Habari wana MMU,
Nadhani mtakubaliana na mimi kwamba wanawake wasio na akili timamu wanaongoza katika suala zima la uzazi holela. Kuna wamama hapa mjini vichaa, yaani after 2 years ukimkuta hana kichanga basi ni bahati sana. Wengi wao wanazaa sana na nadhani sio kosa lao huenda wangekuwa na akili timamu wangeweza kujizuia.
Kinachonitatiza mimi, ivi nani huwapa ujauzito wanawake hawa? Ni vichaa wenzao wa jinsia ya kiume au ni wanaume wenye akili timamu? Kama ni vichaa wenzao wa kiume, kwa nini wakati mwingine unaweza kuta hapo mtaani hakuna chizi mwanaume lakini unamkuta chizi mwanamke ana mimba?? Hivi inawezekana kweli mwanaume mwenye akili timamu akafanya mapenzi na mwanamke kichaa?