Nani atailipa Standard Chartered Bank Hong Kong (SCB HK)?

Nani atailipa Standard Chartered Bank Hong Kong (SCB HK)?

Mkuu Shark ninaamini tatizo sio wanasheria bali tatizo ni wale wanaopanga safu ya wanasheria.

Viongozi wetu hawana uzalendo na kwa maana hiyo, hata mawakili wanaowaweka wanakuwa ni wapiga dili tu. Refer Mkono & Co Advocates kwenye suala la TANESCO.

KAMPUNI ya mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono (Pichani) inadaiwa kulipwa na TANESCO, takriban shilingi 18 bilioni kwa huduma ya ushauri, chanzo Changu kimegundua. Nyaraka ambazo Chanzo hicho kimeona zinaonyesha kuwa tayari kampuni ya Mkono imetumia kiasi hicho kutoka shirika la umeme linalolegalega kifedha. Mkono na kampuni yake ya Mkono & Co. Advocates ya jijini Dar es Salaam, amekuwa mshauri wa kisheria na wakili wa TANESCO tangu Mei 1995.

Nyaraka zinaonyesha kuwa shilingi 18 bilioni zimelipwa kwa ushauri na utetezi ambao kampuni ya Mkono imefanya katika minyukano ya kudaiana kati ya TANESCO na kampuni nyingine ya umeme, Independent Power Tanzania Limited (IPTL). Hivi sasa uhusiano wa TANESCO, kampuni ya umeme ya serikali na kampuni ya Mkono, umekuwa wa kilio kama mawasiliano ya ndani yanavyoonyesha.

Moja ya mawasiliano hayo ni barura ya Jenerali Robert Mboma,Aliyekuwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi TANESCO, ambayo inalalamikia matumizi ya mabilioni ya shilingi ya kampuni ya Mkono, tena bila mafanikio. Barua ya Mboma ya 10 Septemba 2013; kwenda kwa Mkono, inalalamikia matumizi ya kiasi hicho cha fedha katika mashauri ambayo yamechukua muda mrefu na bila kuleta tija. Barua yenye Kumb. Na. SEC.427/IPTL/9/2013; ambayo imebeba kichwa cha maneno kisemacho, “Ushauri ambao kampuni yako imetoa kwa Tanzania Electric Supply Company Limited,” imenukuliwa kwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.

"Kwa sasa, kulingana na kumbukumbu tulizonazo, kampuni yako imekwishatumia takribani Sh. 18 bilioni kama gharama za ushauri katika kusimamia suala hili kufikia Aprili 2013,” anaeleza Jenerali Mboma. Anasema, “Hiki ni kiasi kikubwa mno cha fedha za walipa kodi ambazo zingeweza kuwekezwa kwenye miradi mingine ya uzalishaji kwa manufaa ya Watanzania wote.” Kana kwamba hiyo haitoshi, Mboma anasema, “TANESCO inataka ieleweke kuwa inasikitishwa na namna kampuni yako ilivyotoa ushauri wa kisheria kuhusiana na mivutano iliyohusu Mkataba wa mauziano (PPA) wa tarehe 26 Mei 1995 kati yetu na IPTL, kwa vile ulivyotushauri na katika kuisimamia kesi tangu ilipofunguliwa mwaka 1998.”

TANESCO sasa inatuhumu kampuni ya mkono kutoishauri vizuri hadi kupoteza kesi yake dhidi ya IPTL. Kesi ambayo TANESCO inasema imeipoteza kwa kutoshauriwa vizuri inahusu mkataba wa kununua umeme – Power Purchase Agreement (PPA) wa 26 Mei 1995. Kampuni ya IPTL ndiyo kampuni ya kwanza ya nje kuingiza mitambo ya kuzalisha umeme wa dharula nchini. Mitambo yake inatumia mafuta mazito (Industrial Diezel Oil – IDO); jambo ambalo linasababisha umeme inaozalisha kuwa ghali kuliko ule wa kuzalisha kwa kutumia gesi na, au maji.

