Nani hufanya fujo wakati wa Uchaguzi?

Nani hufanya fujo wakati wa Uchaguzi?

mafutamingi

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2011
Posts
2,775
Reaction score
2,198
Hivi majuzi IGP Sirro alikaririwa akitoa onyo kali kwa wale watakaoleta fujo katika uchaguzi mkuu ujao. Onyo kama hili limekuwa likitolewa pia kwa nyakati mbali mbali na viongozi waandamizi wa serikali. Binafsi nimepiga kura kwa mara ya kwanza mwaka 1970, na baada ya hapo nimekuwa nikipiga kura kila wakati uchaguzi unapoitishwa.

Sijawahi kuona wala kusikia hata mara moja raia ambao ni wapiga kura au wasiokuwa wapiga kura wakifanya fujo wakati wowote wa uchaguzi mkuu. Si hivyo tu, sijawahi kuona wala kusikia hata viashiria vya fujo. Kila mara nimekuwa niona watanzania wanajipanga kwenye mistari na kupiga kura.

Naamini IGP Sirro anafahamu kuwa Watanzania ni watu watulivu sana na hawana tabia ya kufanya fujo wakati wa uchaguzi. Hata pale ambapo utata unapojitokeza kutoka na uzembe wa viongozi, watanzania wameendelea kuwa watulivu.

Kwa mfano, katika uchaguzi mkuu wa 1995 pale vituo vyote vya kupigia kura katika jiji la DSM vilijikuta vinashindwa kuendesha shughuli za kupigia kura kutoka na kukosekana kwa vifaa vya kupigia kura, wananchi waliendelea kuwa watulivu hata pale walipoambiwa kuwa uchaguzi kwa Dsm umefutwa hadi hapo baadaye.

Nadhani ingekuwa jambo bora kama IGP Sirro angewaonya viongozi wanaosimamia uchaguzi wasilete figisufigisu yoyote - maana huko ndo kwenye tatizo. Tatizo ambalo limekuwa likijitokeza siku za nyuma ni pale viongozi wanapokataa kutangaza matokeo kwa kutoa sababu zisizo na mashiko. Hawa ndo wanatakiwa waonywe na si wapiga kura.
 
Muda tu huwa jibu kwa Sasa muda Bado mtafanya manavyotaka lakini muda ukifika huna haja hata ya kutisha watu si unayaona yaliyomtokea Sudan!
 
ccm ndo wafanya fujo akiweo anayeonya
Lianzisheni tu afu tuwaombe polisi wakae pembeni ili muione nguvu ya umma halisi acha huo mnaoutamka kila uchao, CHADEMA yenyewe imebakia mitandaoni tu huku field wote huwaambii kitu kuhusu Magufuli.
 
Siku polisi watalogwa wakakaa pembeni hiyo ndio siku ccm itafutika milele. Hicho ni chama cha wazee na vijana waoga. Naomba hii ndoto yako itimie ili uone ukweli unaofunikwa na propaganda mfu.

S
 
Lianzisheni tu afu tuwaombe polisi wakae pembeni ili muione nguvu ya umma halisi acha huo mnaoutamka kila uchao, CHADEMA yenyewe imebakia mitandaoni tu huku field wote huwaambii kitu kuhusu Magufuli.
Hawajielewi hao
 
Siku polisi watalogwa wakakaa pembeni hiyo ndio siku ccm itafutika milele. Hicho ni chama cha wazee na vijana waoga. Miamba hii ndoto yako itimie ili uone ukweli unaofunikwa na propaganda mfu.

S
Hiyo Sacco's ya mtaa wa ufipa ndio iwe na nguvu(wanachama wa chadema) kuliko CCM? Huo Ni ukilaza!!! Unafikiri wahuni nyie mkijaribu fujo bila hata polisi uvccm tu inawaotosha bila hata mamilioni ya raia ambao Ni wanachama na wafuasi wa CCM
 
Hivi majuzi IGP Sirro alikaririwa akitoa onyo kali kwa wale watakaoleta fujo katika uchaguzi mkuu ujao. Onyo kama hili limekuwa likitolewa pia kwa nyakati mbali mbali na viongozi waandamizi wa serikali. Binafsi nimepiga kura kwa mara ya kwanza mwaka 1970, na baada ya hapo nimekuwa nikipiga kura kila wakati uchaguzi unapoitishwa.

