Nani anajua elimu ya mwandishi Ulimwengu?

Nani anajua elimu ya mwandishi Ulimwengu?

Ni tabia za watawala walio wengi hawapendi kuambiwa ukweli, watakung'oa kucha ikiwezekana hata kukuua kbs as if wao wataishi milele
 
Mleta hoja anadhihirisha kama taifa kuna tatizo kubwa! Hata kama huyo Jenerali hajasoma kabisa mchango wake uheshimiwe kwani hata waliosoma kama hawawezi kutukwamua hiyo elimu yao haina maana katika jamii
 
Elimu ni nini .....je n vidato hapana ....je n university hapana....je n madarasa hapana bas elimu ni nini....?
 
Hivi mwandishi wa magazeti hapa Bongo ajulikanaye kama Ulimwengu ana Elimu gani? Kwa maana hakuna mahali ninapoweza kusoma elimu yake, isijekuwa ni Mbowe type!
Elimu yake unaitaka ya nn ,elimu siyo kigezo cha ufanisi, ukienda Busoga university Uganda watu wanapata shahada( Degree) kwa muda Wa miezi 3 badala ya miaka 3 ,sasa we ulivyo na ubongo mdogo unahangaika na elimu za watu,angalia ufanisi wake katika kazi
 
Hivi mwandishi wa magazeti hapa Bongo ajulikanaye kama Ulimwengu ana Elimu gani? Kwa maana hakuna mahali ninapoweza kusoma elimu yake, isijekuwa ni Mbowe type!
Ndugu yangu,
Mpinge Jenerali Ulimwengu kwa hoja.
Haya mabezo hayasaidii hata kama hakuwahi kuingia shule hata siku moja ilimradi hoja zake zina mantiki.
Babu yangu alikuwa bonge la kichwa hata kama hajaenda shule.

Hata hapa JF hakuna anayejua elimu ya Barbarosa...kwa nini tukusikilize???
 
Barbarosa vp mbona umeamua kupita njia ya mkato mapema kuhusu ulimwengu.

NB:nakumbuka siku zile wakati max melo yupo lupango,ulikuwa unatuma post kuonyesha ni namna gani umefurahia tukio lile.nimekumbuka tu.
 
Unaweza kuhoji makala zake, lakinj unapohoji elimu ya Jenerali Ulimwengu unaonyesha ni jinsi gani ulivyokuwa mteke kwenye siasa za Tanzania na historia ya ukombozi kusini mwa Afrika. Ulimwengu ni mhitimu wa chuo kikuu dar es salaam na amejiendeleza sehemu mbalimbali duniani.
Na pia ni Wakili wa Mahakama Kuu aliapishwa siku aliyoapishwa Werema kuwa Wakili mwaka 2012.
 
Mjengwa alishawahi kunipigia simu akisema yeye sio muandishi wa habari bali ni mwandishi wa makala......kama hii ni kweli basi Generali sio muandishi wa habari
Hawajui tofauti kati ya mwandishi wa habari na mwandishi wa Makala
 
Dah.... Ni jenerali wa jeshi..... Ana elimu ya juu(miye nampa PhD)..... Ni mwandishi wa makala mahiri sana....makala zake huwa zenye kufikirisha sana.....binafsi huwa sipendi kuzikosa....
Ila si mzalendo wa kweli.. ni muoga na laini sana....ninamlaumu sana kwa alichokifanya 2005...hata yeye nadhani anajutia... .na yale aliyoyaachia njiani pale BMT[emoji13] [emoji13]
 
Kwani kuwa PhD ndio nn? Mbona mzee Ruksa ana elimu ya kawaida tu na ka perform vizuri sana hawa a kina bwana yule wanatokwa na mapovu tu mwaka umekwisha , teuwa tengua.kila mmoja yuko high hatujui bangwe au viroba.
 
Ndalama you are not right, knowledgeable how? Talk of the talking? Huyu ni Mbowe type tu. Si unaona huwa ni mlopokaji tu na hajui kujenga hoja. Kama angekuwa na elimu ya ukweli, CV yake ingekuwa inajulikana na hata chuo alichohitimu kingejulikana na watu aliosoma nao wangejulikana na gata walimu waliomfundisha wangejulikana. Hili jamaa ni KIHIYO.
 
