Mwana-diplomasia nguli na jasusi nguli... sawa kabisa, sawa kabisa.
Kwa nafasi yake kama nguli wa diplomasia, ni kwa namna gani kwa miaka 8 akiwa Waziri alihusika kufanikisha biashara ya Korosho kwenye jimbo moja la Mtama kuuzwa kama finished products na sio raw?
Obama alipokuja Tanzania alihamsisha, it is high time kwa Africa (Tanzania ikiwa sehemua ya Africa) kufanya biashara na Marekani. Yeye kama nguli wa diplomasia, alitumia vip unguli wake wa kijasusi pia, walau Mtama kwa kuanzia iwe beneficiary wa fursa za kibiashara zilizo Marekani.
Hizi ni fursa za AGOA. Kwa miaka 8 alifanya nini walau hata kuhasisha Watanzania wayajue haya?
Na kuna wana Mtama wangapi walau wanajihusisha na hilo soko ili kutoke hapo tu-build base ya kama haya alifanya, li-Tanzania hili angeliweza kiulaini kweli
Hivii kuna remarkable mark ipi ambayo ukifumba macho unaona, bila Bernard kuwa Waziri, Watanzania wasingepata hili?
Kuna wakati watu huwa tunawapa sifa ambazo hawana. Ila kwa wale watetezi, sio mbaya mkatuhubiria hayo mema ya msaka urais huyu aliengia kwenye 5-bora 2015 bila shaka tukasadiki.