Nani atakaye mfunga paka kengele?

Nyavinene

Senior Member
Jul 28, 2020
164
173
Kulikuwa na duka Kuubwa la Vyakula na Vinywaji katika mji. Panya Wengi waliishi katika duka hilo la vyakula na vinywaji. Chakula kilikuwa ni kingi sana kwa ajili yao. Walikula kila kitu na kuharibu mifuko yote ya vyakula. Waliharibu pia mikate, biskuti na matunda ya duka.

Mwenye duka alishikwa na wasiwasi kweli. Hivyo, yeye alipata wazo "mimi lazima ninunue paka na atakaa humu ndani ya hili duka. Kufanya hivo naweza kuokoa mambo yangu."

Alimnunua Paka mmoja mzuri, mkubwa na kisha kumwacha pale. Paka alikuwa na wakati mzuri wa kuwinda panya na kuwaua. Panya hawakuweza kuzunguka kwa uhuru sasa. Waliogopa kwamba wakati wowote paka ange wakamata na kuwala.

Panya walitaka kufanya kitu fulani. Wakaitisha mkutano na wote wakasema "Ni lazima kujikwamua na paka. Je, kuna mtu ana maoni?"

Panya wote wameketi na kuogopa. panya mmoja mwelevu alisimama na akasema, "paka hatembea kwa upole. Hilo ni tatizo. Kama tunaweza kumfunga kengele kwenye shingo yake, basi mambo yatakuwa mazuri. Tunaweza kujua harakati zake zote ".

"Ndiyo, hilo ni jibu sahihi," walisema panya wote. panya wa miaka mingi alisimama polepole na akauliza, "Ni Nani atakaye Mfunga paka kengele? " Baada ya muda mchache hakukuwa na yeyote wa kujibu swali hili.
 
Mkuu
Nipo Tupo Pamoja Ila Bado Sijapata Kengele Zaidi Wadau Wanaendelea Kusema Biashara Ya Kengele Hailipi.
Nina Matumaini Nitaipata Halafu Zoezi Linaendea

Halafu ile thread naona kama imefutwa, nimeitafuta ili niweke reference ila sijaona kitu.
 
Kwahiyo unatutukania mtukufu, mheshimiwa raisi wetu kwa mafumbo si ndio?!
 
Hawa jamaa kuna muda wanaondoa thread halafu ukijiuliza sababu hupati jibu.
Haa😁😂
Yaani Thread Haina Ukakasi Wowote Lakini Ndiyo Hivyo Ukizingatia Vigezo Vya Kuwepo Jukwaa Husika La Matangazo Ni Sahihi

Tena Mimi Niliiweka Jukwaa La Habari Mchanganyiko Wao Wakaipeleka Jukwaa La Matangazo Baadaye 😏😐🤔😑😶😶
Naona Wameifuta. Mods Aliye Zamu Rudishe Thread Watu Sasa Hivi Wanatafuta Kengele (Bell)

Tumfunge Paka!!🤩
 
Viongozi Mlio Zamu Muda Huu
Moderator
Active
Fanyeni Mpango Mrudishe Thread Ya Isemayo
Tanzania Wapi Nitapata Sehemu Wanapouza Kengele (Bell)
download.jpeg.jpg
 
Viongozi Mlio Zamu Muda Huu
Moderator
Active
Fanyeni Mpango Mrudishe Thread Ya Isemayo
Tanzania Wapi Nitapata Sehemu Wanapouza Kengele (Bell)
Anzisha nyingine tu kaka ili tuweze kuchangia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom