Nani Anajua Namna ya Kumsaidia Huyu Mdada? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani Anajua Namna ya Kumsaidia Huyu Mdada?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Boflo, May 19, 2010.

 1. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  haya ndio maelezo yake:-

  Habari zenu marafiki ?

  Mimi ni mwanamke mwenye miaka 27 kwasasa nina mtoto mmoja wa kike ambae nilizaa na mshenzi mmoja miaka mitano iliyopita.
  Huyo jamaa jina lake linaanziwa na K, alinikimbia toka kipindi cha mimba na alikuwa akiwaambia watu kuwa mimba sio yake,kwa kudra za mwenyezi Mungu nilijifungua salama na mtoto amefafana na baba yake kupita kiasi.
  Toka kipindi cha mimba mpake leo hii mtoto ana miaka 5 sijawahi kuona hata senti ya huyo kaka kwa ajili ya malezi ya mtoto, huyo kaka ana kazi nzuri sana na analipwa mshahara mzuri tu kwa kweli.
  Swali langu ni kwamba nikimpeleka mahakamani je ataamuriwa kunipa pesa za mtoto? Je pesa za nyuma na hizo ataambiwa anilipe? Je ni kiasi gani kwa mwaka anaweza kuamuriwa anipe. Mshahara wake kwa mwezi sio chini ya milioni 3
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  May 19, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,336
  Likes Received: 22,188
  Trophy Points: 280
  Nenda ustawi wa jamii watakusaidia sana kwa kila aina ya ushauri na kila swali lako litajibiwa kikamilifu nan utapata suluhu ya tatizo lako.
   
 3. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #3
  May 19, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,481
  Likes Received: 2,083
  Trophy Points: 280
  nenda TAMWA watakusaidia mara moja kwa ushauri na watakupa na mwanasheria wao
   
 4. m

  muhanga JF-Expert Member

  #4
  May 19, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 873
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  pole sana dear, kama wengine walivyoshauri nenda tamwa au ofisi za usatawi wa jamii watakupa msaada unaohitaji. Hata hivyo kama mtu hataki mtoto wake usimlazimishe, kwani hata mtoto atajisikia vibaya akijakuwa na akili timamu agundue namna ambavyo babake alimkana na ikafikia hatua ya kulumbana ili tu apate mahitaji yake muhimu. Huyo baba iko siku atakuja kujuta kwa kosa hilo na itamuwia vigumu sana hata kurudi kujieleza hadi umuelewa hapo mtoto atakapokuwa mkubwa. La muhimu tu wewe kama mama, jitahidi ufanye kazi kwa biddiii uweze kumudu mahitaji muhimu ya mtoto Mwenyezi Mungu atakuwezesha Inshaalah
   
 5. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #5
  May 19, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Amefanana na huyo mshenzi???!!!
   
 6. K

  KABAZI JF-Expert Member

  #6
  May 19, 2010
  Joined: Apr 19, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Awasiliane na WLAC (Women for Legal Action) kwa namba zifuatazo 0785-066555 au 0757-726660. Hapa utapata msaada wa kisheria kupitia hizo namba.
   
 7. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #7
  May 19, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Brigita good observation, how can you call baba wa mtoto wako Mshenzi!!?

  By the way sijamuelewa wifi anachotaka, kaka si alishamkataa mtoto tangu akiwa mimba? Sasa wewe unataka kumpeleka mahakamani ili amkubali au ili akupe pesa za fidia? Na je ukishalipwa unamkabidhi kwa babake au ndo inakuwaje sasa? Mimi nafikiri ungefurahi kuwa umeachiwa zawadi ya mtoto. na wala usisikie uchungu kumlea mwanao, she is yours for God's Sake
   
 8. m

  muhanga JF-Expert Member

  #8
  May 19, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 873
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  ni kweli uliyosema nami nadhani angemshukuru Mungu tu kwa hali ilivyo, huyo mume anaweza akaitwa asikubali hata mtoto mwenyewe juu ya kufanana
   
 9. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #9
  May 19, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Natamani ungekuwa na uwezo wa kumtunza mwanao kama wewe.kama baba yake alishakataa mimba tangu zamani ni tatizo.
   
 10. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #10
  May 19, 2010
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  mnahukumu upande mmoja .....amshauri huyo mshenzi wakapime DNA ka mwanamke hajala kona:yuck:
   
 11. B

  Boney E.M. JF-Expert Member

  #11
  May 19, 2010
  Joined: Jan 22, 2007
  Messages: 425
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Ukimwita baba watoto wako mshenzi wewe utakuwa nani? Jifikirie na utupatie jibu.
   
 12. Y

  Yetu Macho JF-Expert Member

  #12
  May 19, 2010
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Tatizo ni kupata hizo hela za matunzo kama sehemu ya mchango wa baba ktk matunzo ya mtoto au tatizo ni mshahara anaopokea? Maana yaonekana unautamani sana huo mshiko anaokamata...

  Naimani pia unaweza kumtunza mwenyewe kama ulivyofanya for the past 5 yrs na kama wengi wanavyofanya.

  Kama tatizo ni hizo Milioni 3 inawezekana mtazamo wako ni kwamba ukienda mahakamani ataambiwa akugawie asilimia flani ktk hizo. Itakula kwako utapoambiwa atakupa buku kwa siku na atakua anapeleka ustawi wa jamii na utatakiwa ukazichukue kila siku. Nauli tu toka kwako mpaka ofisi ya ustafi ni mara tano ya hiyo leave alone kama unaendesha.

  Tafakari- Chukua hatua
   
 13. tete'a'tete

  tete'a'tete JF-Expert Member

  #13
  May 19, 2010
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 474
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakati wanajamiiana alikuwa hamjui huyo kuwa ni mshenzi!! kwanza hana adabu...inaelekewa huyo dada ana lugha chafu na ndio maana hata huyo mshenzi alikataa mimba...next time akikutana na mwanaume awe na kauli nzuri kwani midomo siku zote inajenga....pia kama alikataa mimba mshukuru mungu alikusaidia ulishamlea huyo mtoto siku zote ushindwe sasa omba mungu fanya kazi umlee mwanao...ukishindwa mpeleke kwenye vituo vya kulelea watoto vipo vingi tuu...
   
 14. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #14
  May 19, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  ni haki yake kuhakikisha baba mtoto anatoa pesa ya malezi ya mtoto. haijalishi kama aliikataa mimba awali au la.

  mtoto anaweza kuwa anakosa hudua muhimu kwa kuwa mama labda hana pesa ya kutosha kumhudumia.

  akifungua kesi mahakama itamwita jamaa, atapimwa dna na kama mwana ni wake kweli, atalazimika kumpatia pesa za matumizi na wala haitamamuru ampe mtoto huyu mwanamme.

  haki ya mtu inapiganiwa haiji tu ....................pigania haki ya mtoto wako lakini epuka kumuita baba yake mwanao mshenzi hasa kama una nia ya kumshirikisha kwenye malezi ya mtoto wenu
   
 15. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #15
  May 19, 2010
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Endelea tu kumtunza mwanao-afu cha ajabu wewe unasema mshenzi afu ukisha chukua pesa za mshenzi wewe utakuwa mshenzi pia- au vipi?
   
 16. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #16
  May 19, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Kama ameweza kumlea mwenyewe huyu mtoto mpaka amefikisha umri wa miaka mitano,mimi sidhani kama
  anahitaji tena msaada wa huyo mwanaume mshenzi..Mi namshauri amlee yeye mwenyewe..
   
 17. Gerad2008

  Gerad2008 JF-Expert Member

  #17
  May 19, 2010
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 489
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Hebu dada tueleze ushenzi wa huyu baba ulianza mkiwa bado freinds au baada ya kumkana mtoto? je mlikubaliana mtazaaa au mlikuwa tu rafiki wa kawaida kimapenzi ili kila mtu achukue hamsini zake baada ya hapo?

  wewe kwa nini hukumtafuta huko nyuma mpaka ukasubiri alipopata kazi ya mshahara wa millioni 3 ndo umtafute je huoni wewe huna tatizo la hizo hela?
   
 18. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #18
  May 19, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  huyo dada ni mshenzi ndio maana alipata mshenzi mwenzake,na ana tamaa ya hela ya huyo mshenzi na inavyoonekana huy jamaa ni mshenzi kwelikweli.sasa nampa huyo dada tahadhari popote atakapoenda iwe ustawi wa jamii,tamwa nk jamaa atamriwa ampe si zaidi ya buku jero kwa siku sasa kwa tamaa yake ya hela huyo mshenzi atmdanganya na bia ata

  mtwanga nyingine.
   
 19. E

  Edo JF-Expert Member

  #19
  May 19, 2010
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Kama walivyosema wenzangu, hapa lipo jambo. La msingi mlee mwanao, huna haja ya kumfuata "mshenzi", japo sina hakika kama kweli anastahili jina hilo. Kwa maelezo yako kama kweli ni 'mshenzi" angepata kazi nzuri? Nahisi ulimtibua saaaaaana wakati ule ndo maana jamaa kaamua kutupa jongoo na mti wake. Hebu kumbuka ilikuwaje mpaka akakata mawasilianao, kuna jambo, tafakari kwa kina, kama ulikosa, omba msamaha, nadhani anaweza kumtunza mwanae !
   
 20. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #20
  May 19, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  jitahidiumtunze mwanao kwani kama baba alishakataa mimba haina maana kumkumbusha sa hizi wala usitake pesa yake endelea kulea mbona umeweza mpaka miaka5!
  alafu usimwite baba mtoto mshenzi, kwann nawe ulitembea na mshenzi? na ukazaa mshenzi?
   
Loading...