Mh!acha niwe mkweli tu,mi nilipoingia chuo mwaka wa 1,ARU,mpenzi wangu alijiunga chuo cha mzumbe.Ukweli ni kwamba huyu binti nilitokea kumpenda kupindukia lakini yeye ndo alianza kunitongoza nikaingia line,usicheke.Lakini mara baada ya kutenganishwa na vyuo,mapenzi yake yakawa bariidi,nikipiga simu yuko busy,nikituma sms anajibu after 2 days.Huku nalia kwa uchungu,nilimmwaga kabla yeye hajafikia hatua ya kunimwaga,lakini wanawake hawaeleweki,nilibadili mpaka namba ya simu,lakini ananifuatilia mpaka Facebook eti ooh shetani,tusahau yaliyopita turudiane,jamani!.