GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 63,527
- 127,592
Kuna ' Kautamaduni ' kama si ' Kajitabia ' naona kanaanza Kuzoeleka au Kuota mizizi hapa Tanzania ambako sasa tunaona kila jambo likifanyika nchini hasa likiwa ni la ' Kimaendeleo ' utasikia hao hao waliolifanikisha wakisema kuwa halijawahi kutokea au kufanyika katika nchi zingine nyingi za Afrika.
Kwani huwa tunapambana na Maendeleo yetu ili tushindane na Mataifa mengine Afrika na Duniani kote au tunajitahidi Kujiboresha Sisi wenyewe tu? Na je kuna faida yoyote ile ambayo nchi imeipata pale inapoanzisha Miradi mbalimbali ya Kimaendeleo na Kujitapa kuwa haipo katika nchi zingine barani Afrika?
Kuna Mtu mmoja ( Simkumbuki jina ila nikimkumbuka nitamtaja ) aliwahi kusema kuwa sijui kuna aina ya Ndege ambayo ipo njiani au sijui imeshakuja kwamba haiko nchi zingine zote barani Afrika bali ni Tanzania tu pekee wakati kumbe hapo nchini Ethiopia, kule Egypt na hata South Africa ' nimedokezwa ' kuwa wanazo tena Siku nyingi tu kuliko Sisi.
Nani katufundisha aina hii ya Ushamba / Umbwigira Watanzania ya kutaka Kujifananisha na kama vile Kushindana na Mataifa mengine ya Afrika hasa katika Miradi mbalimbali ya Kimaendeleo inayohusisha Mioundombinu, Usafirishaji na Nishati? Tafadhali naomba tujijenge Kwanza Sisi kama Sisi na tuache kutaka ' Mashindano ' na Mataifa mengine kwani haina faida yoyote Kwetu zaidi tu ya Kutuchoresha kwa waliotutangulia Kimaendeleo na ambao Wao siyo Wazungumzaji / Wapayukaji hovyo kama Sisi bali ni Watendaji zaidi.
Nawasilisha.