Mahusiano yangu yapo kwenye mgogoro, msaada unahitajika

Prince Mhando

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
9,584
12,064
Mimi ni kijana ambae nipo kwenye umri wa kuuvuka ujana na kuuendea utu uzima. Miaka ya nyuma mara kadhaa nimeshawahi kuumizwa sana kwenye mahusiano. Ilifikia kipindi nikaamua kuyapa kisogo mahusiano. Mbinu haswa niliyokuwa naitumia ni ku hit and run.

Ila baadae miaka 6 nyuma nilikutana na msichana wa KIMACHAME nilimpenda akanipenda ila kwa bahati mbaya alikuwa na mpenzi wake tuseme walikuwa kwenye long-distance relationship, hope uzalendo ulimshinda huyu msichana tukajikuta tumeingia kwenye mahusiano, akamuacha mpenzi wake waliosoma wote chuo huko Mwanza.

Miaka mitatu baada ya mahusiano yetu nilibahatika kumpa mimba huyo msichana, kuna siku mimba ilivyokuwa na miezi 5 aliondoka nyumbani from no way... kuanzia saa 11 jioni akarudi saa 2 usiku nilikasirika sana lakini siku muuliza ukizingatia ilikuwa mimba yake ya kwanza.

Maisha yaliendelea tukawa na furaha sana akajifungua mtoto wa kiume. Kipindi chote hiki huyu msichana alikuwa na kazi ambayo kwa kiasi fulani ilikuwa inamuingizia kipato, sikuwahi kujua analipwa kiasi gani na wala sikuwahi kabisa kujua tarehe za mshahara huwa anapokea tarehe ngapi....kiukweli sikuwa na kazi na majukumu yote alikuwa anafanya mwenyewe...nilijitahidi kutafuta kazi {kipindi hicho} lakini jitihada zilikuwa zinagonga mwamba.

Ni mwaka sasa tokea nipate kazi ninayoifanya, kazi yangu hii inanifanya niwe narudi nyumbani asubuhi... hivyo kwa wiki nalala nyumbani mara moja tu...! Mwaka huu mwezi wa tano mwenzangu ni kama alipoteza kabisa hisia za mapenzi na mimi akawa hataki kabisa kushirikiana na mimi kwenye tendo {mnyanduano} nikawa nikimgusa tupo kitandani haonyeshi mshituko wowote wala haonyeshi ushirikiano unaweza ukampapasa masaa mawili mfululizo bila yeye kuonyesha mshituko wowote huku nikona dalili zote za yeye kuwa macho.

Niliivumilia hiyo hali kwa muda wa miezi miwili. Ni kama vile alikuwa ananitafutia sababu mara kwa mara alikuwa na tabia ya kuchunguza simu yangu haswa nikiwa nimelala.. sasa kipindi hiki ambacho alikuwa ananinyima tendo nilitafuta mchepuko nikawa namalizia hamu zangu huko. Baadae huyu msichana alifumania meseji za mchepuko, ikawa kesi nikamkumbusha kuwa umeyataka mwenyewe mimi sio hanisi tuwe tunalala kitandani kama mtu na dada yake.

Tuliyasuluhisha yakaisha tukanyanduana.... baadae akaanzisha tabia ya kumlaza mtoto katikati yetu... yaani nikitaka game hadi nimruke mtoto kisha ndipo nipige game na tokea mwezi wa nne hajawahi hata siku moja kuonyesha dalili kuwa ana hamu ya kunyanduana yani mpaka nimuanze. Kiukweli sijafunga nae ndoa ila kwa muda wote tulioishi sisi ni wanandoa tunao subiri mambo yakae sawa tuibariki ndoa yetu.

Nimeivumilia halii hii ndugu zangu najiona uzalendo unanishinda. Ajabu ni kuwa hana furaha na mimi ila kuna kijana mmoja akija huwa namuona anakuwa na furaha, atacheka hadi jino la ndani kabisa utaliona...

Mwenzangu hataki kunisikia kabisa. Kimaadili mimi ni muislam vile vile niliwahi mara nyingi kumuelekeza juu ya jinsi ninavyotaka awe lakini hakuwahi kabisa kufuata maadili ninayo yataka mimi.... Nimeamua kumuacha japo kwa shingo upande ninawaomba wana JamiiForums mnisaidie mawazo nipo njia panda ndugu yenu​
 
Wewe ndo Fevushka unayekatikaga pale Samaki Samaki M/City?..Maana namuona kwenye Avatar hapo

Anyway..muulize nini shida hasa,na kama amechoka kukaa hapo muache aondoke..hii dunia sio ya kubembeleza sana pale mtu anapokuwa hana interest tena na wewe
 
Pole,
Ila inaonyesha huyo mwanamke hakukupenda toka mwanzo, desperation ya mwanaume wake kuwa mbali ndiyo iliyomleta kwako, hivyo ile excitement imeisha ikaondoka na hisia zake,

Mambo ya ndoa yananizidi uwezo, ngoja wanandoa wenzio waje kukupea somo, ujue cha kufanya..!!
 
asante...kikweli na muwaza sana mtoto wangu...kwa kipato changu cha sasa sina uwezo wa kukigawa mara mbili....hapa nitachanganyikiwa...tu
 
Huwa nawashangaa sana wanaume waliooa af wanalalamika wananyimwa papuchi..naelewa unaweza kunyimwa one day mama hajiskii lakini in long run bado unakuwa unabaniwa i don't get it..

Japo case yako ni tofauti..wewe hujamuoa
 
Wewe ndo Fevushka unayekatikaga pale Samaki Samaki M/City?..Maana namuona kwenye Avatar hapo

Anyway..muulize nini shida hasa,na kama amechoka kukaa hapo muache aondoke..hii dunia sio ya kubembeleza sana pale mtu anapokuwa hana interest tena na wewe
asante sana kaka...nimepanga kesho nikazungumze nae kwa kirefu...ila nia yangu ni kumuacha japo kwa shingo upande
 
Huwa nawashangaa sana wanaume waliooa af wanalalamika wananyimwa papuchi..naelewa unaweza kunyimwa one day mama hajiskii lakini in long run bado unakuwa unabania i don't get it..

Japo case yako ni tofauti..wewe hujamuoa
ni kweli sijaoa kaka lakini tunaishi wote takribani miaka 6 sasa...hapo kunautofauti gani na mtu alie oa...? harafu wazazi wote wanafahamiana...si ni kama wana ndoa tu hadi tumezaa...kweli
 
Haujaonyesha kama anachepuka.

Haujaonyesha kama ana mapungufu mengine zaidi ya kukataa ngono.

Ninaweza kukusaidia moja wapo kati ya mawili;
1) Kujaribu kuongea na mwenzi wako. Ili upate muafaka wa kila unachojiuliza.
2) Kukusaidia to walk you through huu uamuzi uliouamua.

Au waweza chagua vyote viwili. Chochote utakachochagua kitakua na friendly charges, karibu ofisini Msimbazi Round about au nicheki kwenye namba yangu.
 
asante sana....
 
Jomba Jomba..kesho napo kichapo

Sema fresh kwa kumshauri mwana
 
Hakuna Uislam wa namna hiyo! Hakuna mafundisho ndani ya Uislam yanayoruhusu mtu kuishi na kumzalisha binti wa watu kabla ya kumuoa na wala hakuna kubariki ndoa kwenye Uislam. Hayo mengine watakushauri wengine.
asante.....ni shauri kama vile ungemshauri mtu ambaye yupo kwenye ndoa...hakuna binaadam alie kamirika kumbuka
 
Back
Top Bottom