MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,185
- 24,055
Hukumu iliyotolewa wiki iliyopita ambapo World Bank tribunal (international centre for settlement of investment disputes-ICSID imeamuru TANESCO kuilipa Standard Chartered Bank Hong Kong (SCB-HK) kiasi cha dola za kimarekani milioni 148.40 pamoja na tozo riba kwa sasa imeanza kuleta utata kwa wapita njia kama mimi baada ya Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania (IPTL) kupinga maamuzi yaliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Kibiashara (ICSID) huku ikisema kama TANESCO watalipa, wao hawatayatambua malipo ya TANESCO kwa Standard Chartered Bank Hong Kong (SCB HK).
Hii ina maana kuwa IPTL hawaitambui Standard Chartered Bank Hong Kong (SCB-HK) na kwa maana hiyo hata kinga (indemnity) waliyotoa tarehe 27 Oktoba, 2013 kwa serikali ya Tanzania inayosema kama kutajitokeza madai yo yote yale, IPTL yenyewe itawajibika haiwezi kutumika katika malipo kwa Standard Chartered Bank Hong Kong (SCB-HK).
Pamoja na kelele nyingi za kukata rufaa lakini mwisho wake kuna kushinda au kushindwa.
Swali linakuja, Kama TANESCO atashindwa, nani atakayebeba hii adhabu na kulipa pesa?
Je, Serikali ya Tanzania itaipeleka IPTL mahakamani ili kuishinikiza ilipe hizo pesa kwa SCB-HK kulingana na hukumu ilivyotolewa na ICSID kwa sababu IPTL iliweka kinga inayosema kama kutajitokeza madai yo yote yale, IPTL yenyewe itawajibika.
Kama TANESCO itakata rufaa, nani atabeba gharama za kesi ya rufaa kwenye ICSID hasa ikichukuliwa kuwa mashitaka katika ICSID ni kati ya TANESCO na Standard Chartered Bank Hong Kong (SCB-HK) wakati mnufaikaji ni IPTL au SCB-HK kwa mujibu wa kinga (indemnity) iliyotolewa na IPTL kwa serikali ya Tanzania.
Tanzania itapata faida gani kwa TANESCO kukata rufaa ICSID wakati wanufaika ni IPTL au SCB-HK?
As a nation, we’re still bang in trouble!