Taarifa kutoka ndani ya TANESCO zinasema, mbali na malipo kwa Mkono, kampuni ya IPTL hukomba kiasi cha Sh. 1.8 bilioni kila mwezi zikiwa malipo kwa gharama za kuweka mitambo yake nchini –Capacity Charge. Mtoa taarifa kutoka ndani ya serikali anasema, kwa kuwa TANESCO inakabiliwa na ukata mkubwa wa fedha kutokana na mikataba ya kinyonyaji ya umeme, serikali hutoa kila mwezi, kiasi cha Sh. 3.8 bilioni kuwezesha shirika hilo kununua mafuta ya kuendesha mitambo ya dharula.

Source; .: HABARI KUBWA- NIMROD MKONO ALIUA TAIFA,ALIMALIZA SHIRIKA LA TANESCO KAMA LA KWAKE,SOMA HAPA KUJUA
 
MsemajiUkweli jaribu kufikiria au kudadavua ni kesi ipi ambayo serikali imewahi kushinda dhidi ya makampuni ukiacha ile ya City water ndo utambue aina ya wanasheria tulio nao, waeza kuta kutokata rufaa ndo nafuu kwa serikali ili IPTL alazimishwe tu kukazia walichokubaliana mwanzo lkn hawajui
Tatizo ni kwamba wamiliki wa kampani hizo za kufua umeme ndo wanao takiwa kukata rufaa, always watachagua upande wa manufaa kwa kampani wanazo miliki kupitia watu wengine.
 
KAMPUNI ya mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono (Pichani) inadaiwa kulipwa na TANESCO, takriban shilingi 18 bilioni kwa huduma ya ushauri, chanzo Changu kimegundua. Nyaraka ambazo Chanzo hicho kimeona zinaonyesha kuwa tayari kampuni ya Mkono imetumia kiasi hicho kutoka shirika la umeme linalolegalega kifedha.
Mkono na kampuni yake ya Mkono & Co. Advocates ya jijini Dar es Salaam, amekuwa mshauri wa kisheria na wakili wa TANESCO tangu Mei 1995.
Shark
Thanks kwa kuleta hii article.
 
Na hiyo rufaa si kuwa haina gharama...unalipa gharama za advocate...na ukishindwa unalipa gharama za kuendesha kesi...
Mimi jana (au juzi) nimemsikiliza mwanasheria wa IPTL wala sikuambulia chochote ...haeleweki...na ukimsoma machoni...mmmnnnnhhhh ...yani ni nguvu ya hoja...ni kama katumwa kutuchanganya badala ya kutuelewesha...alikuwa anaongea kwenye taharifa ya Azam...amekazana TANESCO inabidi iendelee kuilipa IPTL...nadhani wako concerned zaidi na zile daily capacity charges wanazopokea (zisije katwa) kuliko maamuzi ya hii kesi...
Hukumu iliyotolewa wiki iliyopita ambapo World Bank tribunal (international centre for settlement of investment disputes-ICSID imeamuru TANESCO kuilipa Standard Chartered Bank Hong Kong (SCB-HK) kiasi cha dola za kimarekani milioni 148.40 pamoja na tozo riba kwa sasa imeanza kuleta utata kwa wapita njia kama mimi baada ya Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania (IPTL) kupinga maamuzi yaliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Kibiashara (ICSID) huku ikisema kama TANESCO watalipa, wao hawatayatambua malipo ya TANESCO kwa Standard Chartered Bank Hong Kong (SCB HK).

Hii ina maana kuwa IPTL hawaitambui Standard Chartered Bank Hong Kong (SCB-HK) na kwa maana hiyo hata kinga (indemnity) waliyotoa tarehe 27 Oktoba, 2013 kwa serikali ya Tanzania inayosema kama kutajitokeza madai yo yote yale, IPTL yenyewe itawajibika haiwezi kutumika katika malipo kwa Standard Chartered Bank Hong Kong (SCB-HK).