Sijawahi kuona wala kusikia hata mara moja raia ambao ni wapiga kura au wasiokuwa wapiga kura wakifanya fujo wakati wowote wa uchaguzi mkuu. Si hivyo tu, sijawahi kuona wala kusikia hata viashiria vya fujo. Kila mara nimekuwa niona watanzania wanajipanga kwenye mistari na kupiga kura.

Naamini IGP Sirro anafahamu kuwa Watanzania ni watu watulivu sana na hawana tabia ya kufanya fujo wakati wa uchaguzi. Hata pale ambapo utata unapojitokeza kutoka na uzembe wa viongozi, watanzania wameendelea kuwa watulivu.

Kwa mfano, katika uchaguzi mkuu wa 1995 pale vituo vyote vya kupigia kura katika jiji la DSM vilijikuta vinashindwa kuendesha shughuli za kupigia kura kutoka na kukosekana kwa vifaa vya kupigia kura, wananchi waliendelea kuwa watulivu hata pale walipoambiwa kuwa uchaguzi kwa Dsm umefutwa hadi hapo baadaye.

Nadhani ingekuwa jambo bora kama IGP Sirro angewaonya viongozi wanaosimamia uchaguzi wasilete figisufigisu yoyote - maana huko ndo kwenye tatizo. Tatizo ambalo limekuwa likijitokeza siku za nyuma ni pale viongozi wanapokataa kutangaza matokeo kwa kutoa sababu zisizo na mashiko. Hawa ndo wanatakiwa waonywe na si wapiga kura.

Cccm wapo nyuma ya Hilo.Kila uchaguzi ni lzm watoe kafara
 
Hiyo Sacco's ya mtaa wa ufipa ndio iwe na nguvu(wanachama wa chadema) kuliko CCM? Huo Ni ukilaza!!! Unafikiri wahuni nyie mkijaribu fujo bila hata polisi uvccm tu inawaotosha bila hata mamilioni ya raia ambao Ni wanachama na wafuasi wa CCM

Ccm ingekuwa na wafuasi mamilioni isingetemea vyombo vya dola kutangazwa washindi. Nasema hivi, polisi wakosee tu wawaache mjitegemee, ccm itageuka historia.
 
Hawa ni wale aliwazungumzia Mungu kuwa"wana masikio lkn hawasikii wana macho lkn hawaoni wamepewa akili lkn hawzitumii ipasavyo bac hao ni kama wanyama,lkn ni bora wanyama kuliko hao".Hawatoelewa mpk kufa kwao.
Ccm ingekuwa na wafuasi mamilioni isingetemea vyombo vya dola kutangazwa washindi. Nasema hivi, polisi wakosee tu wawaache mjitegemee, ccm itageuka historia.
 
Hivi majuzi IGP Sirro alikaririwa akitoa onyo kali kwa wale watakaoleta fujo katika uchaguzi mkuu ujao. Onyo kama hili limekuwa likitolewa pia kwa nyakati mbali mbali na viongozi waandamizi wa serikali. Binafsi nimepiga kura kwa mara ya kwanza mwaka 1970, na baada ya hapo nimekuwa nikipiga kura kila wakati uchaguzi unapoitishwa.

Sijawahi kuona wala kusikia hata mara moja raia ambao ni wapiga kura au wasiokuwa wapiga kura wakifanya fujo wakati wowote wa uchaguzi mkuu. Si hivyo tu, sijawahi kuona wala kusikia hata viashiria vya fujo. Kila mara nimekuwa niona watanzania wanajipanga kwenye mistari na kupiga kura.

Naamini IGP Sirro anafahamu kuwa Watanzania ni watu watulivu sana na hawana tabia ya kufanya fujo wakati wa uchaguzi. Hata pale ambapo utata unapojitokeza kutoka na uzembe wa viongozi, watanzania wameendelea kuwa watulivu.

