Nani anafaa kuwa rais wa Afrika Mashariki

Nani anafaa kuwa rais wa Afrika Mashariki

Off course Kagame anaweza, ila ningependelea uwepo wa waziri mkuu wa Kenya katika upambanaji na rushwa, maana yule jamaa mtu ukishindwa kazi anakuja na karatasi halafu anaisoma hivi '' am here to suspend the following ministers for ......................'' halafu anaishia zake ndo amemaliza
 
Hapa kinyang'anyiro kizuri kitakuwa baina ya Paul Kagame na JK huu utakuwa uchaguzi wa kihistoria AM,hapa ninafikiri kijana Paul ataweza chukuwa kura na support zangu nyingi,mimi binafsi ninamkubali sana ingawaje bado ninatatizika na malengo yake mengi hususani mambo ya ukabila hilo ndilo tatizo langu na Kagame,lakini ataweza kutufaa sana AM tutafika mbali sana ,huo ndio ukweli wenyewe lazima tuukubali na kuuangalia kwa kina kirefu sana. M/Mpamba......Peace ...amahoro ,amani iwe juu yenu!
 
Hapa kinyang'anyiro kizuri kitakuwa baina ya Paul Kagame na JK huu utakuwa uchaguzi wa kihistoria AM,hapa ninafikiri kijana Paul ataweza pchukuwa kura na support zuangu nyingi,mimi binafsi ninamkubali sana ingawaje bado ninatatizika na malengo yake mengi hususani mambo ya ukabila hilo ndilo tatizo langu na Kagame,lakini ataweza kutufaa sana AM tutafika mbali sana ,huo ndio ukweli wenyewe lazima tuukubali na kuuangalia kwa kina kirefu sana. M/Mpamba......Peace ...amahoro ,amani iwe juu yenu!
wewe mwenyewe unasema kagame ni mkabila halafu unasema anafaa, kiongozi gani mzuri mkabila. you must not be serioue, kagame is simply a ruthless dictator. amemfunga yule mama wa kihutu ingavire jela simply kwa kutaka kugombea urais.
 
Hilo suala la ukabila linaweza linaweza kufanyiwa kazi na akajirekebisha,huyu jamaa tukubali au tusikubali ndio mtu atakayeweza kuja ondoa matatizo ya nepotism,corruption na ufujaji wa mali pamoja na kuwa ruthless lakini ataweza kugeuka kuwa kiongozi bora sana kwa AM na watu wake,tusumchukie mtu bila sababu yeyote ya kuingia akilini,Kagame ni mtu anaweza akawa ni patriot mmoja mkubwa sana wa AM na nimegunduwa pia ni forward thinker wa nguvu sana karibu anamkaribia rais wetu mstahafu Benjamin William Mkapa kwa kuona mbali,mnajua nini Mkapa kaifanyia nchi yetu wakati wa utawala wake.Nimemuita mkabila kwa sababu moja ya msingi,anajali sana watu wake anaowaongoza na kila siku anawatakia mazuri ndio kwa interpretation hiyo nimemuita ni mkabila hoja ambayo haina nguvu kwa mtazamo wangu.
Kumfunga mtu ndani ya nchi yake isiyo sababu ya kumnyima haki yake hapa,hayo ni mambo ya ndani ya nchi yake,hawezi kuyaingiza ndani ya AM kama watu kufungwa kwa maonezi au kwa sababu zisizo na msingi nasisi pia tunao watu wengi sana wameonewa wako jela bila hata sababu kama ya huyo mama wa kihutu,tunao watu kama akina Viking Nguza,kafungwa kwa case isiyokuwa na kichwa wala miguu case ya kubangikiwa mambo yasiyoingia akilini,sasa utawala ka huu utawezaje kuwatawala watu wa Africa mashariki,yaani maonezi matupu ndiyo nayaona hapa,kwa uchunguzi nilioufanya kuhusu Mr Paul K sijayaona maonezi kama haya ya kwetu.Peace M/Mpamba.End.
 
