Nani amemroga Profesa Palamagamba Kabudi?

tangu siku ile ya mgombea binafsi simwanini huyu mzee
 

Alionja asali sasa ameamua kuchonga mzinga...Weee shilingi tamu jamani mzee kazoea chaki tu hakuna mheshimiwa wala nini mara kapewa sabuni ya roho na heshima kibao badala ya maswali chalenging toka kwa vichwa kule UDSM...Ukizingatia zile zinazotokana na kazi ya research; consultancy unazisotea mpaka mvi zinashindwa kusikilizana kwa jinsi zinavyo compete kila moja kuwahi kutokeza....Uwiiiiiiiiii hata mm karibu ntakuwa Pala mdogo nijilie maisha niachane na huu wehu wakila siku iitwayo leo kuimba kama kasuku miaka nenda miaka rudi the same development concepts and theories huku hao unao waimbia wakitoka madarasani wimbo wako wanauacha hapo hapo wenzako haoooo kusaka deal tu mawizarani pamoja na wanasiasa wao.
 
nawakumbusha kitu kimoja, kabla ya kuwa VC, Prof Mkandara alikuwa akifanya kazi Ikulu kama mshauri wa maswala ya siasa wa JK, na hii ilikuwa baada ya RDET inayoongozwa hadi leo na Prof Mkandara (MSIBISHE) kusaidia ushindi wa JK mwaka 2005. Alipopewa hisani ya kuwa VC na watu wenye akili zao kama Prof Mshana kuonekana hawana akili, Mkandara aliwaweka rafiki zake na wahaya wenzie katika system na mmoja wapo ni Prof Kabudi aliyempa ukuu wa shule ya sheria. na wote waliopewa nafasi na Prof Mkandara walikuwa automatically wateule wa JK na wanaokula matunda ya JK na kupata dili nyingi za serikali moja kwa moja. ndio maana Kabudi ametumiwa katika issue ya mgombea binafsi kwa manufaa ya CCM na kisha katika issue hii ya katiba mpya kwa manufaa yaleyale ya CCM na serikali. yapo mengi sana mfano Dr Ndumbaro ambaye alikuwa msaidizi wa Mkandara pale REDET sasa yeye ndo kapelekwa IKULU kula bata kwa kuwa mshauri wa JK siasa nafasi aliokuwa nayo mkandara kabla ya kuwa VC. kwa ufupi system, na fedha zimemroga Kabudi. sio yule kabudi wa zamni sasa. It's their turn to EAT, Mkandara, Kabudi, et al.
 
Vilaza wanajua sana kuchezea weledi, mwenye digrii amemlubuni Prof. mzima nae kaingia mazima mazima.
Kweli njaa haina baunsa
 
Tawala zote duniani hata zilizo mbovu kiasi gani zina watetezi wake. Prof. Kabudi ni mmoja watetezi wa aina hiyo. Uzuri ni kuwa historia ina tabia ya kuwahukumu vibaya sana wakati mwingine kwa kuwasahau kabisa.
 

Frankly speaking kuna mambo ya ajabu sana humo kwenye higher learning institutions na nashindwa kuelewa mtu msomi anakuwaje such short sighted kiasi hicho. Maana walikuwa wanalalamika hawapewi nafasi wakaamua kuwa wanasiasa; well and gud wengine wakawa mpaka mawaziri sasa ajabu ni kuwa serikali na bunge ambazo wamekuwamo zimekuwa the worst compared na wakati ambapo walikuwa wamebaki kwenye sehemu zao za kazi kitaaluma.

Wengi wanapoteuliwa ama kuchaguliwa ndiyo wamekuwa vinara wa kuingiza ndugu marafiki kwenye posts zingine zikiwa very sensitive...aise hawa wasomi ambao prof Baregu alitoa definition nzuri ya jina lao ni wabaya kuliko CCM yenyewe plus mafisadi wote. Maana wao wamekuwa kama nyundo inayotumiwa na wanasiasa uchwara kubomoa misingi mizuri ya nchi yetu.
 
...maana ya magamba inajulikana,na maana ya para si inajulikana? Huyo anaitwa PARA-MAGAMBA. Tafakari,chukua hatua!!
 

basi mlipo ondoka huku nyuma guru huyo alichaguliwa na kasisi wa ccm kuwa mkuu wa shule ya law, basi sahau vile naye amekuwa mchumia tumbo,ndiyo hivyo je atamaliza nyumba yake vipi.nawakilisha
 
Mkuu upo sahihi kabisa, mto hoja hakumuelewa Prof. Tatizo la watanzania wengi Kama ilivyo kwa mtoa hoja wanapenda kuyasikia yale wanayoyapenda tu!

