Nani analifahamu jimbo la Tandahimba?

trachomatis

JF-Expert Member
Jun 7, 2011
3,758
722
Tandahimba ni jimbo la uchaguzi na pia ni wilaya katika mkoa wa Mtwara. Population ni 240,000 hivi.Kielimu iko nyuma kama maeneo mengine ya kusini yalivyo.Si ajabu mtu wa miaka 30 hadi 40 asiyejua kusoma. Misimu ni miwili tu mvua na jua.

Umeme ukikatika maji ya bomba hayapatikani. Ila umeme hukatika kwa nadra sana kwa kuwa unatumika wa gesi ya Mnazi Bay. Korosho ndiyo tegemeo kubwa kwa uchumi wa wilaya hii.


Halmashauri ya Tandahimba inashindana na Mji /Manispaa kama Ilala kwa mapato! Mfano mwaka wa fedha uliopita takribani bilioni 55 zilipatikana..! Ili kufika Tandahimba inakubidi ufike Mtwara na kufuata barabara ya changarawe kwa urefu km 96.Kipindi cha mvua na baada ya kipindi hicho kunakuwa na mahandaki ya kutisha sana barabarani.

Tangu kufariki Mh Nandonde (mbunge maarufu sana enzi hizo wa Tandahimba) hili jimbo mbunge hufikisha kipindi kimoja tu cha miaka mitano! 2010 ndiyo imevunja rekodi,Mh Juma Njwayo alishinda kwa tabu sana mchujo wa chama chake hadi kupelekea wengi kwenye chama chake kutompenda. ''Alimshinda'' mgombea kijana wa CUF Ahmad Katani.

Tuache mengine yote,lakini kinachonifanya niweke hii thread ni sera moja ya CDM. Kwamba maeneo yenye uwezo kiuchumi yaboreshwe kwanza yenyewe na kwa utaratibu maalum maeneo yasiyozalisha ndipo yaje kupewa mgawo.

Karibuni wana JF kuchangia lolote katika maelez yoyote hapo juu.
 

mfereji maringo

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
1,034
250
Mbunge wa tandahimba mh. juma njwayo hakubaliki hata kijijini kwao mchichira na zaidi kwa kuwa watu wengi wanaamini alishinda kwa magumashi basi wanamuwinda kama popo hawezi kushuka ktk gari yake akatembea kwa amani mitaani.

Watu wanaweza mpiga, yeye mwenyewe anawalaumu watumishi wa halmashauri eti ni wanafiki kwa kuwa wakati wa uchaguzi kituo cha kupigia kura pale halmashauri ambapo wakazi wengi ni watumishi mgombea wa cuf aliongoza kwa kura nyingi.
 

trachomatis

JF-Expert Member
Jun 7, 2011
3,758
722
Kweli mfereji m. Naomba unitajie walau idadi ya wabunge tangu kuachwa jimbo na Nandonde.Na kama unawafahamu nitajie.
 

Chakunyuma

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
810
151
sasa sijaelewa ina maana chadema wametia miguu? ila njwayo nilimuona amepiga picha na rizione wakati anapata uwakili sasa sijui ndio kampi ya jk au EL? vp Katani hajafungua kesi kupinga matokeo? kama amefungua inaendeleaje?
 

THINKINGBEING

JF-Expert Member
Aug 9, 2010
2,778
1,303
Tandahimba yenye uhakika wa umeme wa Mnazi Bay,Tandahimba yenye mapato makubwa yatokanayo na korosho,Tandahimba maskini.
Kinacholsababisha umaskini si kutokuwepo kwa rasilimali muhimu katika uzalishaji mali.

Kinachosababisha umaskini si mfumo wa uzalishaji wala mbinu dhaifu za uzalishaji mali. Umaskini unaletwa na mfumo mbovu wa ugawanaji mali.

Ukiachilia mbali umeme wa mnazi bay na korosho,hata ukiiongezea tandahimba dhahabu,almasi,tanzanite na mafuta;chini ya utawala wa CCM bado itaendelea kuwa maskini wa kutupwa.
 

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,882
Sasa umesema sema sera ya Chedama iko wazi na itumike ila kwa sasa haiwezi maana ma CCM ndiyo yako huko .Tujadili nini mkuu ? Hebu watu wa huko pembezoni watupe habari zaidi juu ya Tandahimba .Huko ndiko walimpa joto ya jiwe aliye kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo ndugu Miti ? Maana wananchi waliitikia Tandahimba hoiiiiiiiiiiiii badala ya Tandahimba hoyeeeeeeeeeeeee.
 

