kbmk
JF-Expert Member
- Feb 22, 2013
- 776
- 158
Hahahaaaa ncheke nnenepeee
Mwenzangu mimi nilikuwa nautamani sana unene ila kwa artical yako siutaki tena kabisaaaaa!!! kilicho nifanya niutake unene ni hivi. siku moja nilinunua nyumba pale kinondoni ni kama nilinunua kiwanja tu kwasbb ilikuwa ni mbovu. nyumba hiyo ilikuwa inakaribia barabara ya lami ila kwa mbele yangu ilikuwa na nyumba moja tu ndo ufikie lami. madalali waliniambia hata hiyo nyumba wenye nayo wanaiuza. hivyo nilifanya biashara ya kununua ile nyumba ya kwanza na nilikuwa na malengo ya kujenga ofisi ya ghorofa moja tu kwa mjengo wa kawaida. kwa bahati mbaya majirani walio kuwa mbele yangu wakitazama barabara ya lami waligombana baada ya baba yao kufariki hivyo wakashindwa kuelewana na hivyo waka kataa kuni uzia nyumba yao wakawa na kesi mahakamani kwasbb marehem alikuwa na wake wawili watoto 15!
Baada ya kuwa wamekataa kila mtu kivyake, nilikata tamaa ya kujenga ofisi yangu uku mbele yake kuna nyumba nyingine. hivyo nilimwambia dalali wangu anitafutie mteja nikauze tena then nikanunue nyumba nyingine. Nashukuru dalali alimtafuta mteja, na kumbuka mteja mwenyewe alikuwa ni waziri flan (.................) nilimwambia dalali leta mteja aone akiridhika na yuko tayari kufanya biashara niite. baada ya muda niliutwa na kuambiwa mheshimiwa flan anataka kununa nyumba yangu na hivyo niende ananisubiri. Baada ya kufika nilikuta gari aina ya Londcruza VX limepak pale na mimi pia nilikuwa na gari yangu. sasa basi niliposhuka kwenye gari yangu yule waziri nikamsalimia akaanza kuniangalia toka juu mpaka chini! akaniambia wewe mtoto tunamsubiria baba yako mwenye nyumba hii tufanye biashara yuko wapi?
Nikamjibu ni mimi ndiye mwenye nyumba hii! yule waziri akasema ni nyumba ya urithi? ni kasema hapana, akanijibu mmmmmm mbona kamwili kako kadogo dogo mimi nilifikiri baba yako anakuja!! ukweli tokea siku hiyo nilichukia kuwa mwembamba nikaanza kula lakini jamani wapi sinenepi!!! nilikula sana misosi unene nikawa sipati mpaka leo. tulifanya biashara ila yule mzee alionesha kunidharau kwasbb ya kuwa mwembamba. mkuu kwa artical yako si taki tena unene nitabaki tu hivyo mwaya!!!!!!!!!!. hivi ni kweli mili ingine hata ule vipi haizi kunenepa?