Hivi mwandishi wa magazeti hapa Bongo ajulikanaye kama Ulimwengu ana Elimu gani? Kwa maana hakuna mahali ninapoweza kusoma elimu yake, isijekuwa ni Mbowe type!
Wewe kinuka mkojo una matatizo gani?
 
Mzeeee ulimwengu n genius ata shvji anajua hilo cyo kama wale wenye ma phd yasiyo kuwa na tija kwa taifa na hizo ndo zmejaaaa katka nchi hiii
Achen tittle watanzaniaa
Think big kama ulmwengu
 
Na pia Wakili wa Mahakama kuu ya Tanzania. Na pia ni mtu wa kwanza akiwa sehemu ya serikali kama mkuu wa wilaya na akiwa mbuge kupitia vijana CCM aliyethubutu kuisema serikali bungeni kuwa imeoza. Kipindi hicho John Malecela akiw waziri mkuu, wakamtuhumu hawezi isema serikali vibaya akiwa sehemu ya serikali. Akasema hawezi fungwa mdomo kwa kuw serikali na hapo akaamua kujiuzuru ukuu wa wilaya. Elewa tu kuw ni mtu anayejitambua
 
Watu wa mlengo huu wa kisiasa mnakatisha tamaa hata watu wanàopenda kujadili mambo bila ushabiki, hivi mtu akitoa mawazo yenye kukosoa utendaji wa MTU Wa upande wenu ndo chanzo cha kuanza kutafuta elimu yake, uraia wake, familia yake, marafiki zake, vinywaji anavyopendelea na nini sijui.? Watu wenye Id za sehemu tunazoziheshimu kama yako hukupaswa kuwa na mawazo ya ovyo kama hayo, au umekosoa jina lako halina "wi" baada ya "m"? Na wewe tuanze kutafuta ulisoma shule gani maana umeandika "Generali" badala ya General au Jenerali!! Hatuna Generali kwenye lugha ya kiswahili. Hivi Mara siku hizi wanazaliwa watu Wa aina yako kweli? Masikini Mara!! Ulikuwa unazalisha Viongozi na watu wenye maono Leo "unatotoa" wambea na wachimba chumvi wanaotafuta kasoro za watu badala ya kufanyia Kazi au kukosoa kwa hoja mawazo yao!!? Kama unahusudu umbea badilisha ID uwafuate waliozoea Kazi hiyo, usiwadhalilishe watu jasiri Wa Mara vinginevyo tutakuita m**senge1993 ili uendane na mawazo yako. Haya; "Mzee Ulimwengu ni darasa la 8, hana mke , ana hawala 2, anapendelea konyagi na mvinyo wa Kirusi, hana Kazi maalum, anàongea baadhi ya maneno ya kiingereza kwa sababu alikaa karibu na ubalozi Wa Uingereza" Haya ndo ulikuwa huyajui juu yake.
Sawa kabisa ni Jenerali badala ya Generali, jamaa aliulizia kuhusu elimu ya Jenerali mimi nikaeleza nachofahamu kuhusu elimu yake, naona wewe unanishambulia mimi, basi sitarudia tena.
Mara wamezaliwa watu wa aina yangu siku nyingi kuanzia kwa mtemi Makongoro, Burito, kuja kwenye kizazi cha Munasa Sabhi,Mutaragara Chirangi na Josephat Kiboko Nyerere.Kwa hiyo usiondoe 'Mwi' maana utakuwa unatukosea sisi wanaMara
 
Sawa kabisa ni Jenerali badala ya Generali, jamaa aliulizia kuhusu elimu ya Jenerali mimi nikaeleza nachofahamu kuhusu elimu yake, naona wewe unanishambulia mimi, basi sitarudia tena.
Mara wamezaliwa watu wa aina yangu siku nyingi kuanzia kwa mtemi Makongoro, Burito, kuja kwenye kizazi cha Munasa Sabhi,Mutaragara Chirangi na Josephat Kiboko Nyerere.Kwa hiyo usiondoe 'Mwi' maana utakuwa unatukosea sisi wanaMara
Nashukru kwa vile bado unajitambua, rai yangu kwako, wanaojitambua hawashambulii personality!
 
Back
Top Bottom