Nani amlaumu mwenzieee..........!!!!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani amlaumu mwenzieee..........!!!!!!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Ligogoma, May 29, 2011.

 1. Ligogoma

  Ligogoma JF-Expert Member

  #1
  May 29, 2011
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 2,135
  Likes Received: 849
  Trophy Points: 280
  Habari wan JF!!!

  Hapa ofisini tuna jamaa (mwanaume) kaajiriwa takribani mwaka sasa umeisha, wakati anahama kutoka alikokuwa (Singida) alikuja na mpenzi wake!

  Mpenzi wake huyu jamaa alikuwa anakuja kwa ofisi kumfuata mshikaji wake yaani full malovee! Ila cha ajabu baada ya kama miezi minne hapa wakagombana kabisa na jamaa likamtimua nyumbani yule binti ila akapata hifadhi kwa rafiki yake ambaye ni staff mwenzetu na alimfahamu huyu rafikiye kupitia mpenziwe wakati akija hapa kazini!

  Kiutani utani jamaa siku hiyo akaropoka `nimempiga chini yule demu.....` bosi wetu akamuuliza, upo serious umemuacha mtoto mzuri na mvumilivu vile? Kumbuka ulivyosota wakati unakuja hapa lakini kakuvumilia leo umeseto unamtosa? Jamaa halikujali likajibu tu ahaa atajua mwenyewe bana!!! Bosi wetu akaongea kiutani kuwa asijekulaumu!!

  Baada ya siku kadhaa yule binti kaibukia kwa bosi wetu, anamfuata kazini kama kawa tena bila woga na ninaposimulia hapa wamefunga ndoa mwezi mmoja sasa.

  Jamaa yetu anatamani kuacha hata kazi.....kachanganyikiwa yaani hatuelewi tumsaidieje wivu si wivu sijui alikuwa bado na mapenzi nae au inamuuma demu kuolewa hapa hapa tena na bosi wake...hatujui!!

  Kuna wanaolaumu demu kuolewa na mtu mwingine hapa hapa kazini kwa mpenzi wake wa zamani na kuna wanaomlaumu bosi wetu kuoa mpenzi wa zamani wa mfanyakazi wake na pia kuna wanaomlaumu staff mwenzetu kumpa hifadhi huyu binti mpaka bosi wetu akapata nafasi ya kuonana nae...yaani hapa vurugu tupu!!!

  Sasa wewe mwana JF kwa mtazamo wako, lawama zako zinakwenda wapi? na kwa nini?!!!

  Je! Huyu jamaa yetu aliyemtoa mpenzi wake hukooo mikoani na kuja nae hapa na baadae kuachana nae but binti kaolewa na bosi wake halafu binti ndo ana shine ile mbaya sasa hivi......Unamshaurije!!!????
   
 2. N

  Ndinimbya Senior Member

  #2
  May 29, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Lawama kwa mshikaji aliyemtoa mkoani. Kwanini aliamua kutangaza kumpiga chini wakati bado anampenda.
   
 3. S

  Sharo hiphop JF-Expert Member

  #3
  May 29, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 662
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Samaki hujua umuhimu wa maji anapofika pwani/nchi kavu, kipindi yupo na demu chali aliona afanye anavotaka, leo kabebwa anaumia.
  Mhhh!

  Alisemwambia boss wake kuwa dem atajua mwenyewe bana, sasa leo;
  na demu aseme msela atajua mwenyewe bana.
   
 4. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #4
  May 29, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  cuz love feelings never die, ingekuwa jamaa kaachana na mdada kistaarabu ningelisema boss anabeba lawama, lakini hiyo kuacha kwa mashauzi sijui "demu nimepiga chini blah blah blah" inanifanya moja kwa moja nimbebeshe lawama mshkaji alotoka singida, na infakt anadeserve hiyo punishment anayopata.
   
 5. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #5
  May 29, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Dahhhh hii story imelalia upande
  mmoja sana hapa tunamwona huyu kijana ndio mmbaya ..lakini na je binti alifanya nini kumtibua nyongo
  huyo kijana..

  mwezi mmoja kaolewa na boss
  mmmmhhhh hiyo sentensi hapo ina
  matata sana .. huu ndio mtazamo wangu..
   
 6. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #6
  May 29, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  Whatever the case jamaa hakuwa gentlemen, vipi utaachana na mpenzi wako halaf ukabwabwaje " nimepiga na chini dem wangu" sifa za kijinga zimemkosti..........ooops wait a minute, kumbe alikuwa ndo kwanza katoka kijijini. Ushamba unagharimu samtaimu.
   
 7. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #7
  May 29, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  kwa maelezo uliyotoa huyo kaka aliyetoka Singida ndo mwenye makosa,mpumbavu na mtoto...there is no point kwenda kutagaza decision inayowahusu wawili kwa ofisi.....nampongeza sana Boss kwa hatua yake ya kuona kilicho chema na kukifanya chake bila kukawia....nawatakia maisha mema na yenye baraka tele.AMEN!
   
