa Zimbabwe, yalinyang’anywa mashamba kutoka kwa Wazungu; wakagawiwa wazalendo ambao wameyaacha yakiwa machaka; huku Zimbabwe ikigeuka ombaomba wa chakula.
Tusijidanganye kwamba tukipora mashamba na mifugo ya hawa ndugu zetu wanaoitwa wahamiaji haramu tutafaidika na lolote.
Huu uamuzi unatokana na tofauti za viongozi wa kisiasa ambao hawaathiriki na kadhia hii. Tukubali ukweli kuwa hili ni tatizo la kikoloni.
Tanzania hatuna uhaba wa ardhi. Wale ambao tunao tayari watambuliwe kama raia wa nchi hii. Tusijidananye, hili si tatizo la Kagera tu. Ni la Kigoma, Tanga, Mara, Mtwara na kwingineko kwenye mipaka kati yetu na nchi nyingine.
Kuna wakati kiongozi mkubwa wa nchi hii alituhumiwa kuwa Mmakonde wa Msumbiji! Nina mfano wa diwani mmoja wa zamani kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye alihudumu kwa vipindi tofauti wilayani Missenyi, akifadhili chama wakati ni mtu wa jamii ambayo sasa ‘haitakiwi’.
Kumbuka hata Marekani imekubali kuwa maendeleo ya nchi yao yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na ‘wahamiaji haramu’. Tushikamane wana Kagera, mkoa wetu unarudi nyuma.

Mwandishi wa makala hii ni msomaji wa Tanzania Daima na mwanasheria anayepatikana kwa simu; 0754 /0784 397350 au barua pepe; cmuleju@yahoo.com.

'

ktk kutetea uhamiaji haramu umekosa Hoja za msing,lazima waondoke bila kujali wanamilki mbuz, kuku au ng'ombe.cha msing ithibitike kwel ni wahamiaji haramu na taaratib zifuatwe wakati wa kuondolewa. wakorea wote kusin na kask ni ndugu Kwan miaka 60 iv walikuwa nchi moja kabla ya vita kuwagawanya wanafanana kwa kila kitu, lakn haliwapi uharali kutoka upande mmoja wa nchi kinyume na sheria.Jr utasemeje kuhusu wasudan?mkoa wa kagera umeathirika zaid sababu kwanza unapakana na nchi nyingi zenye migogoro pili nchi zenye uhaba wa ardhi,kama Rwanda na Uganda.
 
usifananishe Korea na uku Africa,wale mgogoro wao adi wakagawanyika ni kutokana na tofaut za sera ya uchumi ujamaa na Ubepari
 
Hata kusini kuna wanyasa kutoka malawi,wamakonde kutoka msumbiji sema wao hawana tabu wanyasa wamekubali kua walinzi maisha yanaenda wako hapa kwa amani na adabu tatizo la wahamiaji wa rwanda wana tabia za ajbu mara ujambazi mara rais wao atutishie basi mnageuka kero na threat hakatazwi mgeni kuishi au kua raia kabisa sema aukubali utz kwa vitendo sio yuko hapa halafu analeta mambo ya ovyo na rais wenu awe na adabu.hivi fastjet inaenda kigali?natka nimkatie tiketi mleta thread ya kurudi kwao.RUDI KWENUUUUUU!
 
Hawana adabu. Tuwakimbize. Hawa jamaa watatuambukiZa matatizo yao ya ubaguz.
 
Nayasema haya kwa sababu nasikia uchungu na nimeshuudia kuliko wengine mnaoongea kwa ushabiki au kutetea kundi fulani bila kujua madhara gani wananchi wanapata kutokana na wakimbizi haramu.
Yeyote anayeijua pori la Kimisi mpaka utobokee Chanyamisa ni kumshukuru Mungu unapoona umevuka salama. Majambazi hawakai barabarani muda wote bali wana timings na wanakuwa na mtandao wa habari juu ya mlengwa wao na wakikosa basi wanamvamia yeyote. Hali ya ujambazi ilikuwa imevuka hadi kufikia ktk maeneo yoyote yenye minada na hata ktk stations/miji ya tarafa na kata. Hawa wahamiaji kwa kushirikiana na baadhi ya wenyeji wakionekana sehemu fulani wakijikusanya basi ujue jioni kuna duka ama nyumba ya mtu itavunjwa! Ktk baadhi ya maeneo hawa watu walikuwa wameogopwa maana hawana maeneo maalum na wanawezapotea na kuibukia sehemu nyingine na wakaanza maisha! Wahamiaji wenye mitaji na hasa baadhi toka Rwanda na Burundi wanajua kufanya biashara na kutumia kwa matanuzi na hivyo kujijengea mahusiano ya karibu na wenyeji kiasi cha kutowezahoji uhalali wao Nchini!
Binafsi naona kuondolewa kwao ni sahihi kabisa na sijuhi busara gani inatakiwa ambayo ndugu zangu mnaotete mnataka. Ni kweli kuna udhaifu wa mamlaka kwa kipindi kirefu uliopelekea hawa watu wakaingia na kutoka na hata kukaribishana bila utaratibu ...yaani kujogangana kama kwamba "bijagamire" and nobody care. Hapa ndio mzizi wa tatizo uliofanya wahamiaji kujiona wamefika na hata kuwa sugu. Jamani sasa wameambiwa rudi kwenu ama fuata utaratibu, inaonekana taabu????