Ndugu wana JF. Nimewahi kuwasikiliza baadhi viongozi wa nchi za Afrika Mashariki akiwemo Paul Kagame. Kwa mujibu wa Kagame watu wa Afrika Mashariki wapo tayari kuungana kwa sababu tafsiri halisi ya umoja inaonekana kwenye utendaji na ushirikiano wao katika maisha ya kila siku. Kagame alieleza kuwa tatizo ni wao viongozi wanaofikiria nafasi zao. Nimewahi vilevile kumsikia Museveni, katika mazungumzo yake utaona kabisa kwamba yeye anajiona kuwa candidate sahihi wa kuongozawa AM kwa sababu aliachiwa jukumu la kuunganisha nchi zetu na akina Mwalimu. Mimi nimekuwa nikijiuliza kama AM itaungana leo nani kati ya viongozi wetu wakuu wa nchi anaweza kuwa baba wa taifa na rais wa kwanza wa 'The United States of East Africa ', tukizingatia rekodi kiutendaji na kukubalika kwao ndani na nje ya nchi zao.
AM ya Nini wapore Ardhi yetu
 
Huna lolote unajikomba kwake ili akupe Yule Binti yake mrefu uoe. Awe rais wa am Nyumbani kwako
 
Mimi nitajikomba kwa mtu ka yeye?wewe Ambagae wala hunijui mimi na unakurupuka kuandika eti sina lolote bali ninajikomba kwake,ndoto hiyo wala usiwe nayo na kama una chuki za binafsi na yule rais nakusihi uziweke moyoni mwako mwenyewe usizielekeze kwa watu hapa.Maana ya mijadala kama hii ni kila mtu anaandika mawazo na mitazamo yake kuhusu kila jambo,sasa wewe wacha kukurupukia mawazo ya watu na kutaka waandike kama jinsi unavyofikiria au kuona wewe.
Sasa wewe mtu mwenye lolote tafadhali tuwekee hoja zako ili tuone ni kwanini huyu jamaa hatufai AM kuliko kuandika bila kutoa hoja yeyote hapa,fikiri kabla hujakurupukia watu hovyo hovyo.Kumbuka huu usemi kama unakijuwa kweli kiswahili vizuri."Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni".Tafakari hapa,yule mtu kazi anaiweza ni lazima tukubali kuhusu hilo au umekasirika mimi kumlinganisha na rais Mkapa kwa uwezo wa kuongoza nini ?kama wewe ni mbongo kweli naamini unafahamu ka haya maendeleo karibu yote hapa nchini yaliwezeshwa na muishimiwa Benjamin Mkapa na ndio maana nguvu aliyonayo Kagame nimeilinganisha naye.So toa hoja na utajibiwa kwa hoja hapa.M/Mpamba.End.
 
Ndugu wana JF. Nimewahi kuwasikiliza baadhi viongozi wa nchi za Afrika Mashariki akiwemo Paul Kagame. Kwa mujibu wa Kagame watu wa Afrika Mashariki wapo tayari kuungana kwa sababu tafsiri halisi ya umoja inaonekana kwenye utendaji na ushirikiano wao katika maisha ya kila siku. Kagame alieleza kuwa tatizo ni wao viongozi wanaofikiria nafasi zao. Nimewahi vilevile kumsikia Museveni, katika mazungumzo yake utaona kabisa kwamba yeye anajiona kuwa candidate sahihi wa kuongozawa AM kwa sababu aliachiwa jukumu la kuunganisha nchi zetu na akina Mwalimu. Mimi nimekuwa nikijiuliza kama AM itaungana leo nani kati ya viongozi wetu wakuu wa nchi anaweza kuwa baba wa taifa na rais wa kwanza wa 'The United States of East Africa ', tukizingatia rekodi kiutendaji na kukubalika kwao ndani na nje ya nchi zao.
aNAYEFAA NI PROF. ANNA TIBAIJUKA NI MCHAPA KAZI SANA ANAFAA
 
Paulo kagame.jk labda awe wazir asiye na wizara au jinsia na watoto kwenye serikal ya kagame
 
Inategemea unataka kuwa na taifa lenye aina gani ya uongozi; kama ukabila, udikteta na kuua wapinzani, Kagame anafaa sana, kama demokrasia na maendeleo, hakuna kama JK
 
Back
Top Bottom