Nani mhamiaji haramu Kagera? pitia waraka huu

Nani mhamiaji haramu Kagera? pitia waraka huu

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,328
KUNA watu mkoani Kagera wanaitwa ‘wahamiaji haramu'. Hawa wanaoitwa wahamiaji haramu ni wale wanaoishi miongoni mwa jamii zao zilizogawanywa na wakoloni walipoweka mipaka miongo mingi iliyopita.
Ni muhimu kutambua kuwa sehemu zote za mipakani zina matatizo ya aina hii. Kwa sehemu kubwa matatizo haya yanatokana na kutofahamu sheria za uhamiaji.
Kwa bahati mbaya sana, operesheni za kuhamisha hawa wanaoitwa wahamiaji haramu, zimekuwa zikitokea kwa vipindi tofauti, na ghafla zinatoweka baada ya wahusika wa operesheni hizi kuwa wamenufaika na mali wanazopora kutoka kwa watu hawa, hasa mifugo na wakati mwingine hongo ya fedha.
Kitu ambacho watawala wetu wamekataa kutambua ni ukweli kwamba wakati wakoloni wakiweka mipaka, hawakuangalia kama kabila moja limegawanywa na mpaka.
Walichokifanya ni kuweka hiyo mipaka na kuacha makabila tofauti ya mipakani yakiangukia pande mbili za nchi tofauti.
Isitoshe, wakati mwingine makabila haya yalikuwa chini ya himaya moja kama ilivyo Bunyoro Kitara iliyojumuisha watu wa Kagera na sehemu za nchi jirani.

Tangu kupatikana kwa uhuru wa nchi za Afrika Mashariki, suala hili limekuwa likiachwa bila msimamo unaojulikana.
Watu wakaendelea na shughuli zao hadi kunapotokea tatizo la kisiasa kati au baina ya nchi zenye mpaka mmoja, basi suala hilo huibuka na kuwataka wale wanaoshabihiana kwa sura na jamii iliyo upande wa pili, kuondoka na kurudi ‘kwao'.
Kwao ni wapi? Vurugu hizi zimekuwa zikiibuka na kutoweka. Ni ukweli kuwa kutojua sheria si utetezi, lakini je, si busara serikali yeyote makini kuwasaidia wananchi wasio na uelewa wa mambo haya ili kuondoa mzozo wa mara kwa mara?
Hawa tunaowaita wahamiaji haramu, wengi wao wanasalitiwa na maumbile yao ya kinasaba.
Mkoa wa Kagera una watu wa jamii ya wafugaji waitwao Wahima ambao wamekuwa katika mkoa huu kwa miaka mingi.
Haiyumkini watu hawa wanashabihiana zaidi na wenyeji wa nchi jirani, lakini wanaweza kuwa siyo raia wa nchi hizo.
Ni kweli kuna walio raia wa nchi jirani, lakini pia kuna walio raia wa Tanzania.
Kuna wahamiaji wachache wanaweza kuwa wameingia nchini kinyume cha sheria; hawa wanaweza kuondolewa. Lakini si aina hii ya operesheni yenye uonevu ndani yake.
Mimi ninayeandika haya, baba mzaa babu ni kutoka Nkole kule Uganda. Isitoshe, marehemu baba yangu anamiliki shamba Wilaya ya Lakai hukohuko Uganda; hata bibi yangu mzaa huyo baba amezikwa huko.
Leo utaniambia niondoke nirudi ‘kwetu' Nkole? Kwetu wapi? Baadhi ya hawa wanaoitwa wahamiaji haramu katika Mkoa wa Kagera, hususan Wilaya ya Missenyi, kinachowaponza ni utajiri wao wa mifugo. Hapa aliye muungwana atakubaliana na ukweli huu.
Wenzetu hawa wana talanta ya ufugaji na wengi wao wamepata ng'ombe wa kuanzisha ufugaji huo kutoka kwa jamii nyingine mkoani humu.
Hii ni talanta yao kama walivyo wenzetu Wachagga katika umahiri wa uchuuzi na biashara. Sisi wakazi wa Kagera tusimame kidete kukataa uporaji huu wa mali za watu kwani uchumi wa mkoa wetu utarudi nyuma.
Tuangalie mfano wa Zimbabwe, yalinyang'anywa mashamba kutoka kwa Wazungu; wakagawiwa wazalendo ambao wameyaacha yakiwa machaka; huku Zimbabwe ikigeuka ombaomba wa chakula.
Tusijidanganye kwamba tukipora mashamba na mifugo ya hawa ndugu zetu wanaoitwa wahamiaji haramu tutafaidika na lolote.
Huu uamuzi unatokana na tofauti za viongozi wa kisiasa ambao hawaathiriki na kadhia hii. Tukubali ukweli kuwa hili ni tatizo la kikoloni.
Tanzania hatuna uhaba wa ardhi. Wale ambao tunao tayari watambuliwe kama raia wa nchi hii. Tusijidananye, hili si tatizo la Kagera tu. Ni la Kigoma, Tanga, Mara, Mtwara na kwingineko kwenye mipaka kati yetu na nchi nyingine.
Kuna wakati kiongozi mkubwa wa nchi hii alituhumiwa kuwa Mmakonde wa Msumbiji! Nina mfano wa diwani mmoja wa zamani kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye alihudumu kwa vipindi tofauti wilayani Missenyi, akifadhili chama wakati ni mtu wa jamii ambayo sasa ‘haitakiwi'.
Kumbuka hata Marekani imekubali kuwa maendeleo ya nchi yao yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na ‘wahamiaji haramu'. Tushikamane wana Kagera, mkoa wetu unarudi nyuma.