Kwa mfano, katika uchaguzi mkuu wa 1995 pale vituo vyote vya kupigia kura katika jiji la DSM vilijikuta vinashindwa kuendesha shughuli za kupigia kura kutoka na kukosekana kwa vifaa vya kupigia kura, wananchi waliendelea kuwa watulivu hata pale walipoambiwa kuwa uchaguzi kwa Dsm umefutwa hadi hapo baadaye.

Nadhani ingekuwa jambo bora kama IGP Sirro angewaonya viongozi wanaosimamia uchaguzi wasilete figisufigisu yoyote - maana huko ndo kwenye tatizo. Tatizo ambalo limekuwa likijitokeza siku za nyuma ni pale viongozi wanapokataa kutangaza matokeo kwa kutoa sababu zisizo na mashiko. Hawa ndo wanatakiwa waonywe na si wapiga kura.
Ukiona baba mwenye nyumba anapiga kelele sana kuonya wanawe wasiende ngomani basi jua kama yeye si mpiga ni mcheza ngoma ama shabiki.
Mara zote tafiti zimeonesha kote duniani chanzo cha vurugu za chaguzi hutokana na vyombo dola kutumiwa na watawala
 
Ni ccm wakiongozwa na policeccm na greenguard
Hivi majuzi IGP Sirro alikaririwa akitoa onyo kali kwa wale watakaoleta fujo katika uchaguzi mkuu ujao. Onyo kama hili limekuwa likitolewa pia kwa nyakati mbali mbali na viongozi waandamizi wa serikali. Binafsi nimepiga kura kwa mara ya kwanza mwaka 1970, na baada ya hapo nimekuwa nikipiga kura kila wakati uchaguzi unapoitishwa.

Sijawahi kuona wala kusikia hata mara moja raia ambao ni wapiga kura au wasiokuwa wapiga kura wakifanya fujo wakati wowote wa uchaguzi mkuu. Si hivyo tu, sijawahi kuona wala kusikia hata viashiria vya fujo. Kila mara nimekuwa niona watanzania wanajipanga kwenye mistari na kupiga kura.

Naamini IGP Sirro anafahamu kuwa Watanzania ni watu watulivu sana na hawana tabia ya kufanya fujo wakati wa uchaguzi. Hata pale ambapo utata unapojitokeza kutoka na uzembe wa viongozi, watanzania wameendelea kuwa watulivu.

Kwa mfano, katika uchaguzi mkuu wa 1995 pale vituo vyote vya kupigia kura katika jiji la DSM vilijikuta vinashindwa kuendesha shughuli za kupigia kura kutoka na kukosekana kwa vifaa vya kupigia kura, wananchi waliendelea kuwa watulivu hata pale walipoambiwa kuwa uchaguzi kwa Dsm umefutwa hadi hapo baadaye.

Nadhani ingekuwa jambo bora kama IGP Sirro angewaonya viongozi wanaosimamia uchaguzi wasilete figisufigisu yoyote - maana huko ndo kwenye tatizo. Tatizo ambalo limekuwa likijitokeza siku za nyuma ni pale viongozi wanapokataa kutangaza matokeo kwa kutoa sababu zisizo na mashiko. Hawa ndo wanatakiwa waonywe na si wapiga kura.
 
Sio kweli chama dola kinashinda kila chaguzi halafu kina dola kivipi kianzishe fujo? Ni kitu ambacho hakiwezekani!!! Halafu unadanganya kuhusu utafiti Tena unaenda mbali kusema duniani hebu tuwekee huo utafiti wa duniani Tena sikuulizi Nani alietafiti Ila usikimbie
Kamata ilani katika kwa bidii haya mengine yako juu ya upeo wako
 
Lianzisheni tu afu tuwaombe polisi wakae pembeni ili muione nguvu ya umma halisi acha huo mnaoutamka kila uchao, CHADEMA yenyewe imebakia mitandaoni tu huku field wote huwaambii kitu kuhusu Magufuli.
Lazima Kuna Mwisho WA Kila kitu,,hata kama hautaishi Ku ona Mwisho huo!.. KAMA MAGUFULI ANAJUA HAYO ARUHUSU TUME HURU
 
Back
Top Bottom