Nani anaua watu wetu?

Ishimba

Member
May 19, 2017
22
84
Tanzania ya Mwalimu Julius Nyerere sasa inabadilika kwa kasi ya ajabu; unatoka kuwa nchi ya amani na sasa inagubikwa na matukio ya mauaji ya raia kila uchao.

Kibaya zaidi wanaouawa siyo vibaka. Ni viongozi wa vyama vya siasa, hasa kutoka vyama vya upinzani.

Pia wanaouawa, kutekwa na kupoteza au kuuawa ni waandishi wa habari. Inasikitisha sana.

Inashangaza mno kuwa mauaji na mateso haya, hayana majibu kutoka vyombo vya usalama, hatua ambayo inatia shaka kuwa ukimya huo hauna siha njema kwa vyombo hivyo, kiasi cha kuonekana kinahusika na matukio haya.

Tujiulize, nani wanaua Watanzania wenzetu? Tunamsubiri Nani auawe ndiyo tushituke na kupaza sauti?

Naililia Tanzania yangu..
 
Ukisema nchi haiko salama unaitwa mchochezi, tokea lini nchi raia wake wanauwawa na kupotea ikawa salama?

Mbaya zaidi wenye jukumu la kulinda, kuzuia na kuwadhibiti wahalifu wanatuletea misamiati mipya ya watu wasiojulikana.
 
Tutakuja kujua tuu ipo siku, mwisho wa ubaya ni aibu, mara paaaa chakubanga naye limemfika.
 
Hata siku moja Dhulma haijawahi ishinda haki.., ipo siku yote yatadhihiri!!!
 
Kila nafsi itaonja mauti,unapojichukulia nafasi ya Mungu .kulazimishwa uitwe Mungu kaa ukijua Mwenyezi Mungu ni fundi,hakuna aijuaye kesho yake
 
Mauaji ya wapinzani kila kukicha.., Raisi kakaa kimya.., Wabunge wa ccm wanaendelea na shughuli kama kawaida.., hakuna mwenye mamlaka anayejali..!
Na hawa wote wameapa kuwatumikia watanzania .., wameapa kulinda maisha na Uhuru wa kujieleza wa watanzania wote bila ubaguzi wa dini wala vyama..

Cha ajabu, wana ccm wanaochochea chuki, ubaguzi, mauaji, wanaotumia pesa zetu kununua madiwani na wabunge ndio wanaopandishwa vyeo haraka...

Yote haya yanatendeka Tanzania ile ya Nyerere.., maraisi wetu wote wako kimyaaaa..., haya hayawahusu..!

Ni nani auawe.., au ni watu idadi gani wauawe ndio nyie wazee wa nchi hii mshtuke na kumkemea huyu mtu mwenye kiu ya damu ya watanzania...?!
 
Nani anaetuua hilo ndio swali...maana kwa mfumo huo ni hatari kwa kila mtu sio wanasiasa tuu...
 
Back
Top Bottom