So, I believe kama tutangeneza ideology haiwezi kuwa ideology without specificities.. it is has to be an ideology that is sensible, reasonable and more than that it has to be an ideology that is believable and leads to clear achievements. Haiwezi kuwa itikadi ya vitabuni.
Tunarudi kwenye wakulima na wafanyakazi - Wakulima na wafanyakazi - Hawa wanapaswa kukumbushwa kwamba nguvu kazi yao inaweza kuwakomboa katika maisha duni. Pia wanapaswa kukumbuka ni muunganiko wa wakulima na wafanyakazi ndio uliowezesha kuutoa utawala wa kikoloni!
Nivyema kuwakumbusha nia ya Uhuru, maadai ya uhuru na kwanini hayajatimia mpaka sasa, lakini dawa ya umasikini ipo jikoni iwapo wakulima na wafanyakazi watasema "sasa imetosha".
Kuwapata wakulima na wafanyakazi, uchambuzi wa kina juu ya masoko ya wakulima ya ndani na nje lazima ufanyike na maswala ya ruzuku yaangaliwe. Kwa wafanyakazi ni bayana kuangalia maswala ya mishahara - si kwa kusema nyongeza itakuwa shilingi ngapi, ila kuangalia mgawanyo na matumizi ya pesa za serikali, na kukosoa sehemu ambazo matumizi hayako sahihi, na hizo pesa zikitumiwa sahihi basi ni lazima mishahara itaongezeka. Mfumo wa huduma za jamii - hasa afya ni tatizo kubwa sana kwa wakulima na wafanyakazi wa chini! kuwa na mpango wa kutatua tatizo hilo wananchi wanaweza kukusikiliza kwa kina.
Pili kunaswala zima la wapiga kura wapya, hawa ndio watakaoleta mabadiliko katika uchaguzi ujao. Hili kundi linahitaji sababu ya kupiga kura. Sijui idadi yao ni wangapi, lakini naamini ni wengi sana - mimi nawaita watu wa kati. Nitabaka lililokanganyika kabisa - kiuchumi, kisiasa, kiitikadi, kimaadili na mapokeo, lakini linashabihiana katika swala moja tu kuchoshwa na uongozi na jinsi inavyoendeshwa. Kama sio wamechoshwa na uongozi, basi wanachukia foleni za barabarani, ame jinsi internet hazifanyi kazi, uduni wa huduma mbalimbali, kutokupandishwa vyeo, wengi wanawivu wa maendeleo - yawe yale ya taifa au ya ubinafsi. Vichwani mwao wanapicha fulani ya tanzania, yawezekana ni ya ndoto, ama ni ya matamania.
Watu hawa wanaona serikali inaendeshwa kihunihuni, haithamini wala kujali uwezo wa taaluma mbalimbali - agenda yeyote ya kuendesha nchi hii kwa ethics na taaluma ni jambo la msingi sana kwao. Iwapo wataonyeshwa uongozi wetu umeshidwa kutoa muongozo wa maendeleo, na ukatoa mfumo mpya utakaojali ufanisi, mahusiano juu ya elimu na mafanikio, basi ujue utapata wapigaji kura wengi.
Hapa kuna makundi mawili ya wapiga kura, kunawale wanaotaka kujua watafanyiwa nini, na wale wanaotamani kuona nchi hii inaweza kubadilika.