Nani Mfalme wa muziki?

Nani Mfalme wa muziki?

el nino

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2013
Posts
4,712
Reaction score
5,070
Ukizungumzia reggae kuna Bob marley, ukija miondoko ya Rock kuna Elvis presley, Pop yupo mtu mzima Michael Joseph Jackson, Hip hop wapo Tupac na Notorious....je nani ameifanyia makubwa zaidi tasnia ya muziki kwa ujumla??

Michael kupitia album ya thriller alikuwa mwanamuziki wa kwanza mweusi nyimbo yake kupigwa vituo vya tv vya weupe, Michael jackson anatjwa kuwa msanii mwenye mafanikio zaidi katika kitabu cha guiness book of records...

Bob marley aliweza kuusambaza muziki wa reggae katika kona zote za dunia, hakuna mwanamuziki aliyeimba nyimbo za kuelimisha na zikatamba kumzidi Bob marley

Tupac na Notorious wakiwa kwenye ubora wao waliufanya muziki wa Hiphop ukubalike si tu katika jamii ya watu weusi , waliupeleka muziki wa Hiphop kutoka hatua moja hadi nyingine na kuufanya uwe maarufu zaidi..

Elvis presley mfalme wa miondoko ya rock, huyu mtu alichuana na the beatles vikali katika miaka ya 60 hadi umauti ulipomkuta, ni moja ya wanamuziki waliouza sana duniani as solo artist, huwezi taja miondoko ya rock bila kumtaja elvis...

Je, yupi anastahili kuwa mfalme wa muziki?
 
Nadhani Michael ni bora zaid, ndo maana akawa recognized na Guiness Book. Na hii ilitokana na mafanikio makubwa aliyoyapata katka mziki.
 
sawasawa mkuu
 
Kwa hapa kwetu kwa sasa naona ni Wazee Wa Ngwasuma, Msondo, na Extra Bongo Next Level.
 
Ukizungumzia reggae kuna Bob marley, ukija miondoko ya Rock kuna Elvis presley, Pop yupo mtu mzima Michael Joseph Jackson, Hip hop wapo Tupac na Notorious....je nani ameifanyia makubwa zaidi tasnia ya muziki kwa ujumla??

Michael kupitia album ya thriller alikuwa mwanamuziki wa kwanza mweusi nyimbo yake kupigwa vituo vya tv vya weupe, Michael jackson anatjwa kuwa msanii mwenye mafanikio zaidi katika kitabu cha guiness book of records...

Bob marley aliweza kuusambaza muziki wa reggae katika kona zote za dunia, hakuna mwanamuziki aliyeimba nyimbo za kuelimisha na zikatamba kumzidi Bob marley

Tupac na Notorious wakiwa kwenye ubora wao waliufanya muziki wa Hiphop ukubalike si tu katika jamii ya watu weusi , waliupeleka muziki wa Hiphop kutoka hatua moja hadi nyingine na kuufanya uwe maarufu zaidi..

Elvis presley mfalme wa miondoko ya rock, huyu mtu alichuana na the beatles vikali katika miaka ya 60 hadi umauti ulipomkuta, ni moja ya wanamuziki waliouza sana duniani as solo artist, huwezi taja miondoko ya rock bila kumtaja elvis...

Je, yupi anastahili kuwa mfalme wa muziki?
Wote hao hakuna kitu, mfalme ni Robert MArley ambaye ufalme wake ulivuka mipaka bila promo wala kushurutishwa na watawala. Muziki wake ulikuwa kweli zao la jamii yake, licha ya umaarufu wake bado akabaki kuwa mtu wa kawaida huko Trenchtown tofauti na wafalme promo ambao walikuwa maceleb.
 
huyu ndiye mfalme wa muziki duniani Bob Marley...jpg ameishi miaka 36 tu lakini kazi zake zinaheshimika na zitaendelea kuheshimika duniani
 
Kwa hapa kwetu kwa sasa naona ni Wazee Wa Ngwasuma, Msondo, na Extra Bongo Next Level.

Wimbo bora uliouzwa sana Africa Mashariki na kufahamika zaidi ni Kalubandika wa Maquiz wa 1984.Hao ngwasma ni wahuni wa mjini na nyimbo zao ni za Bar
 
Nina haja ya kukujibu maana kama ukisoma uliyo andika naona ushapata jibu lake. Nimesema kwa hapa kwetu kwa sasa (SASA in 2014) wewe unasema Maquis ya 1984....wapi na wapi?
 
getrude lwakatare akifuatiwa kwa mbaaali na mzee wa upako
 
Ukizungumzia reggae kuna Bob marley, ukija miondoko ya Rock kuna Elvis presley, Pop yupo mtu mzima Michael Joseph Jackson, Hip hop wapo Tupac na Notorious....je nani ameifanyia makubwa zaidi tasnia ya muziki kwa ujumla??

Michael kupitia album ya thriller alikuwa mwanamuziki wa kwanza mweusi nyimbo yake kupigwa vituo vya tv vya weupe, Michael jackson anatjwa kuwa msanii mwenye mafanikio zaidi katika kitabu cha guiness book of records...

Bob marley aliweza kuusambaza muziki wa reggae katika kona zote za dunia, hakuna mwanamuziki aliyeimba nyimbo za kuelimisha na zikatamba kumzidi Bob marley

Tupac na Notorious wakiwa kwenye ubora wao waliufanya muziki wa Hiphop ukubalike si tu katika jamii ya watu weusi , waliupeleka muziki wa Hiphop kutoka hatua moja hadi nyingine na kuufanya uwe maarufu zaidi..

Elvis presley mfalme wa miondoko ya rock, huyu mtu alichuana na the beatles vikali katika miaka ya 60 hadi umauti ulipomkuta, ni moja ya wanamuziki waliouza sana duniani as solo artist, huwezi taja miondoko ya rock bila kumtaja elvis...

Je, yupi anastahili kuwa mfalme wa muziki?

Kwa maoni yangu ni ngumu kumpata "mfalme wa muziki" kwa ujumla, ila ni rahisi kumpata mfalme wa aina fulani ya muziki! Nakubaliana na wanaokiri marehemu Michael Jackson ni mfalme wa Pop, lakini pia nathubutu kusema tangu afariki dunia mwaka 1981, siyo tu hakuna aliyemzidi bali hata kumkaribia Bob Marley kwa Reggae.
 
Bob marley ni miongoni mwa watu waliokuwa na kipaji na karisma ya ajabu ya kuuburi mazito kwa namna nyepesi zaidi. Aliutendea haki mziki kea namna ya kipeke.

Bila shaka Nyerere angekuwa hai angeweza kusema lukuki zaidi ya haya.
 
unapozungumzia muziki unaenda mbali zaidi ya ujumbe, kwa ujumbe sidhani kama kuna wakuchuana na bob ila kwa ujumbe na burudani kama nguzo za muziki sijaona wakuchuana na michael
 
Miaka ya 90 kwa hapa Bongo ilikuwa Vijana Jazz "Wana Sagha Rhumba," na kwa sasa kuna kina Extra Bongo Next Level, hii Vijana mpya chini ya Mgonahazeru, F.M. Academia, Msondo, Twanga bado iko juu, yaani vipaji ni vingi tu mkuu kusema bendi moja ndiyo kali zaidi si rahisi.
 
Back
Top Bottom