Watu wawe wapole na wajidhatiti kwa malengo yajayo na zaidi kuondoka kwao tu tusione kama ndo amani imemwagika Karagwe ama maeneo mengine ya mpakani.
1. Ufanyike udhibiti wa makusudi kuingia kwa wahamiaji ili wafuate taratibu ikibidi hata kuomba uraia.
2. Maeneo waliyokuwa wanaishi yasiachwe yakawa mapori bali wayaendeleze na kuzalisha hata zaidi ya walioondoka(hapa kuna tatizo - uvivu).
3. Kama kuna watu ambao inaonyesha kuna utata wa utambuzi(ni wahamiaji/mzawa/raia) basi kuwepo na muda zaidi kumpa nafasi ya kujitetea na kudhihirisha uhalali wake. Najua hili ni tatizo kwani watendaji wa wilaya ambao wamekuwa wakitoa vibali vya muda na hata kuwaficha watu wengine kwa njia ya rushwa hawakuwa na maandalizi ya operation hii kabla ya tamko la Rais.

La msingi Rais ameonyesha njia kuwa hii nchi ina wenyewe bisha hodi ufunguliwe na itakuwa na maana zaidi kama wanaoingia watachambuliwa zaidi, kujua wanafuata nini na wanaondoka lini. Vinginevyo watakaokuja baadaye watakuwa wajanja zaidi na hatari maana wengine wanaenda kuanza maisha upya Nchini kwao. Na kama nchi zao zitawapa ardhi za makambi kama Rwanda ilivyopanga basi ujue hawataisahau Karagwe na muda wote watapenda kurudi ama kuwa na molari wa kulipa kisasi. Operation hii iwe endelevu na vyombo wa usalama wasipumue maana ndiyo kwanza ngoma imeanza na ichezwe vilivyo.

usilazimishe mawazo yangu na wewe yafanane ata kama wote ni watanzania,mimi ninachotetea uamuzi wa kuwaondoa ufate haki,kuna wengine wamekuwepo Tanzania toka 1950's na awajui kwao isipokuwa muonekano wao wa kinyarwanda utafanya warudishwe,pia ninachosema haki itendeke kuwarudisha kwao sio kutake advantage kauli ya Kikwete ili kuwaibia mali zao.

Harafu Kikwete alisema wahamiaji haramu akusema Wanyarwanda tu,kuna upotoshaji mkubwa unaoendelea
 
KUNA watu mkoani Kagera wanaitwa ‘wahamiaji haramu’. Hawa wanaoitwa wahamiaji haramu ni wale wanaoishi miongoni mwa jamii zao zilizogawanywa na wakoloni walipoweka mipaka miongo mingi iliyopita.

Kwa bahati mbaya sana, operesheni za kuhamisha hawa wanaoitwa wahamiaji haramu, zimekuwa zikitokea kwa vipindi tofauti, na ghafla zinatoweka baada ya wahusika wa operesheni hizi kuwa wamenufaika na mali wanazopora kutoka kwa watu hawa, hasa mifugo na wakati mwingine hongo ya fedha.

Tangu kupatikana kwa uhuru wa nchi za Afrika Mashariki, suala hili limekuwa likiachwa bila msimamo unaojulikana.

Ni kweli kuna walio raia wa nchi jirani, lakini pia kuna walio raia wa Tanzania.
Kuna wahamiaji wachache wanaweza kuwa wameingia nchini kinyume cha sheria; hawa wanaweza kuondolewa. Lakini si aina hii ya operesheni yenye uonevu ndani yake.
Mimi ninayeandika haya, baba mzaa babu ni kutoka Nkole kule Uganda.

Isitoshe, marehemu baba yangu anamiliki shamba Wilaya ya Lakai hukohuko Uganda; hata bibi yangu mzaa huyo baba amezikwa huko.
Leo utaniambia niondoke nirudi ‘kwetu’ Nkole? Kwetu wapi? Baadhi ya hawa wanaoitwa wahamiaji haramu katika Mkoa wa Kagera, hususan Wilaya ya Missenyi, kinachowaponza ni utajiri wao wa mifugo. Hapa aliye muungwana atakubaliana na ukweli huu.

