...mimi ni mkazi wa kijiji cha Kinyerezi, nimezungukwa na high profiles politicains wa zamani na wa sasa ninawaona waliokuwa wazuri na wabovu kwa sababu you can tell kutokana na life style zao, mmoja wa majirani zangu wa karibu sana ni Mzee Apiyo na Mahita, you can tell kwamba Mzee apiyo alikuwa ni kiongozi safi, masikini ya Mungu hana kitu kabisaa, lakini ninawangalia majirani zangu wengine kama Mahita.
...sasa hatuwezi kuwatukana viongozi wetu wote kwa sababu ya wezi wachache
Kwamba kiongozi ambae hakuiba ndio kiongozi safi hilo sidhani ni kweli. Kutokuiba, unategemewa usiibe, si sifa. Kutokuiba yabidi kuwe the least common denominator. Zaidi ya maadili, tupime viongozi kwa ufanisi, maono uzoefu, matokeo, fikra, kujitoa katika utumishi, na uchochezi chanya, na pia kutovumilia maovu. Field Marshall ni muadilifu, msafi, sawa, je alifanya nini alipoona uchafu? Ana balls za kukemea maovu?
Na uadilifu wenyewe tusiupime kwa kuangalia "life styles" za wastaafu. Hao unaosema majirani zako wastaafu wasafi wa Kinyerezi, wametangaza mali zao zote Tume ya Maadili? Ni vigumu kujua. Utawezaje kujua mali na vipato vya Kingozi wa Tanzania wakati hata mshahara wa Rais ni siri kali ya serikali?
I seriously respect your view, lakini naomba nikuulize kwa nini umeng'ang'ania kubaki ndani ya chama wakati uongozi wa juu mzima wa CCM hivi sasa ni wanamtandao? They are ineffective na walikuwa part and parcel of one of the most corrupt and sleazy campaign in the history of Tanzania.
MKUU
UNAJUAJE KAMA FMES siyo mmoja wao hao uliowataja hapo juu?
Ngoja nikukumbushe, wakiwa kwenye majukwaa na maeneo yao ya kujidai wanawakemea mafisadi,lakini waulize waseme ni nani kati yao? kila mtu hamjui nani ni fisadi kati yao!!! inawezekana kweli? Maneno mazuri ndiyo silaha yao ,je unakumbuka ile slogan ya "HARI MPYA ,NGUVU MPYA NA KASI MPYA? iko wapi ni NGUVU YA GESI, NI KASI YA KINYONGA? HARI YA GONJWA?
MAJIBU UNAYO MKUU ,FMES .MKIONGEA LUGHA NI NZURI KWENYE VITENDO NI UBADHIRIFU.
Kwa kuwa kuna wanaofaidika na hali hii sasa ni wakati muafaka wa kuwakataa na haya maghala ni lazima yachomwe moto. Kwa kuwa maghala yanalindwa usiku na mchana, hawa walinzi wa maghala haya ya kifisadi lazima tuanze nao kwa kuwachoma moto.
CCM inaongozwa na MH Rostam Aziz Mbunge wa jimbo la Igunga chini ya mshauri mkuu wa Mambo ya Siasa na Uchumi MH Lowassa Mbunge wa Richmonduli.Rostam anaiongoza CCM kwa uhakika wa hali ya juu kwa kutumia Remote Control yake ya kitita cha Noti ambayo ni wana CC wachache sana wawezao kufurukuta mbele ya Remote hiyo.
Rais Kikwete ni Boya.
Wabunge wa CCM ni mihuri.
Wanachama wa CCM ni magharasha( Katata zisizo na thamani)
Chochote atakacho MH huyu hufanyika kwa nguvu ya Remote yake.
Remote ile si yake,wenyenayo wanajua kwamba si yake lakini wamempa uwezo wa kuitumia ili nao wapate kufaidi. Wanamlinda usiku na mchana kwa sababu taabu na mashaka yao ni juu ya remote ile na si mwenye uwezo wa kuitumia.
Wengi wataangamia na mahali pao patatoweka, hata wale wasiofaidika na matumizi ya Remote ile, kama muda apewao Rostamu kuitumia Remote ile hautafupishwa.
Bisha!
- Sikujua kwamba Rostam kuwa rais wa jamhuri, alichaguliwa na wanachama wa CCM peke yao na sio na taifa zima, Wapinzani included.
FMEs!
wanafalsafa hawawi wafalme!
Katika utaratibu wa kumsaidia mtu mlevi (kama aliyelewa madaraka) ujulikanao kama "Hatua 12). Hatua ya kwanza kabisa inamtaka mhusika kukubali kuwa ana tatizo na ya kuwa hakuweza kulikabili. NI hatua ya "kuown" your problem.
Hadi CCM itakapoanza hapa ndipo itaanza kweli kurudi kwenye misingi yake. NI vigumu sana kutoka denial kwenda acceptance. But slowly, watafika tu hata kwa kulazimishwa au kuanzishwa kauli.
"Hi, mimi ni mwana CCM, na Chama chetu kina matatizo!".
Wana CCM wote rudieni kauli hiyo hadi izame kwenye mitima yenu!
nafikiri cha maana ni je akismama na kuwakaripia CCM watamsikiliza? kama watamsikiliza na yeye anaridhika na hii hari ya taifa kwa sasa? maana yeye anatakiwa hawe amekea matatizo yote unless na yeye anafaidika na huu ufisadi.
Kwa mawazo yangu nafikiri Mzee Malecela hakubaliki tena ndani ya chama kwani mvuto unatakiwa sasa ndani ya chama hana, CCM sasa hiviinahitaji watu wenye pesa na ndio maana kama pesa huna hauthaminiwi na yeyote, ndio maana wanashindana kurundika mapesa kwa ajiri ya kutetea nafasi zao katika chama.
Wakuu
naomba mwenye maelezo yanayoweza kunisaidia anifaganulie ,Hivi kati ya wanasiasa hawa ni yupi anaweza kutamka neno kuhusu CCM tukalichukulia kama ndiyo CCM halisi bila kujali vyeo vyao ndani ya chama.
nauliza hivyo kutokana na kuchanganyikiwa baada ya kusikia matamko ya watu hao ambayo yamenixcha nikiwa kama kichaa bila kujua nichukue la nani.
nisaidieni jamani .