Nani anastahili kumrithi Mizengo Pinda?

Nani anastahili kumrithi Mizengo Pinda?

Nafasi hii ibaki wazi, Rais kwa muda huu abebe jukumu hilo mpaka atakapo maliza muda wake. Lukuvi aendelee kuiwakirisha serikali bungeni (kama naye hakuguswa na kadhia hii). Tumechoka kulipa masulufu baadhi ya mawaziri wakuu wasitaafu walioiletea nchi majanga.

Minaona ni bora JK na serikaki yake yote wajiuzulu turudi kwenye uchaguzi.
 
prof. mwandosya, au kwa vile profesa JK anapenda vijana anaweza akawateua kati ya haya, Ridhiwani Kikwete, huyu nadhani asaiv nae ana PHD, Mwigulu Chemba, January makamba, au kama vipi profesa akiona hakuna anayefaa anaweza akajiteua mwenyewe.
 
Sasa awe mwnamke tuandike historia.......nampendekeza mama Rwakatale au yule mbunge wa NKENGE,,,Bi. Asumpta Mshama.........au nyie mnaonajeeeeeee.....!!!!!!!!!!!!!!!!

Wanawake sawa lakini sio wanawake kutoka CCM….Makinda kawaangusha wanawake, Tibaijuka nae skendo kibao, yule mama wa UN kafukuzwa kwa uzembe wake pamoja na uprofesa wake…Huko sisiemu hakuna kitu
 
Ukiangalia mwenendo mzima wa sakata la Tegeta Escrow account,utagundua kuwa, kuna uwezekano mkubwa wa waziri mkuu ambae nae amekuwa akituhumiwa kupata mgao,kuwa implicated katika kashifa hii na hivyo kutakiwa kuwajibika.

Kuna viashiria kadhaa kuwa PM anaweza kutakiwa kuwajibika kwa kujiuzulu.

Mosi,Pinda ametajwa sana kupata mgao katika hili sakata na sidhani kama itakuwa ni uzushi tu maana siku zote mambo huanza hivi hivi na mwisho wa siku inageuka kuwa kweli.

Pili,imekuwa ikisemwa kuwa kashifa hii huenda ikaiangusha serikali na mh.Zitto pekee alikwenda mbali zaidi kwa kusema sakata hili linaweza kuangusha "tembo mkubwa".

Sasa mh.Zitto anaposema kashifa hii inaweza kumuangusha tembo mkubwa,hapo alikuwa anamlenga nani zaidi ya waziri mkuu?

Mbali na viashiria hivyo,jambo lingine linalomuweka Pinda katika wakati mgumu wa ku-survive kashifa hii na pia ku-survive vote of no confidence endapo tutafika huko,ni hatua yake ya kujiingiza katika kinyang'anyiro cha uraisi ndani ya CCM.

Kwa mtazamo wangu,wapinzani wake watatumia mwanya huo kummaliza kwa kuhakikisha(ku-facilitate) upigwaji wa kura hiyo na ikipigwa aondoke.

Sasa kwa utangulizi huo,ni dhahiri PM anaweza kuondoka kwa style ile ile ya mtangulizi wake unless ripoti hiyo ya CAG iandaliwe kum-favor(ichakachuliwe).

Je,endapo hayo yatatokea,unadhani ni nani anastahili/anafaa kumrithi Mizengo Pinda?

Kwa maneno mengine,kuna yeyote mwenye utendaji wa kukushawishi uamini kuwa anafaa kurithi mikoba ya mh.Pinda kutoka katika baraza la mawaziri la sasa?

Kumbuka,kwa mujibu wa gazeti la Nipashe la jana tarehe 08/11/2014,taarifa ya CAG inaweza kuwasilishwa kwa spika wiki hii inayoanza kesho na kisha ikapangiwa siku ya kuwa-tabled bungeni.

Katiba aliyoipendekeza Warioba ingetibu homa hizi zote…Warioba alipendekeza kuwa Mawaziri wasiwe wabunge…lakini maitarahamwe ktk rasimu ya Chenge/Sitta katiba wakaifutilia mbali kipengele hicho..hapo ndipo kwenye tatizo…
Hima Watanzania tuikatae katiba hii ya CCM
 
Hakuna anayefaa kutoka ccm.
Labda wamuazime Prof Lipumba anyooshe mambo kwa muda uliobakia
 
Sasa awe mwnamke tuandike historia.......nampendekeza mama Rwakatale au yule mbunge wa NKENGE,,,Bi. Asumpta Mshama.........au nyie mnaonajeeeeeee.....!!!!!!!!!!!!!!!!

Asumtha Mshana hafai, anasoma kama darasa la pili.
 
==> WAZIRI YEYOTE..KUANZIA MWAKYEMBE, OR PROF. MWANDOSYA, OR HATA MAGUFULI ANAWEZA KUKAIMU HADI UCHAGUZI MKUU UPITE...

ONE OF THOSE ABOVE CAN BE ACTING PM...TILL NEXT YEAR GENERAL ELECTION....Miezi michache ya uchaguzi uliobakia HAKUNA HAJA YA KUMCHAGUA PM MWINGINE....anawekwa Acting PM....Coz Pinda ndio byebyeeee hivyo...hakika hawezi kupona kwa hii scandal ya ESCROW....!!!
 
Back
Top Bottom