Wenzetu hawa wana talanta ya ufugaji na wengi wao wamepata ng’ombe wa kuanzisha ufugaji huo kutoka kwa jamii nyingine mkoani humu.
Hii ni talanta yao kama walivyo wenzetu Wachagga katika umahiri wa uchuuzi na biashara. Sisi wakazi wa Kagera tusimame kidete kukataa uporaji huu wa mali za watu kwani uchumi wa mkoa wetu utarudi nyuma.
Tuangalie mfano wa Zimbabwe, yalinyang’anywa mashamba kutoka kwa Wazungu; wakagawiwa wazalendo ambao wameyaacha yakiwa machaka; huku Zimbabwe ikigeuka ombaomba wa chakula.
Tusijidanganye kwamba tukipora mashamba na mifugo ya hawa ndugu zetu wanaoitwa wahamiaji haramu tutafaidika na lolote.
Huu uamuzi unatokana na tofauti za viongozi wa kisiasa ambao hawaathiriki na kadhia hii. Tukubali ukweli kuwa hili ni tatizo la kikoloni.
Tanzania hatuna uhaba wa ardhi. Wale ambao tunao tayari watambuliwe kama raia wa nchi hii. Tusijidananye, hili si tatizo la Kagera tu. Ni la Kigoma, Tanga, Mara, Mtwara na kwingineko kwenye mipaka kati yetu na nchi nyingine.

Mwandishi wa makala hii ni msomaji wa Tanzania Daima na mwanasheria anayepatikana kwa simu; 0754 /0784 397350 au barua pepe; cmuleju@yahoo.com.

Huu kwa mtazamo wangu ni Propaganda.
Na ni vizuri Rasimu ya Katiba Mpya ikaweka mipaka imara ya uhuru wa namna hii kwa Manufaa ya Taifa .

Hapana kwa baadhi ya mambo ndani rasimu ya katiba mpya-2103

Rasimu ya Katiba Mpya 2013

29.-(1) Kila mtu:

(a) anao uhuru wa-
(i) kuwa na maoni na kueleza fikra zake;
(ii) kufanya mawasiliano na vile vile anayo haki ya kutoingiliwa katika mawasiliano yake;
(iii) ubunifu na sanaa;
(iv) kitaaluma na tafiti za kisayansi; na
(b) anayo haki ya kupewa taarifa wakati wowote kuhusu:
(i) matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi; na

(ii) utekelezaji wa mamlaka ya nchi kuhusu sera za kitaifa na shughuli ya maendeleo ya jamii; na
(iii) masuala mengine muhimu kwa jamii.
(2) Utekelezaji wa haki zilizoainishwa katika Ibara ndogo ya (1), utajumuisha wajibu muhimu kwa mwananchi na wajibu huo unaweza kupunguza haki hizo kutokana na:
(a) vita au machafuko ya kisiasa; au

(b) propaganda kuhusu vita, ushawishi wa chuki kwa misingi ya rangi, ukabila, ubaguzi wa kijinsia, dini au masuala yoyote yanayoweza kuleta madhara kwa Taifa.

Maoni yangu kuhusu Ibara hiyo;

29.
-(1) Kila mtu:

(a) anao uhuru wa-

(i) kuwa na maoni na kueleza fikra zake;

(ii) kufanya mawasiliano na vile vile anayo haki ya kutoingiliwa katika mawasiliano yake;

(iii) ubunifu na sanaa;

(iv) kitaaluma na tafiti za kisayansi; na

(b) anayo haki ya kupewa taarifa wakati wowote kuhusu:

(i) matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi; na

(ii) utekelezaji wa mamlaka ya nchi kuhusu sera za kitaifa na shughuli ya maendeleo ya jamii; na

(iii) masuala mengine muhimu kwa jamii.

(2) Utekelezaji wa haki zilizoainishwa katika Ibara ndogo ya (1), utajumuisha wajibu muhimu kwa mwananchi na wajibu huo unaweza kupunguza haki hizo kutokana na:

(a) vita au machafuko ya kisiasa; au

(b) propaganda kuhusu vita, ushawishi wa chuki kwa misingi ya rangi, ukabila, ubaguzi wa kijinsia, dini ,propaganda kuhusu shughuli za Uchumi yenye mlengo wa ubaguzi au masuala yoyote yanayoelekea kuleta madhara kwa Taifa.

(c) kabla au baada ya mamlaka husika kuchukua hatua kupunguza/kusitisha uhuru wa mtu kwa mujibu wa Ibara 29;2(b) ya katiba hii basi mamlaka husika italiarifu Bunge katika kikao kijacho baada ya tukio husika kuhusu sababu na hatua za kisheria ambazo zimechukuliwa/ inatarajia kuchukuliwa ilikuliepusha Taifa na madhara.

Je huyu mwandishi anafahamu Sheria za Uhamiaji inasema je?.Kwa namna yoyote ile kama kweli kuna Mtanzania amefukuzwa ndani ya Nchi yake kisa si Mtanzania na nadhani Mahakama zipo za yeye kudai uhalali wa Uraia wake.
 
Hivi inakuaje mtu kukataa kurudi kwao???? Harafu rais wao anatukana rais ambae amevumilia kukaa na wananchi wako ambao ndio wana ongoza kwa ujambazi na ubaradhuli,bora wangekua raia wema lakini ni raia wanao hatarisha amani! They have to go!

Hawa jamaa (Watusi) wana dharau sana, wana ubinafsi, hata ikitokea ukaoa binti mtusi hakubali uzae naye anatafuta mtusi mwemzake ndo anamgonga na kumzalisha
 
Back
Top Bottom