Mwandishi wa makala hii ni msomaji wa Tanzania Daima na mwanasheria anayepatikana kwa simu; 0754 /0784 397350 au barua pepe; cmuleju@yahoo.com.





 
we kama umekili kuwa unamiliki shamba Uganda wewe jiandae mwenyewe kuondoka au kutafuta kibali cha kufanya kazi hapa TZ.
 
we kama umekili kuwa unamiliki shamba Uganda wewe jiandae mwenyewe kuondoka au kutafuta kibali cha kufanya kazi hapa TZ.

mkuu unaongea na nani? nani amekili anamiliki shamba uganda?
 
Hakuna lililo na mwanzo likakosa kuwa na mwisho. JK Kwenye hili nadhani amelizungumzia vizuri sana. Ifike wakati tuvae uzalendo kwa mipaka ya nchi yetu. Ni jukumu la kila raia kulinda mipaka ya nchi yake. Kama unaweza kulinda mipaka ya nyumba yako kwa uhai wako iweje ushindwe kulinda mipaka ya nchi yako?
JK amesema wazi kuwa ukitaka kuishi bila kusumbuliwa huna budi kuchukua uraia wa Tanzania. Hutaki nenda kwenu. Hii ndo suluhu stahiki kwa walowezi haramu wote toka nje ya mipaka ya Tanzania.
Watanzania na tuweke utaifa mbele. Nchi za jirani wanasimamia vizuri sana mipaka yao. Sisi kwa nini tusifanye hivyo?
 
Hakuna lililo na mwanzo likakosa kuwa na mwisho. JK Kwenye hili nadhani amelizungumzia vizuri sana. Ifike wakati tuvae uzalendo kwa mipaka ya nchi yetu. Ni jukumu la kila raia kulinda mipaka ya nchi yake. Kama unaweza kulinda mipaka ya nyumba yako kwa uhai wako iweje ushindwe kulinda mipaka ya nchi yako?
JK amesema wazi kuwa ukitaka kuishi bila kusumbuliwa huna budi kuchukua uraia wa Tanzania. Hutaki nenda kwenu. Hii ndo suluhu stahiki kwa walowezi haramu wote toka nje ya mipaka ya Tanzania.
Watanzania na tuweke utaifa mbele. Nchi za jirani wanasimamia vizuri sana mipaka yao. Sisi kwa nini tusifanye hivyo?

umeeleza vizuri na kuonyeshaa uzalendo
 
Article nzuri lakini kwenye bord amekosea kwani Zimbabwe ya sasa mzawa anamiliki na kuzalisha ardhi!
 
we kama umekili kuwa unamiliki shamba Uganda wewe jiandae mwenyewe kuondoka au kutafuta kibali cha kufanya kazi hapa TZ.
Wanaomiliki majumba na fedha huko Dubai na ulaya wataondoka lini?
 
Ni mmoja wao na ukitaka kujua ni mmoja wao angalia treads zote zinazoongelea Rwanda uone mchango wake, wako wanajulikana JF Money Stunna, Mukamasimba, Nicolas, Kalisa, Tutajumbukirwa, etc
Mkuu, mbona unajishtukia? Au wewe ndio uliiandika makala hiyo ya Tanzania Daima?
 
Waganda warudi kwao,wanyarwanda warudi kwao na warundi warudi kwao full stop.
 
Makala kama hii pia kuwekwa kwenye gazeti la Tanzania Daima ni kujivua nguo mchana kweupe,Tanzania Daima mnatumia jina la Tanzania basi muwe na haya msiruhusu kuandikwa vitu kama hivi
 
Waganda warudi kwao,wanyarwanda warudi kwao na warundi warudi kwao full stop.

