Nani kasema unene dili

Nani kasema unene dili

Mwenzangu mimi nilikuwa nautamani sana unene ila kwa artical yako siutaki tena kabisaaaaa!!! kilicho nifanya niutake unene ni hivi. siku moja nilinunua nyumba pale kinondoni ni kama nilinunua kiwanja tu kwasbb ilikuwa ni mbovu. nyumba hiyo ilikuwa inakaribia barabara ya lami ila kwa mbele yangu ilikuwa na nyumba moja tu ndo ufikie lami. madalali waliniambia hata hiyo nyumba wenye nayo wanaiuza. hivyo nilifanya biashara ya kununua ile nyumba ya kwanza na nilikuwa na malengo ya kujenga ofisi ya ghorofa moja tu kwa mjengo wa kawaida. kwa bahati mbaya majirani walio kuwa mbele yangu wakitazama barabara ya lami waligombana baada ya baba yao kufariki hivyo wakashindwa kuelewana na hivyo waka kataa kuni uzia nyumba yao wakawa na kesi mahakamani kwasbb marehem alikuwa na wake wawili watoto 15!

Baada ya kuwa wamekataa kila mtu kivyake, nilikata tamaa ya kujenga ofisi yangu uku mbele yake kuna nyumba nyingine. hivyo nilimwambia dalali wangu anitafutie mteja nikauze tena then nikanunue nyumba nyingine. Nashukuru dalali alimtafuta mteja, na kumbuka mteja mwenyewe alikuwa ni waziri flan (.................) nilimwambia dalali leta mteja aone akiridhika na yuko tayari kufanya biashara niite. baada ya muda niliutwa na kuambiwa mheshimiwa flan anataka kununa nyumba yangu na hivyo niende ananisubiri. Baada ya kufika nilikuta gari aina ya Londcruza VX limepak pale na mimi pia nilikuwa na gari yangu. sasa basi niliposhuka kwenye gari yangu yule waziri nikamsalimia akaanza kuniangalia toka juu mpaka chini! akaniambia wewe mtoto tunamsubiria baba yako mwenye nyumba hii tufanye biashara yuko wapi?

Nikamjibu ni mimi ndiye mwenye nyumba hii! yule waziri akasema ni nyumba ya urithi? ni kasema hapana, akanijibu mmmmmm mbona kamwili kako kadogo dogo mimi nilifikiri baba yako anakuja!! ukweli tokea siku hiyo nilichukia kuwa mwembamba nikaanza kula lakini jamani wapi sinenepi!!! nilikula sana misosi unene nikawa sipati mpaka leo. tulifanya biashara ila yule mzee alionesha kunidharau kwasbb ya kuwa mwembamba. mkuu kwa artical yako si taki tena unene nitabaki tu hivyo mwaya!!!!!!!!!!. hivi ni kweli mili ingine hata ule vipi haizi kunenepa?

wabongo sie ni ajabu sana
yaani tunaamini mwenye maisha mazuri ni mnene au mwenye hela ni mbonge
ila tuangaliewenzetu wa nje wenye vipato wake kwa waumr walivyi na miili ya kawaida
huyo waziri mwehu tu
 
Afu nimegundua ni wanaume ndio wanachukulia wembamba wao kama tatizo...kwa sababu jamii inaheshimu wanaume warefu na waliojaa jaa..kuna kaka yangu hivyo hivyo alipalilia kitambi sasa hivi ameshapigwa red flag na doctor...kisukari inamnyemelea na hajafika hata 45...hatare kuliko tunavyodhania...
Alishaanza kuingia gym kabla ya doctor ku detect tatizo; lakini kilo zilikuwa hazishuki...sasa ameanza kutokula vyakula kibao...shida kweli kweli...nadhani vitisho vya doctor vitamfanya awe more serious...

Lakini mkuu, si unaona hata wewe mwenyewe ukiwa na kakitambi kamechomoza kidogo, ukivaa tai inatuna kidogo tumboni inapendeza? mwenzio mimi nikivaa tai inanyoka kabisa mpaka ulipo mkanda. sipendi kama nini!! niwai kwenda hospital TMJ dar, nilipo mwambia dr alinitoa nduki!! ila ukweli inapendeza mwanaume ukiwa na kakitambi kamechomoza kidogo.
 
