Sam GM
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 535
- 30
Katika matukio ya siku hizi mbili zilizopita kuna kitu ambacho kila nikikisikia na kukifikiria naona kama vile sielewi vizuri labda wenye upeo zaidi watusaidie kuelewa. Huyu mtanzania mgonjwa wa akili alikuwa kalazwa Muhimbili, basi kichaa chake kikamtuma achukue stand ya kutundikia maji yanayoongezwa kwa wagonjwa, basi akaitumia hiyo stand kuwapiga wagonjwa wengine, wawili kwa bahati mbaya wakafariki papo hapo na wengine wanne wakachukuliwa kwa matibabu zaidi pamoja na upasuaji.
Katika Maendeleo ya tukio hili, mgonjwa huyu wa akili kapelekwa mahakamani na kashitakiwa kwa kesi za mauaji. Kwa utaratibu wa kawaida na katika sheria za utetezi (sanity) au kuwa na ugonjwa wa akili ni tetezi moja wapo inayotumika sana kuwatetea hata walio na akili na wakaachiliwa huru. Watanzania na akili zetu tena professionals kama huyu hakimu aliyeisoma na kusikiliza kesi, waziri wa afya aliyekimbilia kuteua tume ya kuchunguza hili jambo na huyu kichaa aliyefanya haya yote, ni nani mwenye ukichaa zaidi hapa?
Source: bbcswahili.com/08/14/08