Hivi inakuaje mtu kukataa kurudi kwao???? Harafu rais wao anatukana rais ambae amevumilia kukaa na wananchi wako ambao ndio wana ongoza kwa ujambazi na ubaradhuli,bora wangekua raia wema lakini ni raia wanao hatarisha amani! They have to go!
 
Nadhani tuwe tunakubaliana na ukweli.
Mtoa mada ameeleza vizuri na inaonekana tatizo hilo la wahamiaji haramu linagusa eneo la magharibi tu!

Kama maeneo mengine ya mipaka yetu, tuna watu wa jamii kama siyo koo moja ukivuka mpaka. Ukiangalia Kusini, huwezi kuwatenga watu wa Mozambique na Mtwara kiasi kwamba kipindi cha uchaguzi, watu wa ng'ambo ya mpaka wanachagua uongozi wa upande mwingine. Ukiangalia wamasai, huwezi kutofautisha wa Kenya na Tanzania. Mkoa wa Mara huwezi kujua nani ni nani mpaka watu wanavuka mpaka kunyang'anyana mifugo. Nk.

Siku zijazo tusishangae wanasiasa wanatushambulia watu wa kusini wakisema wanaopinga bomba la gesi ni wa kutoka Msumbiji. Au tukasikia kuwa wamasai walioko Ifakara ni wanaotoka Kenya; pale wakuu wa nchi watakapotofautiana na nchi hizo jirani.

Ninachokiona, tusiweke siasa kwenye uhamiaji haramu. Kama tunafanya zoezi lisiwe zimamoto na lisiwaguse baadhi kama kweli tuna nia ya kumaliza tatizo.

Angalizo:
Kwa aina ya wahamiaji haramu, hususan wale wa mikoa ya Kagera na Kigoma, kuna makabila ya watusi na wahutu walioingia miaka mingi iliyopita. Hawa wote wamekuwa wakiishi kama watanzania kwa miaka mingi kutokana na historia ya kabla 1920 wakati tukiwa na Deutch East Africa ambapo Rwanda na Burundi zilikuwa sehemu ya nchi hiyo.

Tatizo linakuja pale tunapowafukuza upande mmoja wa wahamiaji hao kutokana na sura badala ya uharamu wao. Watusi wanatambulika kirahisi wakati wahutu wamejibatiza makabila ya hapa nchini na kukubalika. Mimi nasubiri watangaze kuwa iperation imemalizika ndo tutaanza kuwataja waliojificha, ingawa wengine wana nyadhifa za juu na bila shaka itakuwa vigumu kuwashughulikia.

Anjo
 
Kuna mtu kanitaja, na naomba akome. Mo M-tz bwana, ila nina sura ya Kitutsi. Kila anayeniona anasema we si Mtanzania, nikiwa sekondari kuna mwalimu alikuwa ananinyanyasa saaaaana! Ila mi Mhaya damudamu, ila kila siku i am considered a foreigner until I prove the contrary beyond reasonable doubt. Maisha yangu yamekuwa ya ku-prove, kwasababu kwanza watu hawaamini kuwa Mtutsi anaweza kuwa Mtanzania! Watanzania wengi tuna ujinga na ugullible fulani, kutokana na kubaguliwa nimeukataa ubaguzi, na Watutsi ni ndugu zangu. God bless Tutsis they brough cows to Kagera, wafugaji wazuri, si wanafiki na ni marafiki wa kweli. Na si majambazi kama watu wanavyodhani, tajiri wa mifugo ataenda kuteka magari? Ila kuna upotoshaji. Ila sharia zifuatwe basi,
 
mwananchi acha hizo mshikaji, unikome kabisa! Mi natoa comments kwasababu sipendi ubaguziiiii. kwanza mi mwenyewe nabaguliwa kwa sura yangu, ingawa mie Mtanzania, ubaguzi, ubaguziiiii! nchi hii bwana! Huyu mtoa mada ameongea vizuri sana, hata kwetu wa Wanyaihangiro (Masilingi, Salva mpoo) kuna issue hiyo. Ila tuwe makini tusiwakosee majira, wanasema kwa kihaya ati Ikina kya'amlyango otantara nokigwamu!
Ni mmoja wao na ukitaka kujua ni mmoja wao angalia treads zote zinazoongelea Rwanda uone mchango wake, wako wanajulikana JF Money Stunna, Mukamasimba, Nicolas, Kalisa, Tutajumbukirwa, etc
 
money stunna acha kutoa ugwini mwingi nenda kwenu,siku jw wakianza operation utajutia kuchelewa kwako!!!!acha kuadanganya wenzako!!!
 
Back
Top Bottom