Pamoja na kelele nyingi za kukata rufaa lakini mwisho wake kuna kushinda au kushindwa.

Swali linakuja, Kama TANESCO atashindwa, nani atakayebeba hii adhabu na kulipa pesa?

Je, Serikali ya Tanzania itaipeleka IPTL mahakamani ili kuishinikiza ilipe hizo pesa kwa SCB-HK kulingana na hukumu ilivyotolewa na ICSID kwa sababu IPTL iliweka kinga inayosema kama kutajitokeza madai yo yote yale, IPTL yenyewe itawajibika.

Kama TANESCO itakata rufaa, nani atabeba gharama za kesi ya rufaa kwenye ICSID hasa ikichukuliwa kuwa mashitaka katika ICSID ni kati ya TANESCO na Standard Chartered Bank Hong Kong (SCB-HK) wakati mnufaikaji ni IPTL au SCB-HK kwa mujibu wa kinga (indemnity) iliyotolewa na IPTL kwa serikali ya Tanzania.

Tanzania itapata faida gani kwa TANESCO kukata rufaa ICSID wakati wanufaika ni IPTL au SCB-HK?

As a nation, we’re still bang in trouble!
 
MsemajiUkweli jaribu kufikiria au kudadavua ni kesi ipi ambayo serikali imewahi kushinda dhidi ya makampuni ukiacha ile ya City water ndo utambue aina ya wanasheria tulio nao, waeza kuta kutokata rufaa ndo nafuu kwa serikali ili IPTL alazimishwe tu kukazia walichokubaliana mwanzo lkn hawajui
City water yenyewe hatukushinda...wanaharakati wa nchini na wa nje ya nchi walianza kutumia 'name and shame' mpaka City water wakanyanyua mikono juu...walikuwa wanatinga mahakamani kuizomea City water jinsi inavyowanyonya masikini kutumia huduma muhimu ya maji...hatukushinda wala nini....

Kwa makampuni makubwa reputation ni kila kitu...kumbuka kesi ya Shell-Brent Spar na Greenpeace...Shell walikubali kushindwa japo Greenpeace walisema uongo ...kwa kuwa waliona sasa loss wanayopata ni kubwa kuliko kubadili uamuzi wa wapi kutupa Brent Spar...watu walianza kugomea kununua mafuta ya Shell
 
Mkuu Shark ninaamini tatizo sio wanasheria bali tatizo ni wale wanaopanga safu ya wanasheria.

Viongozi wetu hawana uzalendo na kwa maana hiyo, hata mawakili wanaowaweka wanakuwa ni wapiga dili tu. Refer Mkono & Co Advocates kwenye suala la TANESCO.
1+3=3+1=1+2+1 (most of the times)
Ni yale yale tu.
 
Ningekuwa mimi ndio serikari ya Tanzania ningezuia TANESCO kufanya appeal kwanza ukizingatia over 60% ya budget yao chanzo chake ni top up ya donors na government subsidy huko ni kuchezea hela za walipa kodi.

Hili swala linazunguka kama mduara tu, TANESCO hajui amlipe nani, mahakama ya Tanzania inasema PAP wazungu wanasema SCB-HK, na hao kila mtu anafungua kesi za TANESCO ambazo mawakili wanafaidika. Ifike wakati serikari isitishe malipo yoyote mpaka PAP na wazungu wamalizane kisheria kabla ya kuanza kuongea na TANESCO.
 
Watanzania tupinge huu mchezo tunaochezewa.
Ndugu yangu, tutaupingaje mchezo huu wakati ni mchezo unaosimamiwa na serikali yetu? Si tutaonekana hatuna imani, nidhamu wala uzalendo kwa kiongozi wetu bora? Si itatafsiriwa kama tunafanya uchochezi?
 
MsemajiUkweli pia na ile kesi ya Valambhia nadha kamchezo kalikuwa ni hako hako!! Wao mawakili wanalipwa huku kila hatua wanayoshindwa kiasi cha pesa anacholipwa anayetudai kinaongezeka!!
 