Dopas

JF-Expert Member
Aug 14, 2010
1,151
392
Kama wakazi wengi hawajui kusoma, huwezi kushangaa kama rasilimali hizo zikifaidisha mafisadi. Ni aibu mtu mwenye miaka 30 au 40 asijue kusoma Tanzania. Kwani ilianzishwa gombaru miaka ile kwaajili ya kuwaokoa watu wenye umri mkubwa walikosa nafasi ya kuingia darasa. Ni aibu lakini si kosa lao. Ni uongozi mbovu.
 

sifongo

JF-Expert Member
Jun 5, 2011
4,896
5,294
Kingine khs tandahimba ni mila potofu juu ya ndoa kuna kitu kinaitwa safisha ghala maana yake baba kumtaliki mke wake kipindi wakishavuna korosho japo mama ndiye aliyetumika sana shambani,ukiuliza kwanini wanakuambia mke ameshachoka sababu ya Jembe hii kitu ilinishangaza sijasimuliwa nimejionea mwenyewe.
 

mfianchi

Platinum Member
Jul 1, 2009
11,244
7,197
Bwana shamba Juma Njwayo ni mganga njaa tu,kwa tunaomfahamu anapenda sana kuongea na kujipendekeza kwa mtu anyemuona ana nafasi fulani,hao ndio wabunge ambao wao ni ndiooo huku anamwangalia Waziri mkuu kwa kutaka aonekane ni kijana mwenye nidhamu,kama ilivyo ada ya wabunge wengi huko Tandahimba ni kwa ajili ya kupatia kura tu maisha yapo Dar
 

trachomatis

JF-Expert Member
Jun 7, 2011
3,758
722
Kingine khs tandahimba ni mila potofu juu ya ndoa kuna kitu kinaitwa safisha ghala maana yake baba kumtaliki mke wake kipindi wakishavuna korosho japo mama ndiye aliyetumika sana shambani,ukiuliza kwanini wanakuambia mke ameshachoka sababu ya Jembe hii kitu ilinishangaza sijasimuliwa nimejionea mwenyewe.
Kweli kabisa. Ingawa panabadilika kwa haraka. Na tamaduni ovu kama hizo zinafifia kwa kasi. Wageni wanaongezeka. Ilikuwa shida kwa matajiri kufanya maendeleo mfano nyumba nzuri,gari n.k.wakiogopa kulogana lakini kwa sasa kila mtu anafanya maendeleo.Wa kuboresha makazi, kupanua miradi,kuongeza mashamba,magari,pikipiki n.k. Msimu wa korosho ndiyo umeanza. Utaisha mwezi Januari ama Februari. Kwa kipindi hiki hela inatembea wilayani utasema ni mji mdogo!
 

prakatatumba

JF-Expert Member
Oct 17, 2011
1,329
188
Mmejitakia wenyewe,nyie hambadilishi upepo,mmeng'ang'ania magamba tu,2015 ndyo mkombozi wenu mkishangaa subirini 2020 nitakapo kuja kuomba kura za ubunge
 

trachomatis

JF-Expert Member
Jun 7, 2011
3,758
722
Bwana shamba Juma Njwayo ni mganga njaa tu,kwa tunaomfahamu anapenda sana kuongea na kujipendekeza kwa mtu anyemuona ana nafasi fulani,hao ndio wabunge ambao wao ni ndiooo huku anamwangalia Waziri mkuu kwa kutaka aonekane ni kijana mwenye nidhamu,kama ilivyo ada ya wabunge wengi huko Tandahimba ni kwa ajili ya kupatia kura tu maisha yapo Dar
ni kweli mfianchi. Wajua kuna waliowahi kusema hata boga ukilisimamisha kugombea kwa tiketi ya chama tawala,litashinda. Na kushinda kwenyewe kwa chama tawala ndiyo hivyo tena.
 

trachomatis

JF-Expert Member
Jun 7, 2011
3,758
722
Mmejitakia wenyewe,nyie hambadilishi upepo,mmeng'ang'ania magamba tu,2015 ndyo mkombozi wenu mkishangaa subirini 2020 nitakapo kuja kuomba kura za ubunge
kwa taarifa yako mbunge aliyewahi kupendwa Tandahimba ni mmoja tu. Nandonde. Aliwahi kuitwa mtani wa bunge. Aliwahi kuingia bungeni akiwa katapakaa tope. Walipomuuliza kwa nini alijibu bila serikali kuona halihalisi haiwezi kuelewa kelele za kusema kuna shida kubwa ya barabara.
 

trachomatis

JF-Expert Member
Jun 7, 2011
3,758
722
Mmejitakia wenyewe,nyie hambadilishi upepo,mmeng'ang'ania magamba tu,2015 ndyo mkombozi wenu mkishangaa subirini 2020 nitakapo kuja kuomba kura za ubunge
kwa taarifa yako pia huku hakuwahi kuchukua vipindi viwili mbunge yeyote baada ya Nandonde. Kwa mara ya kwanza ndiyo huyu Juma Njwayo. Wana CCM wengi inasemekana hawakumpenda. Alikuwepo mtoto wa hayati Nandonde,ambaye inasemekana alikuwa rahisi kuuzika kwa wananchi kuliko Juma N. ambaye ililazimu defender na mabomu ya machozi,amri ya kutotembea zaidi ya saa 3 ili kumhalalisha!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom