Ana shahada ya kwanza na ya pili kutoka chuo kikuu cha Dar. Ni wakili wa mahakama kuu ya Tanzania. Shahada ya kwanza sijui alisoma nini lakini ya pili ni LL.M. Ameshiriki sana katika ukombozi wa Bara la Afrika na aliwahi kuwa kiongozi wa vijana barani humo huko Algeria. amesafiri sana duniani. Anajua Kiingereza, Kireno, Kiswahili na bila shaka na Kifaransa. Jenerali siyo tu kwamba amesoma bali anasoma sana. Amewahi kuwa mbunge na pia mkuu wa wilaya nadhani Ilala, baadaye akahamishiwa mikoa fulani ya kati,Singida au Dodoma, akakataa maana nasikia kulikuwa na figisu figisu na Waziri Mkuu wa wakati huo Bw. Malecela. Ni kati ya watanzania wachache wanaosoma sana, ni sampuli ya Zitto. Ana msimamo usiotetereka. Wakati wa Mkapa alitengenezewa zengwe kwamba siyo raia wa Tanzania ikiwa ni visa tu kwa vile alikuwa akiukosoa utawala wa Mkapa jambo ambalo lililalamikiwa sana na baadhi watu nchini na duniani.