Nani anataka Sethi wa IPTL afe gezerani?

Jakomhabari

Member
Joined
Jul 29, 2015
Posts
26
Reaction score
15
Wanajamvi, naomba kuleta kwenu mada hii ambayo ninafahamu kuwa itapata wachangiaji wenye mitazamo hasi na wengine wenye mitazamo chanya, ukizingatia mitazomo iliyojengeka miongoni mwa wanajamii kuhusu muhusika mkuu katika mada hii.
Mimi binafsi nimebaki kujiuliza maswali mengi kuhusu uwezo/heshima/ na nguvu za mahakama zetu. Je, amri zinazotoka mahakamani zinapaswa kuheshimiwa na kutekelezwa na nani? Nani anapaswa kudharau amri ya mahakama na asichukuliwe hatua? Je, Mahakama zetu zinauwezo wa kusimamia na kuona kwamba amri/hukumu/maamuzi yake yanaheshimiwa?
Nimejiuliza maswali haya baada ya kufuatilia kesi ya anayedaiwa kumiliki IPTL (Harbinder Singh Sethi) ambaye ameshtakiwa pamoja na aliyekuwa mwanahisa wa IPTL (James Rugemalira) kwa makosa mbali mbali ikiwemo utakatishaji fedha haramu na uhujumu uchumi.
Katika kesi hii (pasipo kuingilia mwenendo wa kesi ya msingi) kuna kipengele cha malalamiko ya mtuhumiwa wa kwanza (Sethi) ambaye amekuwa akilalamika mahakamani (Kisutu) kuwa anaumwa na akaiomba mahakama imsaidie ili apate matibabu/huduma ya kitaalam ya kitabibu.
Kwa maelezo yake mwenyewe mbele ya Hakimu Shaidi, Sethi alieleza mahakama matatizo yake na kuiomba mahakama imsaidie apate matibabu. Wakati anamalizia maelezo yake, alisema kuwa asingependa kufia gerezani bali angependa awe na afya njema ili aweze kujitetea dhidi ya kesi hiyo inayomkabili. Naomba ninukuu maelezo yake kama ilivyochapishwa kwenye nakala ya amri/maamuzi ya pili kutolewa mahakamani hapo:-
"1st Accused: I want to explain about my hearth. I have been in severe ulcers and last year I had operation at my intestine at South Africa the doctor inserted balloon at my intestine and I have to see a doctor.
Last time you ordered me to be taken to Muhimbili but I was taken to Amana, Amana Doctors surprised a lot and wanted me to be taken to Muhimbili, however they didn't. The balloon is with fluid and if not checked well increase the danger of my health. I don't want to die in remand custody, I want to be health to fight for my case and whatever." ...mwisho wa kunukuu.
(nimenukuu kama ilivyochapwa kwenye nakala niliyoambatanisha hapo chini -2nd Order)
Kwa maelezo yake mwenyewe, Sethi ameonyesha hofu ya afya yake kuendelea kuzorota endapo hatapata matibabu ya haraka na ya kitaalama kutoka kwa madaktari bingwa. Hii hali inaweza ikapelekea apoteze maisha kabla ya hata kesi yake haijafikia tamati.
Mimi binafsi naiona hofu ya Sethi ikiwa na mashiko, baada ya kuziona nakala za amri tatu (3 court orders) ambazo zinaelekeza upande wa mastaka (jamhuri) kuhakikisha kwamba Sethi anapata matibabu, hakimu akisisitiza kuwa swala la afya ni jambo ambalo silo la kulifanyia masihara. Akasema wataalam kutoka katika hosipitali ya tiaifa ya Muhimbili washirikishwe katika kuipatia ufumbuzi swala hili.
Utekelezaji wa Amri hii ya mahakama imeonekana kuwa ngumu sana. Hadi sasa, mahakama hiyo imetoa amri tatu ikiwa na maelekezo hayo hayo. Ikiwa inataja kuhusisha wataalam kutoka Muhimbili. Katika amri yake ya mwisho (third court order) Hakimu Shaidi alisisitiza kuwa hana nia ya kubatilisha amri yake ya awali.
Sasa kama mahakama imetoa amri na maelekezo kuhusu kutibiwa kwa mtuhumiwa, ni nani anazuia utekelezaji wa amri hii? Je, lengo lake ni nini? Je, yupo juu ya sheria kwa maana ya kwamba halazimiki kutii amri ya mahakama? Je, Sethi akifa huko rumande, tutapata kujua kilichojiri katika mchakato wote wa uchotwaji fedha zile katika akaunti ya Escrow? Nani ataibeba lawama endapo huyu mtuhumiwa atapoteza maisha kwa uzembe au kwa ukorofi wa kutotii amri ya mahakama?

Jamani, haya ni maswali ambayo yamekuwa yananisumbua.

Unaweza kupakua amri zote tatu ili kujionea.
 
Attachments

  • 1st ORDER.jpeg
    1st ORDER.jpeg
    61.9 KB · Views: 66
  • 2nd ORDER.pdf
    2nd ORDER.pdf
    562.4 KB · Views: 56
  • 3rd court order.pdf
    3rd court order.pdf
    251.3 KB · Views: 50
Huyo jamaa ni kiungo muhimu sana kwenye hiyo kesi, na yeye ndiyo mwenyewe kuweka kila kitu wazi... Ndiyo maana wanamfanyia yote haya ili kumdhoofisha...

Cc: mahondaw
 
U

Unaweza ukamdhoofisha mtu hadi ukampoteza kabisa. Baada ya hapo? Tuta recover hizo fedha kwa njia gani?
 
Ateme mzigo wote watamuachia tu!

