Elections 2010 Nani kuukwaa uwaziri mkuu?

Status
Not open for further replies.
duh akimuweka Magufuli nitajua siku zake za Kufa ziko karibu......, Kikwete na Hekima ni kama maji na mafuta lol:bowl:
 
kwa kweli Magufuli angekua the best option.lakini kwa ninavyofahamu utendaji wa JK na serikali yake hawawezi kukubali kumpa Magufuli uPM kwa sababu wanajua wakifanya hivyo JK hatasikika.kila chombo cha habari kitajaa sifa za Magufuli na JK atafunikwa TOTALY.JK analifahamu hilo vizuri sana ndio maana anajaribu kumtupa Magufuli wizara ambazo haziwiki lakini still tunaona hata kwenye hizo wizara bado anasikika kwa kazi zake nzuri.
 
Ni kweli watu hao watatu wanaweza kuwa wanazungumziwa kama possible candidate. Ukweli ni kwamba kwa unafiki wa serikali ya CCM Sitta hawezi kupewa u PM kwani ndiye aliyemtoa Uspika. Magufuli toka serikali ya awamu ya nne ianze JK kwa sababu anzozijua mwenyewe alimchukia tu. Magufuli ni mchapa kazi wa kweli na mfuatiliaji position ya u PM ingemfaa zaidi. Hivyo basi Pinda atarudishwa nafasi ya u waziri mkuu ingawa hawaivi kiivyo.

Issue hapa kwa CCM ni juu ya chama na sio nani anafanya kazi kwa manufaa ya wananchi nani atalinda maslahi ya viongozi wa chama. Kwa hao watatu Pinda ndio anaqualify zaidi. Get jamani serikali ya CCM si kwa ajili kuwatumia wananchi. Chama kwanza wananchi baadae ikibidi.

Umenena yoote: Kwanza magufuli hawezi kupewa u PM kwa sababu ya kufunikana!Kuna watu humo kwenye hicho chama wanaamini utendajii wa Magufuli ni sawa na ule wa EDward Sokoine kiasi anaweza mfunika hata presidaa!refer kashifa na uzushi uliokuwa ukiripotiwa na gatezti la Rai ukilenga kumdoofisha kisiasa bwana Magufuli(Phd).Hizo zote zilikuwa ni mbinu chafu za viongozi waliokuwa karibu na JK ingawa Jk hakuhusika katika uchafu huo.Jamaa zake walipandikiza chuki na yawezekana hata angetoswa kwenye uwaziri ila ndo washauri wakaona hali ya mambo isingekuwa shwari kwa jamaa kutoswa!!Akatupwa kwenye wizara zisizokuwa na profile kubwa bado jamaa profile yake ikazidi kuwa kubwa maana alifanya vitu ambavyo hakuna waziri tangu kuundwa kwa nchi alikwisha kufanya.Napenda msimamo wa magufuli,refer alivyokuwa akipingana kipindi hicho na Mwandosya akiwa waziri wa Mawasiliano na uchukukuzi kuhusu boti za Bakhresa kwenda Mwanza!!
Sitta hawezi kupewa uwaziri mkuu maana itakuwa kama kumkaribisha paka kwenye nyumba ya panya!
Mtoto wa mkulima anabaki kuwa ndio chaguo lao hao wanaopenda kuendelea kumfanya JK asiwe na makali!
CCM si mchezo aisee,nakumbuka JK wakati anaingia madarakani alikuwa na mchecheto kweli,full kutembelea wizara kila dei,na nakumbuka hata kuna wakati alikuwa akiimba wimbo wa Tanzania tanzania akawa very emotional mpaka katoa machozi kumbe jamaa wanamwambia subiri muda si mrefu utasahu ulikuwa unalilia nini!Kutoka hapo wakaanza kumpangia ziara za nje kila wiki ili kusudi habari awe anazipata tu kupitia kwa katibu wake.Aisee jamaa wajanja kweli JK angejua asingeamini mtu pale zaidi ya wife wake maana jamaa zake wa karibu wamemjaribu ndo nguzo yao ya kuficha maasi wanyofanya kwenye wizara!Sishangai kumwona pinda akirudi madarakani lakini nitashangaa sana kumwon aidha magufuli(Phd) ama Sitta mzee wa viwango akiwa PM.
 
Mambo ya kutaja taja watu in advance mtasababisha watu wakose UPM ivi ivi
 
Nadhani CCM "walisahau" wakati wa mchakato wa uraisi juu ya kuwa na wagombea wanawake kwa nafasi hiyo kwa sababu haijawahishikwa na mwanamke. Wakati wa kumtafuta spika CCM wakakambuka hilo kuwa ni zamu ya wanawake sasa katika nafasi hiyo kwa sababu haijawahi kushikwa na mwanamke. Vipi nafasi ya Uwaziri mkuu si haijawahi pia kushikwa na mwanamke. inakuaje? Tujadili wana JF.
 
Mambo ya kutaja taja watu in advance mtasababisha watu wakose UPM ivi ivi

umeona eeeh .mi ndo maana nimekaa kimya maana najua ninayemtaja ndo PM sasa asije kuukosa bure akaja nilaumu maana tunatoka kijiji kimoja kule Monduli
 
CCM wameshatuaonyesha mambo ni kupeanapeana tu na siyo uwezo!!! Ila kwa uPM nafikiri wanawake hawatakumbukwa anytime soon!!!
 
Gharama za kuhudumia waziri mkuu msataafu ni kubwa sana atakuwa rais wakwanza kutuingiza katika gharama hizo kwa kipindi kifupi sana cha miaka minne........
 
Kuna jitihada kubwa na fedha nyingi zinatumika ili EL awe PM 2010-15. Wazee wa CCM wakiwepo marais wastaafu wanafanya kila namna kumshawishi JK amteue EL kushika wadhifa huo kwa mara nyingine tena kwa kuzingatia kuwa "amejisafisha" kwa kashfa zilizomng'oa kwenye wadhifa huo. It's just the matter of time, let's wait and see.

Habari ndiyo hiyo:sad:
 
Kuna jitihada kubwa na fedha nyingi zinatumika ili EL awe PM 2010-15. Wazee wa CCM wakiwepo marais wastaafu wanafanya kila namna kumshawishi JK amteue EL kushika wadhifa huo kwa mara nyingine tena kwa kuzingatia kuwa "amejisafisha" kwa kashfa zilizomng'oa kwenye wadhifa huo. It's just the matter of time, let's wait and see.

Habari ndiyo hiyo:sad:

Ni masaa chini ya 24 yamebakiwa watanzania tumfahamu waziri mkuu, tungoje badala ya kukalia ubashiri
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom