SoC03 Nani anawajibika kulipa walimu mshahara kati ya wazazi au serikali?

Stories of Change - 2023 Competition

mackj

Member
Jul 25, 2023
5
1
Naanza kwa kuwashukuru waandaaji wa jukwaa hili la stories of change, kutoka jamii forum, kwa kuendelea kuwaleta wananchi karibu na serikali ili kujibu hoja zinazoibuka huku nami nikihoji nani anawajibika katika kuwalipa mshahara walimu katika shule zetu za kata hapa nchini tanzania kati ya wazazi au serikali?

Serikali ya jamuhuri ya muungano wa tanzania katika serikali ya awamu ya nne iliyokuwa ikiongozwa na dr jakaya mrisho kikwete kupitia kwa waziri mkuu wake edward ngoyayi lowasa ilianzisha shule za kata ambapo kila halmashauri zilielekezwa kupitia sera ya elimu kuanzisha shule za sekondari kila kata, ambapo zoezi hilo lilishirikisha wananchi kwa kushiriki kupitia rasili mali na nguvu kazi katika kutekeleza adhima hiyo.

Ambapo mpango huu ulifanikiwa kwa asilimia mia moja mpaka hii leo karibu tanzania nzima shule za kata zumejengwa jambo lililochochea kiwango cha ufaulu kwa wananfunzi wanaomaliza darasa la saba hapa nchini ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo uhaba wa shule za sekondari ulikuwa kikwazo kikubwa katika eneo la ufaulu wa wanafunzi waliokuwa wanahitimu darasa la saba, hongera sana rais jakaya kikwete kwa mpango huu mzuri na serikali ya awamu ya nne kwa ujumla.

Mnamo mwaka 2015 serikali ya awamu ya tano chini utawala wa dr john joseph pombe magufuli ulinzisha mfumo wa elimu bila malipo mfumo amabao umekuwa ni kichocheo kikubwa cha wazazi kupeleka watoto shule na hivyo kuongozeka kwa hitaji la mahitaji ya miundombinu ya kitaaluma na ufundishaji jambo ambalo limeonekana kuwa mzigo kwa serikali ambapo hivi karibuni serikali ya awamu ya sita nayo imetilia mkazo uwepo wa uhakika wa watoto kusalia mashuleni huku walimu wakiwa ni kikwazo kinachopelekea watoto wengi pamoja na miundo mbinu ya kumfanya mtoto kujifunza vizuri nayo kuwa changamoto lakini kuna kila sababu ya kuipongeza sana serikali katika eneo hili.

Katika hatu hiyo, hivi karibuni serikali imetangaza viashiria vya ufanisi yani KPI's (key performance indicators) kuwa ni pamoja na uwepo wa chakula mashuleni jambo ambalo limekuwa ni jukumu la mzazi na siyo jukumu la serikali huku walimu nao wakilazimika kuwarudisha watoto nyumbani kwa kukoswa chakula hicho ambapo katika shule za manispaa ya musom ambako makala haya yamejikita, katika jukwaa hili,nikuwa shule zote, za kutwa za uma wanatakiwa kutoa mchele kilo 4 maharage kilo 3 na pesa ya mafuta sh 3000.

ikiwa nchi ilalalamikia mfumuko wa bei za vyakula ambapo mchele unakadiriwa 3000 kilo moja na maharage kitenge 3500 kwa wastani wa bei hiyo kila mzazi anatakiwa kutoa sh 22500 kwa mwezi ambapo kwa mwaka ni sawa 306,000 laki tatu na elfu sita.

Huku wananchi wakiwa bado wanakumbukumbu ya mfumo wa elimu bila malipo, lakini wanapewa agizo hilo na serikali yao ambayo hiyo hiyo, iliahidi katika ilani ya uchaguzi kuwa wanafunzi elimu ni bure kuanzia shule ya msingi mpaka kidato cha sita" kitu ambacho kinazua mgongano wa mawazo miongoni mwa wadau.

Ikiwa hilo bado ni mwiba kwa wazazi limeibuka suala la hela ya taaluma kama inavyoitwa na wenyewe wakuu wa mashule pale wanapoita vikao na wazazi kuzungumza juu ya maendeleo ya kitaaluma kwa watoto wao, lakini pesa hii inatakiwa kulipa mishahara ya walimu wanaojitolea kufundisha masomo ya sayansi kwakuwa hawana ajira.

Katika shule ya mwisenge pale manispaa ya musoma, darasa moja lina mikondo A mpaka F ambapo kila darasa moja lina wanafunzi kati 76 mpaka 84 kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne maana yake darasa moja lina wanafunzi 480 kidato cha kwanza inamaana kwa madara manne yaani kidato cha kwanza mpaka cha nne ni wastani wa wanafunzi 1920 huku agizo la michango ya hela hiyo ya kulipa walimu wa sayansi ni sh 20,000 kwa kila mzazi,ukizidisha mara 1920 unapata 38,400,000 milioni thelathini na nane na laki nne kwa mwaka ndiyo pesa inayokusanywa kupitia akaunti za shule ikiitwa pesa ya taaluma.

Ambapo isipotolewa pesa kwa kipindi cha mwezi mmoja katika muhula wa masomo walimu wakuu wanalazimika kuwachapa watoto viboko na kuwarudisha nyumbani inakadiriwa watoto 50 kati ya 125 hurudishwa nyumbani na kukosa masomo kwa wiki je?mzazi mwenzangu ndio maana katika makala hii nimehoji wajibu wa kulipa walimu mshahara ni wa nani kati ya serikali au wazazi nipeni jibu na tukiwa tunaendelea kutafakari tujiulize hivi huu ni msimamo wa serikali au ni utashi wa walimu na watendaji wa halimashauri? Na je? shule hizi za kutwa za uma tangu serikali ilipozipa mamlaka ya kuwa na akaunti zao na siyo kupitishia fedha za ruzuku na maendeleo katika akaunti za halmashauri zinakaguliwa na wakaguzi au hapana?

Ikiwa hiyo ndio pesa inayokusanywa kwa mwaka je? ni sawa na wastani wa shilingi ngapi katika mshahara wa kima cha chini cha mwalimu wa daraja la kawaida anayepaswa kufundisha masomo ya sayansi katika shule za O level? Mfano ikiwa shule moja ina walimu wanne wa kitado cha kwanza mpaka cha nne mshahara wao ni laki 8 kwa mwezi kwa walimu 4 kwa pesa hiyo inayotajwa kuchangwa na wazazi kwa mwaka je? Nikweli kuwa huo ndio mshahara wanaopata na kama jibu ni ndiyo kwanini mbona hawaajiriwi? Maana wa kulipa ameishaapatikana ambaye ni wazazi.

Na je? Ni wajibu wa mwananchi kulipa watumishi wanaofanya kazi za uma? ama kwa hakika kwa chemsha bongo hii mzazi. mwenzangu nidhahiri umebaini majibu nikuwa dhana ya utawala bora katika sekta ya elimu ya sekondari kwenye shule za kata za uma haipo na ni wizi wa mchana kweupe kwa gahara hizi shule hizi kiuhalisia nikuwa ni shule za kulipia na neno elimu bila malipo ni siasa ambayo kwa miaka mitano ijayo inaweza kuja kuwa tatizo kubwa linaloweza kuichonganisha jamii na serikali nilazima hatua zichukuliwe haraka hasa katika shule za pembezoni serikali iwatume wakaguzi ili kujiridhisha matumizi ya hizi fedha.

Maana katika shule ya mwisenge kuna mwalimu mmoja aitwaye peter bonface wambura, ambaye ndiye anafundisha masomo ya sayansi kwa shule nzima na kulipwa kwake ni shida mpaka ameanza kukata tamaa nimezungumza nae wakati wa ukusanyaji taarifa hizi na kuniambia kuwa akipata ajira pengine anaweza kuondoka "mimi leo hapa ni mwaka wa nne najitolea na watoto ukiwauliza wanakwambia wamelipa kama fomu one wote hakuna ambaye hajalipa watoto 400 lakini mkuu ananilipa leo 20000 kesho 40000 hivyo" alisema mwalimu peter.

Jitihada za kumpata mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya mwisenge ezbon kikula, ziligonga mwamba kwakuwa alikuwa msibani akadai hawezi kuongelea mambo ya kazi nje ya kituo ama kwa hakika ukiyafuatilia kwa kina masuala ya utawala bora katika sekta ya elimu kwa sasa ni njaa isiyojulikana shibe yake, wazazi tangu shule hizi zimeitwa zao kwakuwa hujengwa kwa nguvu zao wametwishwa mzigo wote na serikali lakini ukweli ni kwamba shule ni mali ya serikali namaliza kwa kutoa shukrani za dhati kwenu wanajukwaa kwa mada zenye tija kwaherini.
 
Back
Top Bottom