Nani anastahili kumrithi Mizengo Pinda?

Nani anastahili kumrithi Mizengo Pinda?

Ndugu wana JF

Ni wazi kuwa kashfa hii ya Escrow itamlazimisha JK kubadilisha baraza lake la mawaziri kwa mara nyingine tena. Naomba tuanze utabiri wetu kama kawaida, nani na nani atakuwepo katika safu hii ya lala salama kuelekea uchaguzi mkuu 2015.

Mimi naanza hapa. Wengine endeleeni

1. Waziri mkuu- Prof Mwandosya
2.Nishati na Madini- Stephen Wasira
3.
4.
5.
6.
7.

Peleka utabiri wako huko si rahisi kihivyo unavyofikiria ndiyo maanamnashirikiana na mafisadi kuhujumu serikali ili baraza la mawaziri livunjwe na nyie mafisadi muweke watu mnaowataka ili muendelee kunyonya rasirimali za taifa letu tunajua wazi chini waziri mkuu PINDA kaminya mianya ya rushwa na ufisadi,Waziri wa Nishati na madini Prof.Muhongo kawashika pabaya mafisadi ndiyo maana nae wanahangaika kumuhujumu ili waweke mtu wao jamani viongozi na watendaji wa serikali ambao wanaonekana kuwa mwiba kwa mafisadi hapa nchini wanapigwa sana vita na mafisadi kwa kutumia wabunge wachumia tumbo,vyombo vya habari uchwara pamoja na magazeti navyo vinatumika kwa kiasi kikubwa na mafisadi katika kuwahujumu watendaji imara wa serikali mf.Magazeti ya Mtanzania,RAI,Mwananchi,The Citizen,Fahamu,Mawio,NIPASHE hayo ni baadhi tu ya magazei ambayo yanamilikiwa na wafanyabiashara hapa nchini kama Rostam Aziz,Reginard Mengi na wengineo ambao wamekuwa wakiyatumia kuwahujumu viongozi wa serikali ambao wamekuwa mwiba kwenye harakati zao kuhujumu rasirimali za Tanzania kupitia kwenye mikataba mibovu yenye manufaa kwa matumbo yao,familia zao na marafiki zao.
 
raisi nae,aondoke,,haiwezekani Anabadili baraza la mawaziri kama pichu,,,inamaana Uteuzi wake umekua hauna mantiki,,,na yeye awajibike sasa,,,

Hivi Tanzania kuna rais kweli. Au picha tu. Sasa hivi yuko usa na bi mdogo anakula bata. Tell me ameshachukua maamuzi gani tokea aingie madarakani maamuzi tote magumu hufanywa na bunge
 
akarithi ili afanye nini? kumbuka kuwa kwa mujibu wa "mama lion" kule green party hakuna aliye msafi; nani alitegemea pinda angechafuka! ukiingia msafi leo kesho unachafuka, hata binyamini alikuwa msafi lakini sasa yukoje?
 
Pinda, Membe na Nyalandu tafadhali sana wasiwe kwenye baraza jipya.......

Wewe hakuna kitu kama hicho(time will tel,wacha tusubiri) ndiyo maana ndugu yangu Ocampo four siku zote nimekuwa nakuambia wewe ni mchanga sana kwenye duru za masuala ya kisiasa hayo unayoyawaza hayawezi kutokea mara kwa mara kwenye posts zako umekuwa ukiwachaua Pinda,Membe na wengineo ambao wamekuwa tishio kwenye mbio za uraisi za Mzee wenu Edward Lowassa kuelekea uchaguzi 2015 kaeni mkijua mbinu zetu hazitofanikiwa na soon mtaumbuka
 
Wadau mie.nafaa kuwa pm sifa ninazo ni mtoto wa kweli wa mkulima kwani nimeishi kijijini na kusoma.shule zetu kuanzia mwanzo hadi mwisho maisha ni kijijini mwinyi anakashfa ya mabomu ya mbagala akipewa itawakumbusha mengi waathirika huku hawajalipwa nime sintasema mpigwe ila cdm hawataachwa watambe labda ukawa nitawaruhusu
 
Ukiangalia mwenendo mzima wa sakata la Tegeta Escrow account,utagundua kuwa, kuna uwezekano mkubwa wa waziri mkuu ambae nae amekuwa akituhumiwa kupata mgao,kuwa implicated katika kashifa hii na hivyo kutakiwa kuwajibika.

Kuna viashiria kadhaa kuwa PM anaweza kutakiwa kuwajibika kwa kujiuzulu.

Mosi,Pinda ametajwa sana kupata mgao(sina uhakika) katika hili sakata na sidhani kama itakuwa ni uzushi tu maana siku zote mambo huanza hivi hivi na mwisho wa siku inageuka kuwa kweli.

Pili,imekuwa ikisemwa kuwa kashifa hii huenda ikaiangusha serikali na mh.Zitto pekee alikwenda mbali zaidi kwa kusema sakata hili linaweza kuangusha "tembo mkubwa".

Sasa mh.Zitto anaposema kashifa hii inaweza kumuangusha tembo mkubwa,hapo alikuwa anamlenga nani zaidi ya waziri mkuu?

Mbali na viashiria hivyo,jambo lingine linalomuweka Pinda katika wakati mgumu wa ku-survive kashifa hii na pia ku-survive vote of no confidence endapo tutafika huko,ni hatua yake ya kujiingiza katika kinyang'anyiro cha uraisi ndani ya CCM.

Kwa mtazamo wangu,wapinzani wake watatumia mwanya huo kummaliza kwa kuhakikisha(ku-facilitate) upigwaji wa kura hiyo na ikipigwa aondoke.

Sasa kwa utangulizi huo,ni dhahiri PM anaweza kuondoka kwa style ile ile ya mtangulizi wake unless ripoti hiyo ya CAG iandaliwe kum-favor(ichakachuliwe).

Je,endapo hayo yatatokea,unadhani ni nani anastahili/anafaa kumrithi Mizengo Pinda?

Kwa maneno mengine,kuna yeyote mwenye utendaji wa kukushawishi uamini kuwa anafaa kurithi mikoba ya mh.Pinda kutoka katika baraza la mawaziri la sasa?

Kumbuka,kwa mujibu wa gazeti la Nipashe la jana tarehe 08/11/2014,taarifa ya CAG inaweza kuwasilishwa kwa spika wiki hii inayoanza kesho na kisha ikapangiwa siku ya kuwa-tabled bungeni.

#NADHANI ushapata confirmation kuwa #Pinda hajakula pesa hiyo.

Now,funga uzi huu utuletee mngine(yaan huu ushakuwa out of date)
 
Wadau mie.nafaa kuwa pm sifa ninazo ni mtoto wa kweli wa mkulima kwani nimeishi kijijini na kusoma.shule zetu kuanzia mwanzo hadi mwisho maisha ni kijijini mwinyi anakashfa ya mabomu ya mbagala akipewa itawakumbusha mengi waathirika huku hawajalipwa nime sintasema mpigwe ila cdm hawataachwa watambe labda ukawa nitawaruhusu

umebemendwa
 
tusubiri report ya CAG itoke na maamuzi ya bunge ndipo tuweze kutoa maoni yetu ;vinginevyo kibao kinaweza kubadilika tuhuma zikatupwa nje kwa sababu za mizengwe mtasemaje?
 
#NADHANI ushapata confirmation kuwa #Pinda hajakula pesa hiyo.

Now,funga uzi huu utuletee mngine(yaan huu ushakuwa out of date)
Hiyo pekee haiwezi kumbeba kwani bado anaweza kuwajibika kwa makosa ya waliochini yake.

Hivyo mh.Pinda bado amekalia kuti kavu na ingekuwa ni nchi za wenzetu,hakika angeshawajibika pasipo kusubiri shinikizo la bunge.
 
#NADHANI ushapata confirmation kuwa #Pinda hajakula pesa hiyo.

Now,funga uzi huu utuletee mngine(yaan huu ushakuwa out of date)
Hiyo pekee haiwezi kumbeba kwani bado anaweza kuwajibika kwa makosa ya waliochini yake.

Hivyo mh.Pinda bado amekalia kuti kavu na ingekuwa ni nchi za wenzetu,hakika angeshawajibika pasipo kusubiri shinikizo la bunge.
 
Back
Top Bottom