Nani kampa Membe cheo Cha mwanadiplomasia nguli?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Watanzania wengi tuna tabia ya kumpaka mafuta mtu kwa mgongo wa chupa, tunatabia ya kumwonea mtawala na tajiri huruma pale anapokuwa ananyanyasika au ameyumba kidogo lakini hatuna tabia za kulia na watu wazalendo wala wasiokuwa na kitu.

Mzee Membe amekuwa kwenye utawala na amekula mema ya nchi kwa miaka mingi na kipindi chote hicho hakuwa kujishusha na kuwa muungwana wa kuwasaidia maskini na wasiojiweza, hakuwahi kulia na waliolizwa na tawala alizokuwa anazitumikia bali miaka hiyo yote alikuwa upande wa ukandamizaji wa serikali dhidi ya wanannchi.

Leo amekaa pembeni tumeanza kumpa sifa zisizofaa, kumwita membe jasusi nguli bila kutueleza faida za ujasusi wake kwa Taifa ni kudhiaki majasusi Duniani. Kumwita Membe mwanadiplomasia nguli bila kutueleza ubobezi wake kwenye diplomasia ni kuwatukana wanadiplomasia Duniani.

Hakuna Mambo yakimaendeleo kwa nchi yaliyoletwa na mzee huyu ambayo tunayaona na ambayo yanatushawishi kuona kwamba anapaswa kuungwa mkono, huyu amejituliza na kujiunga kundi la wanyonge kwa sababu tu anataka wanyonge wamwinue arudi kileleni lakini akifika kileleni hawezi kuwakumbuka waliomnyanyua.

Angalia jimboni kwake amefanya nini hadi tuseme anafaha kutuongoza kama Taifa.

Hakuna mwanachama aliyelelewa na kukulia kwenye siasa za chama tawala anaweza kulia na wanaolia bali anao uwezo wakupaka mate machoni tukajua analia kumbe anatusindikiza kulia.

Let us be serious na tutoe sifa kwa watetezi wa Taifa letu waliokubali kuteswa kwa ajili yetu na bado wanapigania kutukomboa.

Mwisho, sikubaliani kabisa na kauli ya Jasusi nguli wala mwanadiplomasia nguli ...sifa hizi wapewe waliotenda Mambo ya kulikomboa Taifa siyo kutukandamiza.
 
Kwani akiitwa hivyo unapungua/unaengezeka nini au unapata faida/hasara gani?
Waache wanaopenda kumuita hayo majina wamuite hivyo.
Mbali na hapo ni wivu tu unakusumbua na chuki binafsi dhidi ya Mzee membe, Rais wetu 2020 kama Tundu lisu hatagombea.
 
"kumwita Membe jasusi nguli bila kutueleza faida za ujasusi wake kwa Taifa " Nahitajika nikukumbushe hapa tu

Hili swali muhimu ungemuuliza Dr. Kitine ndo angekupa jibu lilinyooka mpaka leo ana hasira nae
 
Ana lolote ni wapinzani ndio wanampa hayo majina mara kechero nguli utasikia wakisema jasusi wa kimataifa,wanataka kumkopa kwenye chaguzi zijazo si unajua ukiwa ikiongozwa na CHADEMA hawana rasilimali watu kwahiyo wanawatafuta malaya wa kisiasa wenye uroho wa madaraka kama walivyo wao alafu wanawajaza sifa za kijinga na kuwapa nafasi ya kupima upepo.
 
Ana lolote ni wapinzani ndio wanampa hayo majina mara kechero nguli utasikia wakisema jasusi wa kimataifa,wanataka kumkopa kwenye chaguzi zijazo si unajua ukiwa ikiongozwa na saccos ya chadomo hawana rasilimali watu kwahiyo wanawatafuta malaya wa kisiasa wenye uroho wa madaraka kama walivyo wao alafu wanawajaza sifa za kijinga na kuwapa nafasi ya kupima upepo.
ni manyumbu
 
Ana lolote ni wapinzani ndio wanampa hayo majina mara kechero nguli utasikia wakisema jasusi wa kimataifa,wanataka kumkopa kwenye chaguzi zijazo si unajua ukiwa ikiongozwa na saccos ya chadomo hawana rasilimali watu kwahiyo wanawatafuta malaya wa kisiasa wenye uroho wa madaraka kama walivyo wao alafu wanawajaza sifa za kijinga na kuwapa nafasi ya kupima upepo.
Mwisho wa siku roho inakusuta sababu unajua kwenye chaguzi ccm inaiba kura wazi wazi
Wananchi walishawakataa siku nyingi,bunduki ndio zinafanya muendelee kutawala,but tbe day is coming
 
Anajengewa daraja apate pa kuvukia...
Wanaomnadi wanaujua mshahara wao unapotoka.

Ni walewale wa kundi lilelile.

WANAJUANA!!!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mwana-diplomasia nguli na jasusi nguli... sawa kabisa, sawa kabisa.

Kwa nafasi yake kama nguli wa diplomasia, ni kwa namna gani kwa miaka 8 akiwa Waziri alihusika kufanikisha biashara ya Korosho kwenye jimbo moja la Mtama kuuzwa kama finished products na sio raw?

Obama alipokuja Tanzania alihamsisha, it is high time kwa Africa (Tanzania ikiwa sehemua ya Africa) kufanya biashara na Marekani. Yeye kama nguli wa diplomasia, alitumia vip unguli wake wa kijasusi pia, walau Mtama kwa kuanzia iwe beneficiary wa fursa za kibiashara zilizo Marekani.

Hizi ni fursa za AGOA. Kwa miaka 8 alifanya nini walau hata kuhasisha Watanzania wayajue haya?
Na kuna wana Mtama wangapi walau wanajihusisha na hilo soko ili kutoke hapo tu-build base ya kama haya alifanya, li-Tanzania hili angeliweza kiulaini kweli


Hivii kuna remarkable mark ipi ambayo ukifumba macho unaona, bila Bernard kuwa Waziri, Watanzania wasingepata hili?

Kuna wakati watu huwa tunawapa sifa ambazo hawana. Ila kwa wale watetezi, sio mbaya mkatuhubiria hayo mema ya msaka urais huyu aliengia kwenye 5-bora 2015 bila shaka tukasadiki.
 
Sijui ni kigezo au vigezo gani mnatumia vya ISO au TBS?
Neno lenyewe Intelligence Officer inakwenda na ukubwa wa IQ.
Wakati mwingine tungelinganisha Dr Salim Ahmed Salim kama kiwango cha Unit mmoja, gwiji la diplomasia,je Membe alifikia level gani?
 
Back
Top Bottom