 8. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #8
  May 29, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Watu wengine kweli wana midomo
  mikubwa kuliko akili zao..kweli sim
  tetei jamaa hata kidogo kwa kusema alicho sema ..

  lakini hii story inaundani zaidi angalia upande wa bosi na binti..
  na si tuliotoka kijijini tukianzaga
  kujua mji ni matata.. tunakuwa
  wataalum kuliko waliozaliwa hapo..

  si mlaumu yeyote mpaka
  tuwekewe upande wa pili
  wa hii story..
   
 9. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #9
  May 29, 2011
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,811
  Likes Received: 1,146
  Trophy Points: 280
  no way,mara nyingi wanaume huwa tunakosea hapo tu,hatujui ni nini tunakitaka,yeye kampiga chini demu wa watu na demu kakubali kisha kachukua bosi wake aendeleze makamuzi jamaa anachanganyikiwa nini sasa??hakujiandaa na wala hakujali alipokua anamuacha kwanini aumie akiona mwenzie kachukua mzigo jumla,hiyo imekula kwake yeye kama alikua anatingisha kiberiti mwenzie kakilipua analo hilo,alitaka baada ya kumpiga chini demu achooooke sana.sasa demu kamzidi kete anatapatapa,mwambie aache kazi kama vipi arudi kwao singida akauze kuku wa kienyeji:pound:
   
 10. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #10
  May 29, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Safi kabisa muosha huoshwa, acha binti wa watu ale kivulini, si alimtimua bila kujali ataenda wapi?hapo mwanaume alikuwa anatamani amuone msichana kafeli maisha yaani awe miserable
   
 11. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #11
  May 29, 2011
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,462
  Likes Received: 1,341
  Trophy Points: 280
  Mimi nawapa hongera tu hawa wanandoa wapya basi mengine sitaki kujua
   
 12. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #12
  May 29, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,673
  Trophy Points: 280
  Huyo jamaa ni ****,analeta mambo ya sizitaki mbichi,we unasema wanini wenzako wanawaza watampata lini,mwanamke ni malkia mtunze ipasavyo!
   
 13. Kitty Galore

  Kitty Galore JF-Expert Member

  #13
  May 29, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 347
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  naungana na wewe, ndoa yao idumu na iwe na faraja tele
   
 14. Ligogoma

  Ligogoma JF-Expert Member

  #14
  May 29, 2011
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 2,135
  Likes Received: 849
  Trophy Points: 280
  Kujua mambo yao ya ndani kiukweli ni ngumu maana jamaa haongei kuhusu hilo cha msingi jua tu kwamba waliachana jamaa akasema hivyo kwamba nimempiga chini demuu!

  Hapo za kwako changanya na zangu utapata jibu, ni hivi jamaa kaja takribani mwaka mmoja sasa baada ya kama miezi minne wakaaachana then iliyobaki ni miezi nane ambayo ndiyo wamespend na bosi maana haukupita muda wakaanza relation tangu walipoachana na jamaa. Wamefunga ndoa mwezi mmoja uliopita, hivyo hapo nilimaanisha ndoa yao ina mwezi sasa!!!

   
 15. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #15
  May 29, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Maana kilichounganishwa na Mungu! binadamu asikitenganishe, hata ukijadili haitabadilisha status ya huyo binti, jamaa ajitahidi a move on maisha mengi tu yapo yanamsubiria
   
 16. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #16
  May 29, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  hivyo ndivyo mabosi wote tunavyofanya lol
   
 17. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #17
  May 29, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Kumbe na wewe ndivo ulivyo lol
   
 18. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #18
  May 29, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Du imekula kwake.ukishare maisha yako na mtu umpendaye kwa muda fulani feelings lazima ziwepo hata kama mmetosana.washkaji tuache hii tabia ya kufukuza watoto wa watu huwa wanachukuliwa na mtu wa jirani alafu we unabaki unalia
   
 19. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #19
  May 29, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Jamaa ndio mwenye makosa.alipo mfukuza nyumbani alitegemea ataenda kupata hifadhi wapi? Manake wameamia wote kutoka singida hana ndugu hapo dar kwahio kumfukuza ilikuwa kuwafungulia njia watu wengine.


  Kafanya hasira za kijinga kumfukuza huku bado anampenda, sio kila kosa mtu uchukue hatua za kumfukuza mwenzako ndani ya nyumba.mnaweza kukasirikiana ndani huku mnaendelea kutatua tatizo lenu.

  Huyo dada hana kosa kwani wakati amefukuza hujui Msaada gani aliopata mpaka akatokea kumpenda bosi wenu kwa vile mapenzi uanza kwa sababu tofauti.
   
 20. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #20
  May 29, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hivi kazini wapi kunaongewa upuuzi wa hivyo kati ya boss na sub-ordinate. Bosi naye heshima zero.
   
Loading...