Jana nimekaa nikatafakari sana, na tafakuri yangu kwa kuangalia machapisho ya oganaizesheni mbalimbali baada ya kufanya tafiti zao pamoja na kuangalia upepo wa kisiasa nchini, nikaja na orodha ya hawa watu watatu....ambao kwa mtazamo wangu come 2015 mmojawapo ataingia ikulu.
1. Prof. Mark Mwandosya- utendaji wake na umakini unafahamika, kitaifa na kimataifa.
2. P.M. Mizengo kayanza Pinda- wote tunamfahamu ni mtu wa namna gani, mtendaji safi.
3. Edward Ngoyai Lowassa- kada mbali mbali zinakubali misimamo yake, na nia dhabiti ya kuleta maendeleo kwa kusimamjia uwajibikaji na utendaji uliotukuka.
Sina chuki wala nia mbaya kwa yeyote ambae sikumtaja ila nimeona nianze na hao watatu ambao nahisi kwamba wanayo nafasi kubwa ya kuingia ikulu.