Khantwe
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 59,410
- 119,115
Wanadai mitungi yao inatumia card na inapatikana kwa elfu 95 (hii ni pamoja na jiko la plate mbili)
Unaweza kulipa kwa mkupuo au ukaanza na deposit ya 30,000 kisha utakatwa asilimia 15 kila utakapokuwa unanunua gas (bei ya kununua cash ni sawa na bei ya mkopo)
Unapewa mtungi uliojaa gas ila ili uitumie unatakiwa ulipie kuanzia 1000 na kwa pesa hiyo unapata unit nane, gas ikiisha kwenye mtungi unajaziwa bure. Hakuna limit ya muda ni wewe tu na ulipaji wako hadi utakapomaliza deni lao la elfu 65.
Wanasema when the deal is too good think twice. Kuna mtu ametumia hii? Nahisi kuna zaidi ya haya ambayo hayasemwi.