Ground Zero
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 342
- 95
Ndugu wana JF. Nimewahi kuwasikiliza baadhi viongozi wa nchi za Afrika Mashariki akiwemo Paul Kagame. Kwa mujibu wa Kagame watu wa Afrika Mashariki wapo tayari kuungana kwa sababu tafsiri halisi ya umoja inaonekana kwenye utendaji na ushirikiano wao katika maisha ya kila siku. Kagame alieleza kuwa tatizo ni wao viongozi wanaofikiria nafasi zao. Nimewahi vilevile kumsikia Museveni, katika mazungumzo yake utaona kabisa kwamba yeye anajiona kuwa candidate sahihi wa kuongozawa AM kwa sababu aliachiwa jukumu la kuunganisha nchi zetu na akina Mwalimu. Mimi nimekuwa nikijiuliza kama AM itaungana leo nani kati ya viongozi wetu wakuu wa nchi anaweza kuwa baba wa taifa na rais wa kwanza wa 'The United States of East Africa ', tukizingatia rekodi kiutendaji na kukubalika kwao ndani na nje ya nchi zao.