Nani atamfunga paka kengele?

CK Allan

JF-Expert Member
Aug 14, 2013
2,729
5,918
hapo zamani za kale kulikua na kijiji kimoja cha panya, kijiji kile kilikua na panya wengi na waliendelea kuongezeka siku hadi siku! ilitukia siku moja panya wakaanza kupotea, na wengine wakakutwa porini na sehemu nyingine wakiwa tayari wamekufa, wengine walikutwa wakiwa hawana vichwa, au viungo mbali mbali! mateso yalizidi sana, panya waliokua na ndugu zao sehemu za mbali walijitahidi kukimbia hali ile ya hatari, hata hivyo katika hali isiyokua ya kawaida muuaji wa panya akajitokeza hadharani na siku nyingine alivamia mchana kabisa na kuondoka na panya.....PAKA! hakika huyu ndie alikua adui mkubwa wa panya! jina la paka likawa maarufu sana katika jamii ile ya panya kwa kipindi kile! hatimaye hali ya hatari ikatangazwa na mfalme wa panya na siku ya mkutano mkuu ikatangazwa panya wote wakusanyike kwa ajili ya kujadiliana juu ya nini kifanyike kumdhibiti yule paka!

basi siku ikawadia, kama ilivyo ada wengine walikuja kwenye mkutano wakiwa na mapanga, marungu, sime n.k katika kuonyesha kukerwa na paka! penye wengi pana mengi na mjadiliano yakaanza! hakukua na majibu ya maswali mengi ndipo mpambe mmoja wa mfalme akatoa wazo...
"mkuu mimi nashauri tumfunge paka kengele! ilikila anapopita tusikie na hivyo itakuwa rahisi kwetu kujilinda!" baada ya hoja hii zilisikika kelele za shangwe na vifijo na nderemo! mpambe wa mfalme akabebwa juu juu na ilkabidi mfalme afanye kazi ya ziada kutuliza ule umati!

mfalme mwenyewe alifurahi sana, akaamuru yule mpambe avikwe nguo za thamani apewe nyumba na mashamba na kila kitu alichohitaji! ,falme pia akaamuru watu washerekee wasiende kazini wakae nyumbani kwani sasa dawa ya adui yao imepatikana! wakati sherehe zikiendelea mzee gwaya yeye machozi yalikua yakimtoka alishindwa hata kusimama na alijaribu kunyoosha mkono wake ili atoe wazo lake lakini hakuna aliyemsikiliza kila mmoja likua bize kufurahia na mkutano ukaishia pale!
kijiji kizima ilikua ni mzee gwaya tu ambaye hakufanya sherehe yoyote, hakula wala kunywa na habari zikamfikia mfalme! mfalme akaamua gwaya akamatwe kwa kuwa eti anashirikiana na paka kuhujumu panya wengine! ikumbukwe kua pamoja na ile hoja kutolewa bado panya waliendelea kupungua! hivyo mzee gwaya akachukuliwa kama mhaini na akafungwa jela!

mzee gwaya akiwa katika matesomakali gerezani aliomba kuongea na mfalme! mfalme akakataa kata kata! mfalme alisema yeye ni mtetezi wa panya hawezi kukaa na mhaini!
mzee gwaya akiwa peke yake katika chumba cha gereza akatumia damu yake kuandika maandishi makubwa ukutani , kisha akakata roho, akafa!
kila mmoja aliingia pale chumbani aliona yale maandishi akasoma akatoka nje mbio! hakuna aliyekua tayari kusema nini kilikua kimeandikwa! hatimaye habari zilifikakwa mfalme ambaye aliamua kwenda mwenyewe kusoma maandishi hayo! mfalme baada ya kuona ujumbe ule aliishiwa nguvu! aliita madaktari na waganga wajaribu kumfufua mzee gwaya lakini hakuamka! mzee Gwaya aliashaenda mbele ya haki! mfalme alilia sana.... hata baada ya kurudi nyumbani mfalme alishindwa kula wala kulala... maneno yale yalijirudia kichwani kama mwangi...
'NANI ATAMFUNGA PAKA KENGELE?'

____MWISHO____
 
Back
Top Bottom