Dawa hapo ni kusitisha malipo ya IPTL (capacity charges sijui nini) na kumwambia yeye ndio akapinge hayo mahamuzi...asitutwishe mzigo usio kuwa wetu...
Tufungue Escrow nyingine (mmmnnnhhh) tuweke ela ambazo tulitakiwa tumlipe IPTL...akishinda tutampa ela yake...akishindwa tunampa Standard Chartered...simple...
 
Hapo ndio unakuja umuhimu wa kuwa na mahusiano mazuri na watu wa haki za binadamu...wangetusaidia kutumia strategy nyingine nje ya mahakama...wangejenga case ya jinsi gani hawa mabepari wanatunyonya wananchi masikini kutumia ujanjua ujanja....wangeona kama hao Standard Chartered hawajaomba poh...maana taregt ingekuwa wateja wa bank...kama wako tayari kutumia benki isiyofata principles za SRI
 
Dawa hapo ni kusitisha malipo ya IPTL (capacity charges sijui nini) na kumwambia yeye ndio akapinge hayo mahamuzi...asitutwishe mzigo usio kuwa wetu...
Tufungue Escrow nyingine (mmmnnnhhh) tuweke ela ambazo tulitakiwa tumlipe IPTL...akishinda tutampa ela yake...akishindwa tunampa Standard Chartered...simple...
Hizo gharama za kuendesha mitambo zitatoka kwa nani?

Tukubali tu Watanzania wenzetu wametuingiza kwenye huu mtanziko. Kumbuka IPTL ndiyo ufisadi mkubwa wa kwanza Tanzania ikifuatiwa na Songas. Hatutoki kirahisi
 
Tanzania itapata faida gani kwa TANESCO kukata rufaa ICSID wakati wanufaika ni IPTL au SCB-HK?

As a nation, we’re still bang in trouble!

Mkuu hii nchi kulikuwa na mtandao wa vibaka wa kimataifa.Hiki kitu kinaonyesha wazi kilipangwa na vibaka wa kimataifa wa ndani wakishirikiana na vibaka wa kimataifa wa nje .Vibaka hao wamo walioko serikalini,kwenye mahakama,bunge na mawakili na sekta binafsi.

TANESCO si mteja wa hiyo benki ya SHB-HK na wala haijawahi fanya biashara naye.Lakini kwa nini hiyo benki iliamua kuishtaki TANESCO badala ya mmiliki mpya wa mitambo hiyo PAP? Sababu kama swala ni kuwa hiyo mitambo iliwekwa dhamana kwa ajili ya mkopo waliochukua kwa nini wamfuate TANESCO ambaye sio mteja wao? Wao walitakiwa wamfuate mmiliki wa hiyo mitambo wamwonyeshe hayo makaratasi yao ya dhamana kuwa huu mtambo wa kwetu kama wana chochote cha kuongea waongee na huyo aliyechukua huo mtambo na angewaambia mimi ndiye mmiliki mpya wa huu mtambo hivyo na madeni yanayohusiana na huu mtambo ulio wekwa dhamana ni yangu.

Je hili swala wanasheria wa TANESCO na serikali hawakuliona? Kwa nini hawakuwaambia hao SCB -HK waende kwa mmiliki wa huo mtambo ambaye yupo.

Hapo kuna mchezo mchafu unachezwa.
 
Kiukweli uamuzi huu ni uonevu kwa Tanesco yetu.
IPTL ndio kupitia mbia wake kampuni ya Mechima ndio waliokopa kutoka benki mbili za nchini Malaysia, benki ya Sima na Bumiputra kisha serikali ya Malaysia ikilihamishia deni hilo kwa kampuni hodhi ya Danahatra ya Malaysia ambayo ndiyo iliyoliuza deni hilo Stan Chart HK.

Wakati deni hilo limeuzwa, huku nyuma Mechima wakauza hisa zake za IPTL kwa PAP kwa kuuza assets tuu na sio liabilities! . Hivyo SCBHK alinunua deni hewa toka Danaharta! .

