Mkuu.
Niliishi Dunga pia.
Babu alikuwa anatembea kwa mguu jiji zima.
Mfano pale kwetu alikuwa akitokea msasani, kisha anaingia Drive-in,kisha Moroko ananyooka kama anaenda Magomeni, kisha anakatisha kulia anaingia Dunga street. Anakujatokea magenge ya Msufini kisha huyooo Msisiri anaishia zake Mwananyamala.
Alikuwa msanii kwa ujumla.
Watu wazima pia waliinjoi kumuona.
Isipokuwa alikuwa na kawimbo kake kanasema "mimi majambo nakula watu" kisha anakanyaga kishindo kuliza kengele/ manyanga yake nje nje njee!.
Hicho ndicho kilichokuwa kinatutisha watoto.
Na pia hapakuwa na mtoto anaesalia nje.
Yaani vikojozi na wasio vikojozi woote tulitimua mbio kuogopa kuliwa na Majambo.
Nb.
mkuu, Dunga iko Moroko siyo Kinondoni b.