Nani anamkumbuka Mzee Majambo?

Nani anamkumbuka Mzee Majambo?

Hivi vijana wenzangu wa zamani, mnamkumbuka mzee Majambo? Alikuwa anavaa vitu fulani hivi miguuni na alikuwa anatembeza na kuuza karanga. Yule mzee alikuwa ananitisha sana na nilikuwa napata wakati mgumu mno nikisika anakuja mtaani kwetu.
pole kikojozi
 
Murukulazo

Asee! Umenikumbusha mbaaali. Wakati huo nlikuwa shule ya vidudu tulikuwa tunaishi kinondoni mtaa wa ufipa. Akipita nlikuwa najificha ndani kwakuwa bb alikuwa anataka nimuone bas alinibeba ili nami nikashangae
kikojozi mwingine tena hapa
 
Nje.....nje....nje.....majambo nje.....nje......
Ni mlio wa kengele huku watoto wakimfuata......watoto wema wasiokojoa vitandani.......
 
Hivi vijana wenzangu wa zamani, mnamkumbuka mzee Majambo? Alikuwa anavaa vitu fulani hivi miguuni na alikuwa anatembeza na kuuza karanga. Yule mzee alikuwa ananitisha sana na nilikuwa napata wakati mgumu mno nikisika anakuja mtaani kwetu.

Hhahahahahaaaa naona watu wanakushambulia ooh mzee majambo alikuwa anajulikana tanzania nzima, tupa kulee wasio mjua mzee majambo walikuwa mikoa ya boarding sie tuliokuwa tunakaa mkoa wa day tunamjua mzee majambo vizuri.
Mie nakumbuka alikuwa akipita kinondoni B karibu na kwa dokta mvungi enzi hizo watoto wote wanaogoma kula wakisikia mzee majambo huyoo wanakula fastaa.
Umenipa taswira ya mtaani kwetu jinsi alivokuwa kipita na kofia yake na kapu la karanga na manyanga yake mkononi akipiga huku na kule na kuimba.
Hope atakuwa ameitwa mbele za haki au may be yuko hai ila wakati huo nilikuwa niko secondary school.
 
Mkuu sema vijana wa zamani wa uswahili ndio tuliokumbana na mzee majambo ,unasepa ukisikia katimba kitaa na wewe umelimwaga kojo kitandani jana usiku au umefanya msala wowote ule na bi mkubwa anaamua kuku discipline kisaikolojia kwa kumtumia mzee majambo na mipengo yake na mngozi wake sijui wa simba ule na ile harufu ya mijasho maana anapiga kwata manzese buguruni tandika nk!
kama yuko hai basi sasa atakuwa kwenye 100++!
 
Hhahahahahaaaa naona watu wanakushambulia ooh mzee majambo alikuwa anajulikana tanzania nzima, tupa kulee wasio mjua mzee majambo walikuwa mikoa ya boarding sie tuliokuwa tunakaa mkoa wa day tunamjua mzee majambo vizuri.
Mie nakumbuka alikuwa akipita kinondoni B karibu na kwa dokta mvungi enzi hizo watoto wote wanaogoma kula wakisikia mzee majambo huyoo wanakula fastaa.
Umenipa taswira ya mtaani kwetu jinsi alivokuwa kipita na kofia yake na kapu la karanga na manyanga yake mkononi akipiga huku na kule na kuimba.
Hope atakuwa ameitwa mbele za haki au may be yuko hai ila wakati huo nilikuwa niko secondary school.

Nimetaarifiwa kuwa alishafariki miaka mingi sana iliyopita!
 
Ha ha ha kweli bora umeuliza...wanavyosema ni as if alikuwa anapita Tanzania nzima kuuza karanga
Zamani Dar ndio Tanzania huko kwenu kote porini tu!hata hizo karanga mlikuwa hamlimi mnaenda kung'oa au kuchuma tu porini!
 
kwa ufupi wote waliomuogopa walikuwa vikojozi akiwemo mtoa mada bila shaka!unaruhusiwa kukanusha #Murukulazo
Ukikojozi kile cheo kama kupiga puu tu asilimia kubwa ya marijari wamepitia! hata wewe unalimwaga kojosema ulikuwa unaamka night unachenji kivazi unamweka mdogo kwenye "bwawa"lako na kumsingiziayeye ndiye "kabwanda"
 
kwa mtu aliyekaa dar miaka ya tisini lazima uwe unamjua mzee majambo..watu walikuwa wanasema ana nyumba kumi na pia ni usalama wa taifa. haka kawimbo tulitungiwa na mama zetu "mimi majambo nakula watuuu"

Jiulize why alikuwa anapatikana sana mitaa ya Makumbusho, K/nyama, Kinondoni, Mwananyamala, and kuna mdau mmoja kachangia kuwa hadi mitaa ya TMK - Chang'ombe alikuwa anagusa.
 
Mkuu.
Niliishi Dunga pia.
Babu alikuwa anatembea kwa mguu jiji zima.
Mfano pale kwetu alikuwa akitokea msasani, kisha anaingia Drive-in,kisha Moroko ananyooka kama anaenda Magomeni, kisha anakatisha kulia anaingia Dunga street. Anakujatokea magenge ya Msufini kisha huyooo Msisiri anaishia zake Mwananyamala.

Alikuwa msanii kwa ujumla.
Watu wazima pia waliinjoi kumuona.
Isipokuwa alikuwa na kawimbo kake kanasema "mimi majambo nakula watu" kisha anakanyaga kishindo kuliza kengele/ manyanga yake nje nje njee!.
Hicho ndicho kilichokuwa kinatutisha watoto.
Na pia hapakuwa na mtoto anaesalia nje.
Yaani vikojozi na wasio vikojozi woote tulitimua mbio kuogopa kuliwa na Majambo.

Nb.
mkuu, Dunga iko Moroko siyo Kinondoni b.

Babu alikuwa anagusa mitaa yote-nadhani jiji zima, kila akipiga mguu chini kuliza manyanga yake - basi wale akina bro and wakubwa wasiomwogopa walikuwa wanaitikia "majambo njeee"
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom