Nani anajua kwa hakika kwanini Rais anachukua muda mwingi sana huko aliko?

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
13,813
18,546
Sisi kama wananchi hatujui kama rais yupo quarantine, anaugua au anauguza. Tuna haki ya kujua japo hata kwa kiasi fulani hali ya kiongozi wetu na sababu za yeye kuwepo kwa muda wa zaidi ya siku 45 sasa nje ya makazi yake rasmi. Yeye ni kiongozi wa nchi sio kiongozi wa kampuni binafsi. Hata wenye makampuni binafsi huwaambia waajiriwa wao juu ya kutokuwepo kazini kwa boss wao.

Watu wangejua ukweli haya maneno mengi wala yasingekuwepo.

Waziri mkuu wa Uingereza alisema waziwazi kuwa anaugua corona. Mwana mfalme wa Uingereza Prince Charles alitangaza hadharani kuwa amekutwa positive corona. Wapo viongozi wengi tu Ulaya na America wameweka wazi hali zao. Ni kwanini sisi tunaficha ugonjwa huu na kufanya kuwa jambo binafsi wakati tunajua kuwa hii ni pandemic na inamhusu kila mtu?

Mimi nimejifunza jambo; kwamba sisi waafrika baado sana kuwa na fikra huru. Unaweza kuona wasomi na madigrii yao lakini fikra zao bado ni sawa na wasiosoma darasa hata moja. Na hii ndio sababu maendeleo ya Afrika ama yamebaki pale pale tangu uhuru au mambo yamekuwa mabaya zaidi kuliko kabla ya uhuru.

Mambo ya kienyeji yatufanya tushindwe kuendelea miaka nenda rudi. Watu wamekuwa wakiuliza kwanini Afrika haindelei, nafikiri mnaweza kujionea wenyewe sababu.
 
Wanasheria wapeni ushauri wananchi, kwa sababu msingi wa dola upo kwa wananchi na kwa sababu cheo cha Urais kipo ki katiba, Je wana uwezo wa kuhoji mahakamani Rais wao alipo? na kwa nini yupo huko aliko?
 
Hivi mtu anapoji Isolate kipindi hiki cha corona hupati majibu tu mpaka upewe?

Mkuu jiongeze.....!
 
Musa alifunga kwa siku 40 huku akijitenga na watu wake, na kilivaa kwa dhati jukumu kubwa la kuwapeleka wana Israel nchi ya ahadi, nchi iliyojaa maziwa na asali. Pengine tujipe muda na tusubiri, labda zifikapo siku 40 za kujichimbia Mzee anaweza kuibuka na maono mazito ya kulinusuru taifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
.
tapatalk_1589233528561.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa afrika tofauti ya kusoma na kutokusoma ni ndogo zana. Labda tu ni kwa kuwa msomi anapata mshahara mkubwa lakini zaidi ya hapo hakuna maana yoyote ya kwenda shule.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom