Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Ni mgongano wa kihistoria ambao ulipaswa kutokea. Ni mgongano ambao hutokea mahali popote panapokuwa na tofauti kubwa kati ya watawala na watawaliwa. Ndivyo ilivyokuwa kwenye Mapinduzi ya Ufaransa, Mapinduzi ya Marekani na Mapinduzi ya Bolshevik (Urusi).
Ni yale yale yaliyotokea na kusababisha mapinduzi ya Cuba yaliyomuingiza Castro madarakani. Ndiyo! Ni yale yale yaliyotokea pia kwenye mapinduzi ya Zanzibar!
Migongano ya namna hiyo asili yake mara zote ni pale wananchi wanapotambua kuwa hawana usawa na watawala wao na ya kuwa tofauti ya maisha yao na yale ya watawala ni kubwa mno na ya kwamba mwananchi wa kawaida anajikuta hana nafasi yoyote aidha ya kufanikiwa au ya kuweza kuishi maisha yenye utu, usawa, haki na heshima.
Nchi chache zimeweza kupitia mgongano huo kwa njia ya nguvu (kama mifano niliyotoa) au kama ilivyotokea huko Ukraine na Georgia miaka ya karibuni kwa njia ya nguvu ya umma.
Tanzania yetu inapitia mgongano huo katika hatua zake za awali. Silaha ambayo wananchi wanatumia leo hii ni nguvu yao ya hoja na wanatarajiwa kubadilisha serikali yao kwa nguvu ya kura.
Hata hivyo hilo halitakuwa rahisi kwani dalili yote inaonesha kuwa watawala hawako laini kuruhusu mabadiliko makubwa ya kiutawala yenye kupendelea wananchi wa kawaida. Hivyo, mgongano unaendelea. Swali ni nani ashinde? Na ni nani ataamua mshindi!?
Nisikilize:
[mp3]http://mwanakijiji.podomatic.com/enclosure/2009-04-29T23_41_36-07_00.mp3[/mp3]
http://www.box.net/shared/nfq7nv9lit