Nani mabingwa wa huduma kwa wateja nchini?

Midevu

JF-Expert Member
Feb 11, 2012
272
435
Nadhani sote tunafahamu kuwa suala la huduma kwa wateja kwa asilimia kubwa ya biashara, mashirika na ofisi za umma ni janga la taifa.

Unaweza kufika kwenye biashara ya mtu na ukaishiwa kupata maumivu mpaka ukajiuliza kati ya wewe mteja na mwenye biashara nani mtafutaji. Watoa huduma wanatoa huduma muda watakaojisikia, kwa uharaka wanaoutaka. Wanataka kuulizwa maswali wanayotaka wao sio ya kwako mteja. Namba za simu zipo kumi na zote hazipatikani. Kwa wale wa ATCL unaweza kulazwa airport siku mbili huku ukila cancellations back to back. Kwenye maduka ya nguo wanakuhesabia nguo za kujaribu na usiponunua utaporomoshewa mvua ya matusi. Si ajabu ukakuta mhudumu wa biashara anagombana au kutukanana na mteja.

Matatizo ni mengi sana siwezi kutaja hata robo yake. Leo nisingependa kukaa kwenye mambo hasi.

Badala yake ningependa kujua kutoka kwenu, ni wapi umewahi kwenda zaidi ya mara moja na ukapata huduma nzuri sana mara zote? Ni biashara, shirika au ofisi ya umma ipi unaamini wanaongoza kwa kuwa na huduma nzuri kwa wateja Tanzania nzima?
 
Ofisi za umma ni za umma tu kwanza zimeghubikwa na RUSHWA yaani ili upate huduma nzuri ni hadi uwe mtoaji rushwa mzuri.

Sijawahi kuona shirika lenye customer care nzuri Tanzania serikalini au taasisi binafsi zaidi ya makahaba. Hawa wanakupa huduma zaidi hata ya ulichotoa.
 
TTCL wapo vizuri kuhuduma
 
Nadhani sote tunafahamu kuwa suala la huduma kwa wateja kwa asilimia kubwa ya biashara, mashirika na ofisi za umma ni janga la taifa.

Unaweza kufika kwenye biashara ya mtu na ukaishiwa kupata maumivu mpaka ukajiuliza kati ya wewe mteja na mwenye biashara nani mtafutaji. Watoa huduma wanatoa huduma muda watakaojisikia, kwa uharaka wanaoutaka. Wanataka kuulizwa maswali wanayotaka wao sio ya kwako mteja. Namba za simu zipo kumi na zote hazipatikani. Kwa wale wa ATCL unaweza kulazwa airport siku mbili huku ukila cancellations back to back. Kwenye maduka ya nguo wanakuhesabia nguo za kujaribu na usiponunua utaporomoshewa mvua ya matusi. Si ajabu ukakuta mhudumu wa biashara anagombana au kutukanana na mteja.

Matatizo ni mengi sana siwezi kutaja hata robo yake. Leo nisingependa kukaa kwenye mambo hasi.

Badala yake ningependa kujua kutoka kwenu, ni wapi umewahi kwenda zaidi ya mara moja na ukapata huduma nzuri sana mara zote? Ni biashara, shirika au ofisi ya umma ipi unaamini wanaongoza kwa kuwa na huduma nzuri kwa wateja Tanzania nzima?
BM Coach 😍😍😍😍
 
Back
Top Bottom