Ova
 
Hio janja tu hivi mnaamini kweli huyo ni mgonjwa?? Janja yake tu hio ili akimbie kwanza huko China watu kama hawa ni shaba tu hamna mjadala wowote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanajamvi, naomba kuleta kwenu mada hii ambayo ninafahamu kuwa itapata wachangiaji wenye mitazamo hasi na wengine wenye mitazamo chanya, ukizingatia mitazomo iliyojengeka miongoni mwa wanajamii kuhusu muhusika mkuu katika mada hii.
Mimi binafsi nimebaki kujiuliza maswali mengi kuhusu uwezo/heshima/ na nguvu za mahakama zetu. Je, amri zinazotoka mahakamani zinapaswa kuheshimiwa na kutekelezwa na nani? Nani anapaswa kudharau amri ya mahakama na asichukuliwe hatua? Je, Mahakama zetu zinauwezo wa kusimamia na kuona kwamba amri/hukumu/maamuzi yake yanaheshimiwa?
Nimejiuliza maswali haya baada ya kufuatilia kesi ya anayedaiwa kumiliki IPTL (Harbinder Singh Sethi) ambaye ameshtakiwa pamoja na aliyekuwa mwanahisa wa IPTL (James Rugemalira) kwa makosa mbali mbali ikiwemo utakatishaji fedha haramu na uhujumu uchumi.
Katika kesi hii (pasipo kuingilia mwenendo wa kesi ya msingi) kuna kipengele cha malalamiko ya mtuhumiwa wa kwanza (Sethi) ambaye amekuwa akilalamika mahakamani (Kisutu) kuwa anaumwa na akaiomba mahakama imsaidie ili apate matibabu/huduma ya kitaalam ya kitabibu.
Kwa maelezo yake mwenyewe mbele ya Hakimu Shaidi, Sethi alieleza mahakama matatizo yake na kuiomba mahakama imsaidie apate matibabu. Wakati anamalizia maelezo yake, alisema kuwa asingependa kufia gerezani bali angependa awe na afya njema ili aweze kujitetea dhidi ya kesi hiyo inayomkabili. Naomba ninukuu maelezo yake kama ilivyochapishwa kwenye nakala ya amri/maamuzi ya pili kutolewa mahakamani hapo:-
"1st Accused: I want to explain about my hearth. I have been in severe ulcers and last year I had operation at my intestine at South Africa the doctor inserted balloon at my intestine and I have to see a doctor.
Last time you ordered me to be taken to Muhimbili but I was taken to Amana, Amana Doctors surprised a lot and wanted me to be taken to Muhimbili, however they didn't. The balloon is with fluid and if not checked well increase the danger of my health. I don't want to die in remand custody, I want to be health to fight for my case and whatever." ...mwisho wa kunukuu.
(nimenukuu kama ilivyochapwa kwenye nakala niliyoambatanisha hapo chini -2nd Order)
Kwa maelezo yake mwenyewe, Sethi ameonyesha hofu ya afya yake kuendelea kuzorota endapo hatapata matibabu ya haraka na ya kitaalama kutoka kwa madaktari bingwa. Hii hali inaweza ikapelekea apoteze maisha kabla ya hata kesi yake haijafikia tamati.
Mimi binafsi naiona hofu ya Sethi ikiwa na mashiko, baada ya kuziona nakala za amri tatu (3 court orders) ambazo zinaelekeza upande wa mastaka (jamhuri) kuhakikisha kwamba Sethi anapata matibabu, hakimu akisisitiza kuwa swala la afya ni jambo ambalo silo la kulifanyia masihara. Akasema wataalam kutoka katika hosipitali ya tiaifa ya Muhimbili washirikishwe katika kuipatia ufumbuzi swala hili.
Utekelezaji wa Amri hii ya mahakama imeonekana kuwa ngumu sana. Hadi sasa, mahakama hiyo imetoa amri tatu ikiwa na maelekezo hayo hayo. Ikiwa inataja kuhusisha wataalam kutoka Muhimbili. Katika amri yake ya mwisho (third court order) Hakimu Shaidi alisisitiza kuwa hana nia ya kubatilisha amri yake ya awali.
Sasa kama mahakama imetoa amri na maelekezo kuhusu kutibiwa kwa mtuhumiwa, ni nani anazuia utekelezaji wa amri hii? Je, lengo lake ni nini? Je, yupo juu ya sheria kwa maana ya kwamba halazimiki kutii amri ya mahakama? Je, Sethi akifa huko rumande, tutapata kujua kilichojiri katika mchakato wote wa uchotwaji fedha zile katika akaunti ya Escrow? Nani ataibeba lawama endapo huyu mtuhumiwa atapoteza maisha kwa uzembe au kwa ukorofi wa kutotii amri ya mahakama?

Jamani, haya ni maswali ambayo yamekuwa yananisumbua.

Unaweza kupakua amri zote tatu ili kujionea.
Hawa watu huwa wakifanya madudu yao sijui huwa wanakumbuka kwamba mwizi siku zake ni arobaini?Afadhali hata Ruge,Sethi ni mtu wa hovyo sana,ni tapeli la kimataifa hasa.

Ila pamoja na utapeli wake,nisingependa afe bila kukumbana na mkono wa sheria.Ningependa ahukumiwe adhabu stahiki, ili hatimaye ajutie matendo yake.He is a very evil man.
 
Kwa nini kesi haianzi ili tujue mbivu na mbichi, watu wanalundikwa rumande tu! Inanikumbusha MAUMAU huko kenya enzi za kupigania uhuru " detention without trial" wapelekwe mahakamani
 
Back
Top Bottom