Haya na wew unalipwa ngapi bwana mkubwa tuambie tujue
 
basi mlipo ondoka huku nyuma guru huyo alichaguliwa na kasisi wa ccm kuwa mkuu wa shule ya law, basi sahau vile naye amekuwa mchumia tumbo,ndiyo hivyo je atamaliza nyumba yake vipi.nawakilisha

njaa inaua hata ndugu hivi kale kamjengo kake changanyikeni hajakamaliza mpaka waleo???duu
 
Tawala zote duniani hata zilizo mbovu kiasi gani zina watetezi wake. Prof. Kabudi ni mmoja watetezi wa aina hiyo. Uzuri ni kuwa historia ina tabia ya kuwahukumu vibaya sana wakati mwingine kwa kuwasahau kabisa.

Ni kweli, historia huwa haina haja na wale wote wenye kushindwa,
labda tu kunukuu tarehe walizokutwa na umauti wao...
 
 
haa haa haa haa haa ite ite ite!!!!!!!!!!!, kwa namna ulivyo lichambua jina lake na thubutu kusema pamoja na uprof wake, unamzidi busara, hekima. na maarifa.

kwa namna nilivyo muona sure anatafuta mkate sijui anabembeleza awe amrithi Prof. Mkandala wa udsm
 

Wakimbizi utawajua tu,we ni mmojao maana hawana uchungu na nchi ambayo siyo yao.We fikiria watu kama akina RA atakuwa na uchungu na hii nchi saa ngapi.Sisi wenye nchi yetu tunauchungu sana so hatutaki manyang'au na wanafiki watuharibie nchi
 
huyu jamaa Ndo Anayeforce Ishu ya law scul anasema kama huna pesa ya lawscul nduguzo wakuchangie. Ni mtu wa kwanza na wa mwisho kupata gpa ya 4.8 Law ana masifa. Ndo aliyedraft mswada wa kwanza . Mh kikwete ndo alimtaja huyu kuwa mwanasheria maarufu Huyu jamaa AKA MC WA IKULU
 
Prof. Palamagamba kabudi



Hii ndo SOurce ya NENO GAMBA

Mkuu nimecheka kweli lol! yaani umenikumbusha falsafa ya kuvua gamba na ukifuatilia maana ya neno 'PALAMAGAMBA'='KUTOAMAGAMBA'. Ila sitaki kuamini kama kuna uhusiano na falsafa hiyo.

Hakuna kitu kibaya kama kukosa uhuru wa kusimamia kile unachokiamini na huo ni utumwa mbaya kuliko ule wa kuwekwa ndani au shambani kumlimia master. Ninakuhakikishia kuwa si Palamagamba, Kombani, au Werema wote wanaamini kuwa muswada huu ni FLAWED AB INITIO, Ila kwa kuwa wanamtumikia kafiri wacha wapate mradi wao.

The only thing can rescue these people from Kafiri ni kuwapa pressure ya umma ambayo wataitumia kujitetea mbele ya kafiri huyo kuwa walikuwa hawana jinsi zaidi ya kuachana na masilahi ya kafiri huyo na kutumikia waumini (Watanzania). Vikao vya ndani vya CCM vimeweka wazi kuwa katiba mpya itokanayo na watanzania ni one way ticket out of power, hivyo basi kwa kuwa hakuna anayeweza kumvisha paka kengere si JK wala Werema ni dhahiri wanachofanya sasa ni firewall against any attack from CCM Tycoons that they save them. Tukikaa kimya na kukubali kutomaswatomaswa tunakofanyiwa sasa basi tukijikuta wajawazito tusimlaumu mtu. We need to show them that what they are doing is not of national interest, they should either rescind the process or take the right path, the path of inclusiveness not monopoly.
 
Kwanza katika mazungumzo yake yote ya kuutetea mswada alijua anaongea uongo kwa sababu alikuwa anajiwekea kinga kwamba wananchi tusimuelewe vibaya,tusipinge kila kitu ,tutakosa tunachokitaka kama hatutauukubali haya si maneno ya kitaaluma na yanayoshawishi watu tuweze kufahamu nia ya serikali alikuwa amejiandaa kuuutea kwa nguvu zake zote
 
 
Kwa hili alilolifanya Magamba Kabudi,sina hamu na wasomi wa Tanzania,kwani uwezo wake wa kufikiri una tofauti gani na wa Professor Maji Marefu?sikuamini hicho kilichokuwa kinatoka kinywani mwake na kutamka mbele ya wa-TZ wengi walioangalia TV.
kama ni hivi silaha pekee ya kuikomboa nchi hii ni nguvu ya umma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…