Afu nimegundua ni wanaume ndio wanachukulia wembamba wao kama tatizo...kwa sababu jamii inaheshimu wanaume warefu na waliojaa jaa..kuna kaka yangu hivyo hivyo alipalilia kitambi sasa hivi ameshapigwa red flag na doctor...kisukari inamnyemelea na hajafika hata 45...hatare kuliko tunavyodhania...
Alishaanza kuingia gym kabla ya doctor ku detect tatizo; lakini kilo zilikuwa hazishuki...sasa ameanza kutokula vyakula kibao...shida kweli kweli...nadhani vitisho vya doctor vitamfanya awe more serious...

A friend of mine almost got stroke at 32, and he wasn't even that heavy na pia akagundua kuwa he was diabetic. Yaani sasa mwendo wake ni dirt za kufa mtu, shiiiider!
 
I wish tuone kuwa vyakula vyetu natural is the best food ever!, and it's organic if am not wrong. Ambavo in other places it's more expensive than processed food cause it's more healthy.
Halafu the notion that eti unene ndo deal huku kwetu?!, I will not buy it in a million years, it comes with the price, in the long run huo unene ndo unaleta kila kitu, heart disease sijui cholesterol, diabetes, you name it!, na kama huna tabia ya kufanya check up, you can just drop dead halafu watu waanze kusema, "mguu wa ntu huo"
 
Kumbe kamwili kangu dili eeh... Mie mwenyewe nilikuwa najichukia na kamwili kangu....

Siku moja nilikwenda hosp, Dr.akaniuliza unasoma wapi?

Siku nyingine nikawa napita Karume wacha wale wauza mitumba waniite "Wakusoma njoo kuna begi zuri hapa la shule" "Wakusoma njoo kuna viatu vya shule vya ukweli"...Lol mie mama mtu mzima nasoma khaaa..... Ila saiv najikubali jamani awali nilikuwa najiona kembambaaa mpaka natisha!!
 
hhaaaaa naomba nicheke mana ni kama umenisema mimi........mwe.....
 
Unene mzuri ni ule wenye shepu.
Tyta nisaidie picha.

c4fb4d540e5e3043204d91dd1c6811a2.jpg

KNY: #TeamWekaPicha
 
Last edited by a moderator:
Hahahaa.... Wakusoma kumbe tupo wengi eeeh!!! sasa ndio ukute na nywele unakata, ndio unakuwa Wakusoma square...

hahaaaa na nywele nilikata sasa ikabidi nianze kusuka tena mana ilikuwa ni shida......na nina mtoto nikawaambia huyu mwanangu ndo kabisa.......wanasema mtoto kazaa mtoto......
 
hahaaaa na nywele nilikata sasa ikabidi nianze kusuka tena mana ilikuwa ni shida......na nina mtoto nikawaambia huyu mwanangu ndo kabisa.......wanasema mtoto kazaa mtoto......

Hahahaaa.... Yaan hatutofautiani, ila mie kusuka bado. Nikimwambia mtu umri wangu anakataa... Et anasema ntakuwa kwenye 22/23yrs huwa nacheka mno.

Ila ni jambo la kushukuru make tuna kaudongo fresh..
 
Kuwa mnene ni hatari kwa afya sana, simshauri mtu awe mnene. Kuwa mwembamba haimaniishi kwamba una afya njema au ni ngumu kupata maradhi. Ishu hapa ni life style yako, kuna watu wembamba lakini wanabugia vyakula vya mafuta na mavinywaji ya sukari kama soda na the like cha kushangaza wapo vile vile,sasa mtu kama huyu siku akikumbwa na kisukari , shell au stroke anaona kama kaonewa. Mimi nimegundua kwamba watu wengi ninaowajua wenye kisukari ni wembamba kabisa. Nawashauri wale wanaotembea huku wamekaa wawe na utaratibu wa kufanya mazoezi ya kutembea mara moja moja, kisukari kinawakumba sana watu wa namna hiyo bila kujali ni Fidodido au Betina, unakuta mtu hata umbali mfupi tu, anachukua kaboksi kake
 
Hahahaaa.... Yaan hatutofautiani, ila mie kusuka bado. Nikimwambia mtu umri wangu anakataa... Et anasema ntakuwa kwenye 22/23yrs huwa nacheka mno.

Ila ni jambo la kushukuru make tuna kaudongo fresh..

kwanza nikiwaambia chuo nimemaliza lini ndo wanakataa kabisa......aisee...huu mwili sitauharibu hata nikinenepa kidogo sana......
 
Back
Top Bottom