Baada ya PAP kuinunua 70% ya Mechima ndani ya IPTL akamalizia kwa kuinunua 30% ya VIP toka kwa James Rugemalira hivyo kumi likijirudia 100% ya assets za IPTL bila madeni! na ndio maana akapewa fedha za escrow!.

Mdeni halisi wa SCBHK ni Danaharta na sio Tanesco.
Pasco
 
.Hiyo benki Stan chart HK imeona ije kufisadi Tanzania kwani inaona ndiko kuna mafisadi rahisi kuwarubuni kuliko kufisadi kule malyasia ambako ndiko mnunuzi wa hilo deni yuko.Hata kama dhamana ilikuwa hiyo mitambo walitakiwa wakamate hiyo mitambo sio kuishupalia Tanesco!! Tanesco ni mteja tu.unamkomaliaje mteja ambaye sio wako eti akulipe!!!
 
JokaKuu ushauri wako ni mzuri lakini nina wasiwasi kama unawezekana katika mazingira yaliopo kwa sasa hasa ikichukuliwa kuwa IPTL wanadai hawaitambui SCB-HK wakati SCB-HK wanajifanya hawatambui mkataba wa TANESCO na IPTL.

..fuatilia vizuri suala hili.

..tulikosea kuzitoa zile fedha za escrow.

..fedha zile kwa mtizamo wangu zilikuwa mahususi kutulinda ikiwa madai ya aina hii yangejitokeza.

..sasa kwa werevu wetu itabidi tuwalipe scb-hk kwa fedha za kodi ya wananchi.
 
Hukumu iliyotolewa wiki iliyopita ambapo World Bank tribunal (international centre for settlement of investment disputes-ICSID imeamuru TANESCO kuilipa Standard Chartered Bank Hong Kong (SCB-HK) kiasi cha dola za kimarekani milioni 148.40 pamoja na tozo riba kwa sasa imeanza kuleta utata kwa wapita njia kama mimi baada ya Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania (IPTL) kupinga maamuzi yaliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Kibiashara (ICSID) huku ikisema kama TANESCO watalipa, wao hawatayatambua malipo ya TANESCO kwa Standard Chartered Bank Hong Kong (SCB HK).

Hii ina maana kuwa IPTL hawaitambui Standard Chartered Bank Hong Kong (SCB-HK) na kwa maana hiyo hata kinga (indemnity) waliyotoa tarehe 27 Oktoba, 2013 kwa serikali ya Tanzania inayosema kama kutajitokeza madai yo yote yale, IPTL yenyewe itawajibika haiwezi kutumika katika malipo kwa Standard Chartered Bank Hong Kong (SCB-HK).

Pamoja na kelele nyingi za kukata rufaa lakini mwisho wake kuna kushinda au kushindwa.

Swali linakuja, Kama TANESCO atashindwa, nani atakayebeba hii adhabu na kulipa pesa?

Je, Serikali ya Tanzania itaipeleka IPTL mahakamani ili kuishinikiza ilipe hizo pesa kwa SCB-HK kulingana na hukumu ilivyotolewa na ICSID kwa sababu IPTL iliweka kinga inayosema kama kutajitokeza madai yo yote yale, IPTL yenyewe itawajibika.

Kama TANESCO itakata rufaa, nani atabeba gharama za kesi ya rufaa kwenye ICSID hasa ikichukuliwa kuwa mashitaka katika ICSID ni kati ya TANESCO na Standard Chartered Bank Hong Kong (SCB-HK) wakati mnufaikaji ni IPTL au SCB-HK kwa mujibu wa kinga (indemnity) iliyotolewa na IPTL kwa serikali ya Tanzania.

Tanzania itapata faida gani kwa TANESCO kukata rufaa ICSID wakati wanufaika ni IPTL au SCB-HK?

As a nation, we’re still bang in trouble!
Mlisha tuaminisha kuwa zile siyo fedha za serikali sasa unahangaika kitu gani?
 
Back
Top Bottom