Sioni umuhimu wa daraja la Aga Khan - Coco beach kwa sasa - JamiiForumsNdo umeandika nini ndugu? Kama huoni umuhimu wa hilo daraja basi utakuwa ni taahira
Mimi pia taahira, lakini mwenye subira maana ya Mungu mengi.Ndo umeandika nini ndugu? Kama huoni umuhimu wa hilo daraja basi utakuwa ni taahira
Daraja hili halina umuhimu wowote, gharama zake bora wangevunja police surrender na kupanunua lililopo kwani ndio kikwazo. Magari yatokayo oceans yakiungana na mhimbili tayari foleni. Bora wangejenga interchange mchezo ungeishaNadhani umekurupuka, kwanza hilo daraja ni juhudi za Mh JK..Kipenzi cha watanzania, aliondoka akiwa tayari ameshaweka misingi na makubaliano kama lilivyo daraja la Mfugale...
Pili Unasema daraja liko liko chini au unaliita kidaraja.. nIkwambie tu kwamba yale ni matayarisho ya ujenzi tu na lile daraja unaloliona likiwekwa lile sio daraja halisi, ni njia tu ya wakandarasi kupitisha materials na nyenzo vilevile litatumika kama support wakati wa ujenzi wa daraja halisi
Tatu.. Unaijua foleni ya kutoka na kuingia mjini wakati wa asubuhi na jioni hapo selander na stanbic? Daraja hili ni muhimu sana kama tunataka kupunguza foleni ali Hassan mwinyi road.
Nne; Jiji la Dar es salaam litaendelea kukua kwa kasi licha ya Serikali kuhamia Dodoma hivyo daraja hili bado ni muhimu sana
Hata ziliponunuliwa ndege mlisema hazina maana. leo hii ndio mnazitumia. tulipojenga barabara za mwendokasi mlibeza. leo hii mnafurahia. tunafanya maendeleo kwa wapenda maendeleo na si ninyi msio na mwelekeoMimi pia taahira, lakini mwenye subira maana ya Mungu mengi.
Kilipotangazwa kikokotoo cha 25% napo nilikuwa taahira, lakini kama nilivyosema, Ya Mungu Mengi...juu ya kikokotoo mimi si taahira tena.
Hii awamu imejaa matumaini yenye kuthibitika kabla ya jua kupambazuka, maana hata Ubungo pambazuko limeonekana. Mkandarasi kaweka round about ili atujengee flyover...mashallah! Foleni imeondoka na round hata kabla flyover haijaonesha dalili.
Waarabu wanasema: Inna allahu maaswabirinah...acha leo niwe taahira
Hapo sawa, nilidhani unataka kusema zimeingiza faida.Hata ziliponunuliwa ndege mlisema hazina maana. leo hii ndio mnazitumia. tulipojenga barabara za mwendokasi mlibeza. leo hii mnafurahia. tunafanya maendeleo kwa wapenda maendeleo na si ninyi msio na mwelekeo
Watu wengine mnapaswa kuhurumiwa tu-Watu kuzitumia hizo ndege au mwendokasi haimanishi maamuzi za kuzinunua hayakuwa ya Kipuuzi? Kwangu mimi Ujenzi wa aina ile wa Mwendo kasi ilikuwa ni Upuuzi. Hivi Ukiacha Joberg-SA tena maeneo machache-Kuna nchi nyingine Duniani imejenga barabara kama kwetu?Hata ziliponunuliwa ndege mlisema hazina maana. leo hii ndio mnazitumia. tulipojenga barabara za mwendokasi mlibeza. leo hii mnafurahia. tunafanya maendeleo kwa wapenda maendeleo na si ninyi msio na mwelekeo
Katika miradi ya kipumbavu iliyowahi kufanyika hapa nchini ni daraaja ya Cocbeach.Ukipita barabara ya Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es Salaam baada ya mataa ya barabara inayoelekea Masaki pembeni ya bahari ya Hindi utakuta kuna kadaraja fulani hivi kanaunganisha kona moja na nyingine ambako kako mita chache sana kutoka barabara hiyo na kapo kando kidogo mwa bahari ya Hindi. Hili ndilo daraja la coco beach ambalo limenyanyuka mita chache sana kutoka usawa wa bahari.
Ukiangalia kwa umakini daraja hili basi unajikuta ukijiuliza maswali mengi sana na kama una hasira basi utaishia kutoa lugha za kuudhi kimawazo na hata kwa mdomo.
Unajiuliza ni nini hasa umuhimu wa daraja hili? Unakosa jibu! Unajiuliza ni nani hasa anagharamia? Unaishia kuomba Mungu zisiwe kodi zetu!
Daraja limejengwa pembeni kidogo mwa barabara ya Ali Hassan Mwinyi na hivi karibuni Rais Magufuli na ikulu yake watahamia Dodoma, balozi za Umoja wa Ulaya Canada, China na nyingine zote ambazo labda wao ndiyo hasa walengwa wa daraja hili hawatakuwepo tena.
Unajiuliza kama daraja litatumika kama kivutio cha utalii unarudi unaangalia jinsi ujenzi wake ulivyo, lilivyonyanyuliwa kutoka usawa wa bahari, umbali kutoka daraja hilo na nchi kavu ulivyokaribiana unajikuta ukikasirika tena.
Any way naona sasa tumekuwa "Dona Kantre" kiasi kwamba tunaweza kutumia fedha jinsi tunavyotaka maana zipo nyingi.