Elections 2010 Nani mbunge wa Vunjo

Herin Zakayo

New Member
Aug 10, 2010
1
0
Vunjo ni jimbo lililopo mkoani Kilimanjaro, wilaya ya Moshi vijijini. Jimbo la Vunjo limewahi kuwa chini ya wabunge kutoka vyama mbalimbali vya siasa kwa nyakati tofauti. Anaye maliza mda wake ni Mh. Kimaro kupitia CCM. Kwa tetesi zilizopo ni kwamba ameshindwa katika kura za maoni. Kipindi alichoshinda Mh. Kimaro alivishinda vyama vingine vilivyokuwa vimesimamisha wagombea ikiwemo TLP na CHADEMA. Msimu huu kupitia TLP anagombea Mh. MREMA wakati vyama vingine kama CCM bado havijasimamisha wagombea. Mrema aliyewahi kuwa mbunge na hata waziri miaka mingi iliyopita je leo anao uwezo wa kutosha kuliongoza jimbo hili? Haya ni moja ya maswali ya kujiuliza. Wana jamvi wenzangu ninyi mnasemaje?
 
Hapo ndipo kipimo cha akili za wana vunjo wa mjini na vijijini,maana wanamjua mrema na tabia zake.
Kama walivyo na ushirikiano kwenye kuchangishana pesa kwenye matatizo yao basi ni wakati wao kuchangishana akili zao kumkataa kibaraka mrema
 
Back
Top Bottom